KWELI Ubandikaji wa Kope na Lenzi Bandia machoni unaweza kusababisha Upofu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
768d3290-8664-11ed-90a7-556e529f9f89.jpg

Kuna dada zetu wanapenda sana urembo hivyo kujiongezea baadhi ya vitu kama matako, kope, lenzi kwenye macho, matiti vimekuwa vitu vya kawaida sana kwao. Ukweli hayo yote wanayojiongea yanakuwa na madhara.

Mimi nipende tu kutoa hadhari kuwa kope na lenzi bandia mnavyojiongezea ni hatari kwa afya ya macho yenu. Chonde chonde ridhikeni na mlivyoumbwa navyo.

Khadija Omary ni mmoja wa wahanga wa kupofuka baada ya kuwekewa kope bandia.

Ni hayo tu.
 
Tunachokijua
Wanawake wanaopaka wanja chini ya macho na wale wanaobandika kope bandia, wapo hatarini kupata upofu.

Madai haya yaliwahi kuthibitishwa na Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Huduma ya macho, Dk. Bernardetha Robert, wakati akizungumza kwenye kilele cha siku ya afya ya macho duniani, Oktoba 18, 2018.

Dk. Bernadetha alisema wakati wa uwekaji wa kope bandia, huwa kuna maji maalum ambayo yamekuwa yakitumika kugundishia karibu na kingo ya jicho.

Alisema maji hayo yana madhara makubwa na wanawake wengi wamekuwa wakipata madhara ikiwemo macho kuvimba na wakati mwingine kushindwa kuona huku sababu hiyo na ile ya kupaka wanja karibia na macho, zimekuwa ni mojawapo ya sababu ambazo zimekuwa zikichangia upofu.

“Wanawake wengi wanakuja kwetu macho yakiwa yamevimba sababu ni wanja na kope za bandia, tunawashauri kuacha matumizi hayo na jicho linatakiwa muda wote liwe safi hasa sehemu za nje ya jicho

Dk. huyo alisema bado jamii ya kitanzania haizingatii vyema utunzaji wa afya ya macho, hivyo aliwaasa kujenga utaratibu wa kupima angalau mara moja kwa mwaka.

“Tusinunue dawa bila ya kuandikiwa na daktari. Tusipake ama kubandika vitu vigeni kwenye vifuniko vya jicho ama kingo za vifuniko vya jicho kama vile rangi. Tusivae miwani bila kupimwa na mtaalamu wa macho” alisema Dk. Bernardetha.

Tahadhari kama hii iliwahi pia kutolewa na mratibu wa huduma ya macho ya mkoa wa Iringa, Dk George Kabona, alipokuwa akitoa tathmini ya huduma ya macho ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya afya ya macho duniani mwaka 2016.

“Ningependelea wasipende kuzivaa kama fasheni ya kawaida,kwasababu zina madhara sana. Kwasababu hizo kope unabandika kwa kile kitu ambacho ile chemical ya kubandikia ndio huwa inaogopwa zaidi kuliko hata kope zenyewe. Ingekuwa labda unazibana na stapler hivi labda lakini kuna kitu unabandikia ile kitu ndio jicho halikitaki kama kinaendelea kukaa pale muda mrefu,”alisema Kabona.

“Pia hupelekea uoni hafifu. Pia linaweza likawapelekea watu shida ya kuona kwasababu uoni hafifu kuna ule mkali na uoni hafifu wa nafuu. Ukiwa ule mkali utakuletea shida kwenye shughuli zako za kila siku. Ukiwa katikati kama unaangalia TV, ukiwa unataka kumuona mtu unasogea maisha yanaweza yakaendelea. Lakini kuna ule mkali kabisa unakaribia na upofu unahitaji huduma.”

Kope bandia zinaweza pia kusababisha maumivu, kuvimba na mzio wa macho.
Sasa mdada unahangaika kubandika hivyo vyote wakati sisi tunachohitaji ni "pruuuu mpaka Makkah thing" tu kwenye mwili wako
 
Je unafahamu kuwa Ubandikaji wa Kope husababisha Upofu?

Katika jamii yetu, mjadala wa urembo umechukua nafasi kubwa, na baadhi ya dada zetu wanapenda kujiongezea vitu kama vile, kope, lenzi kwenye macho wakiamini kuwa hivyo wanavyojiongezea kunawafanya kuonekana warembo zaidi. Hata hivyo, inasemekana kuwa vitendo hivi vina madhara makubwa kwa afya.

Wataalamu wa afya wamebainisha kuwa wanawake wanaopaka wanja chini ya macho na kubandika kope bandia wanaweza kuwa katika hatari ya kupoteza uwezo wao wa kuona.

Wamebainisha kuwa wakati wa kuwekewa kope bandia, gundi inayotumika kugundishia karibu na kingo ya jicho huwa na madhara makubwa. Hii inaweza kusababisha macho kuvimba na hata upofu.

Kwa hiyo, ni muhimu kwa jamii kuchukua tahadhari na kuepuka vitendo vinavyoweza kuathiri afya ya macho.

Kwa taarifa nyingine kama hii tembelea jukwaa la JamiiCheck lililopo ndani ya JamiiForums.com​
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom