Iliwahi nitokea..nimerud toka job nikasalimiana na watoto..na mbwa wangu pia..nikauliza watoto mama yenu yuko wapi! Wakajibu ameenda kwa mama Nalieth(jiran)..badae akarud..hakusalimia akaingia ndani .nikamfata nikamsalimia tena akanyamaza. Nikamuuliza kwa nn huitiki salam..bila kutegemea akaniambia malaya zako waite wakusalimie kisha akanitukana tusi kuubwa na akamalizia kutukana kutukana kabila langu..nikamwangaliaa ..akafokaaa kama nusu saa, anatukana tu.
Nikachukua taulo nikaingia bafun..nikiwa bafuni hasira zikanijia..hasira kali .nilipomaliza nikatoka bafuni. Nikavaa..ile hasira niliyokuwa nayo nikasema nikipiga huyu mtu ntamuua .nikawasha gari nikaenda kulala kili golf kwa siku sita ..nilliporejea wala sikusema kitu nikaa kimya..nikalala chumba cha wagen kwa miez mitatu..ndan ni kimya..alikuwa anakuja analia mlangon usiku kucha na kiomba msamaha..ooh mama nalieth alinidanganya mume wangu.. mie wala..niko kimya tu anaomba msamaha mie kimya. Akakondaaa mie wala. Sili chakula chake. Siogi maji yake..najifulia . Najinyoshea..
Siku moja narud toka job ile nimepak akaja akaanguka pemben mwa gari anaomba msamaha. Nikamruka nikaingia ndan..akakaa hapo nje amelala had saa saba usiku..mie wala kimya tu...
Akashitak kwa kaka yangu..kaka yangu akaniuliza..nikajibu muulize yeye...
Aisee nilimpa teso moja matata sana had mda ,majira na wakat mwafaka ulupowadia nikamuita nikamwambia neno moja tu SIPENDI KELELE na usirudie ujinga..had leo ana adabu zote..