Katika comment za huu uzi na nyingine zenye aina hii ya maudhui ya kuongelea changamoto za wanaume kuishi na wanawake, huwa kuna Mambo yananipa wakati mgumu sana kuyaelewa.
1. Mwanamke huwa anachukuliwa kuwa anachofanya ni factory default yaani ni asili yake na si jambo la kutakiwa kujirekebisha. Ila mwanaume anaporeact kutokana na anachofanyiwa inaonekana mwanaume ni mkosaji na aliamua kwa utashi. So jamii inajisahaulisha kuwa hapa kuna swala la accountability kwa mkosaji na sio mkosewaji.
2. Jamii imeshajiaminisha kuwa mwanamke automatically ndie anaeonewa.
Visa anavyofanya mwanamke kwa mwanaume wake huwa vinakuwa over looked, katika macho ya jamii huchukuliwa kama ni sehemu ya haiba ya mwanamke kimapenzi na sio mwenendo mbaya wa tabia zisizotakiwa katika mahusiano yenye afya.
Mfano kulalamika, kulaumu, kutotii maelekezo, kudai matumizi yaliyo nje ya uwezo wa mwanaume, kutosaidia mwanaume anapokuwa hayupo vema kifedha na kadhalika, wivu kupitiliza, ubinafsi, haya yanapofanywa na mwanamke, jamii husema ni sawa ila huwa hayachukuliwi kuwa ni sehemu ya emotional abuse ambayo ikiendelea kwa muda mrefu hujenga kisasi ambacho matokeo ni matukio ya ukatili.
Suluhu ya jamii utasikia, 'KAMA UMEMCHOKA SI MUACHANE AU UONDOKE' . Hivi ukae na mtu miaka zaidi ya 10 au 20 halafu uachane nae kirahisi tu na umeshainvest maisha yako kwake na mna hadi watoto sababu anashindwa tu kubehave na kuacha aina fulani ya mienendo yake ili muwe na amani.
3. Why accountability huwa ni kwa mwanaume tu wanawake wanakuwa treated kama victims. I mean mwanamke anaweza kuwa na mwenendo ambao ni psychologically toucher kwa mwanaume na mwanaume akavumilia kwa muda mrefu akiathirika kifikra na hata afya ya mwili. Ila kwasababu haya hufanyika ndani hakuna atakae jua mwanamke ni mkorofi. Ila moment mwanaume atapoanza kujihami shida itaanza hapo. Jamii itaanza kuona mwanaume mkorofi.
Mwanaume unadaiwa kodi baada ya mwezi, ada ya mtoto bado haijaisha, umeme unit zimebakia 10, king'amuzi kinakaribia kukata, madogo wanakucheki wanataka sapoti , wazazi haujawacheki uwatoe kidogo maana umri wao umeenda wanakuhitaji, gari inahitajika service, halafu mwanamke wako anakuja pembeni anakusomea list ya vitu vya ndani vinakata , gesi, mchele, sukari, mafuta ya kupikia, umeme, na anataka pesa ya saloon, na sim yake anataka iwe replaced na mpya.
Haya anakwambia huku amekutumbulia macho bila hata chembe ya huruma kuwa huyu mume wangu ni mtu kama mimi, kuna kuzidiwa majukumu hebu nimsikilize anatakaje ili tuokoe jahazi. Ukitaka space ili ufikirie namna ya kutatua haya yote kwa maana hakuna msaada kutoka kwake, anaanza kuleta hisia za kuwa una msaliti na kununa bila sababu. Katika hali kama hii hivi mwanaume anaanzaje kumuona mwanamke ni baraka kwake kama sio mikosi juu ya balaa?!
Hebu kama wanajamii kwasasa tuanze kubalance swala la "Accountability" kwa wanawake pia. Kuna matendo yanafanywa na Wanawake ambayo huwa ni maumivu katika maisha ya mwanaume kwa namna ambayo jamii huwa haijui au imeamua kuchukulia poa, ila baada ya mwanaume kufika breaking point ndipo jamii huanza kutazama na kutuhumu kuwa mwanamke anaonewa.
Imagine situation kama mwanamke kutoka nje ya ndoa sababu mume hamudu kumpa baadhi ya mahitaji. Mwanamke kumpandishia mwanaume sauti na kuleta kiburi kisa tu mwanaume anapitia hali tete ya kiuchumi na kushindwa kumudu baadhi ya gharama, why hivi huwa vinachukuliwa normal, halafu huyu mwanaume akipata unafuu wa maisha akamudu gharama mwanamke ndipo anajirudi tabia wakati mwanaume tayari ameshakufa ganzi moyo hauna tena mapenzi na mkewe. Anajikuta anatafuta mwanamke wa nje ili akapate upendo mpya utaompa sababu ya kufurahia dunia.
Tuanze kuaddress changamoto za wanawake na kuwawajibisha kwa wakati. Midomo inawaponza sana wanawake. Huwa hawaogopi impact ya maneno yao kwa wanaume zao. Huwa wanafocus katika kutoa hasira vifuani hasira ambazo mara nyingi ni zao la kutumia akili ndogo katika mambo yasiyohitaji kukurupuka au kushirikisha akili za marafiki zao vilaza wadangaji wa mjini kuhusu mambo ndoa.
Nenda madawati ya jinsia ya vituo vya polisi, utastaajabu kukuta askari wa kike watakayokwambia kuhusu Wanawake wenzao sababu baada ya kuwabana na wao kusema ukweli wameona shida chanzo kipo wapi.
Hii habari ya kusema mwanamke ni kiumbe dhaifu hata sisi wanaume ni viumbe dhaifu vile vile.