Hali si Shwari kati ya DC, Madiwani na Watendaji Wilayani Mkuranga

The Thugs001

JF-Expert Member
Sep 13, 2018
425
914
Hali ya sintofahamu imetokea Mkoa wa Pwani,Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga baada Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu Chakoma kupokea zuio kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Khadija Nassir Ali la kutopokelewa vifaa vya Afya alivyokuwa amepeleka katika kituo cha Afya cha Msorwa.

ikiwa ni katika juhudi za kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo Diwani wa Kata ya Mbezi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Rashid Selungwi kwa niaba ya madiwani wenzake alionesha msimamo wake wa kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya madiwani wenzake na kusema kuwa vifaa hivyo watavipeleka katika ngazi za juu za CCM kuwaeleza kadhia hiyo iliyowakumba.

Aidha Selungwi amesema imekuwa muendelezo wa mkuu huyo wa Wilaya kuingilia majukumu ya watendaji kwa kuwakataza mambo mengi.

Taarifa kamili tembelea YouTube channel ya ManaraTv
 
Back
Top Bottom