Wanawake acheni kuvaa mawigi

Wanawake acheni kuvaa mawigi

Kuna wale Team Mawigi sugu hata ukiwaletea habari za google wataona kama unawazingua, labda mpaka wao wenyewe wakutane nazo wenye maombi

Huwa napata shida sana kuwaza unawezaje kusimama na kuanza kumshukuru Mungu kwa uumbaji wake halafu kichwani umemkosoa kwa kuweka vitu ambavyo yeye hakukuumba navyo. Unakuta midude migumu kwa ndani mtu kashonwa na nyuzi kichwani yaani kisa fashion halafu ngoja uzi uachie bahati mbaya huwa nacheka sana kwani wengine niko nao ofisini mara ooo naomba nirekebishie
 
Wamekubali, after all mawig mnavaa mtuvutie, na sis hayatuvutii Tupa Kule, kuwa simpo tu,
 
Mwanamke anapendeza na kuvutia zaidi anapokuwa na nywele zake za asili wala sio mawigi. Hiyo ni FACT.

Mawigi yanaboa na yanatupunguzia hisia, mfano pale mwanaume unavyozishika au kujaribu kuzichezea halafu unajua kabisa hizi nywele sio.

Ni kama likofia fulani hivi linalovaliwa au kushonwa kichwani kwa mwanamke, ambayo pamoja na kwamba KIUHALISIA halimuongezei mwanamke mvuto (hata kama ni la Laki Moja), linatakiwa libadilishwe kila baada ya muda fulani.

Wanawake bakini na nywele zenu za asili, zipeni matunzo na usafi wala hamna haja ya kuhangaika na kubadilisha mawigi maana wanaume {99.99%} hatuzipendi. Zinaboa hata kuangalia.

Cha kushangaza, utamkuta mwanamke wa kibongo eti naye anahangaika kuweka liwigi lake vizuri kanakwamba linamzuia kuona vizuri wakati ni FAKE HAIR na yeye mwenyewe kaliweka hivyo kwa makusudi kuiga Wazungu.

Say NO to Fake Hair.

Duh aise,nimeupenda uzi huu.
 
Wewe Sonko, Jr umeleta mjadala mzuri sana. Kwa kweli wazungu ni 'washenzi' kweli kweli. Yaani wanatuletea mawigi eti tufanane na wao. Nashukuru mke wangu havai mawigi ila mabinti zangu weeee ni shida. Sijui sisi waafrika tukoje. Nikiwaambia mabinti zangu ambao nawamudu majibu yao hunikatisha tama. Yaani utasikia wanasema wewe baba sisi tunakuheshimu na tunakupenda na umetusomesha ila tunakuomba utuache na haya mawigi kwani ndiyo mambo ya kileo...huwa nabaki nashangaa. Angalau nashukuru jambo moja. Mabinti zangu hawajagusa mikorogo. Yaani jamani mikorogo ni shida kuliko mawigi. Mimi niliwaambia mabinti zangu kuwa wakianza mikorogo nachukua panga na kuwashughulikia sitaki ujinga huo.....
 
Mawigi kwa mwanamke ni kerooo kupitiliza,mwanamke hata akinyoa au abaki na vipilipili inavutia zaidi kuliko kuvaa mawigi.
 
bhaaaasss! mie mwenyewe kichuna nipo naturaliiii, staki shida!
 
Mimi kila siku ndo ugomvi wangu na wife, ijapokuwa ana nywele ndefu nzuri na nyeusi lakini bado na mawigi sijui maweaving hata simwelewi hawa wanawake wetu ni shida
 
Wewe Sonko, Jr umeleta mjadala mzuri sana. Kwa kweli wazungu ni 'washenzi' kweli kweli. Yaani wanatuletea mawigi eti tufanane na wao. Nashukuru mke wangu havai mawigi ila mabinti zangu weeee ni shida. Sijui sisi waafrika tukoje. Nikiwaambia mabinti zangu ambao nawamudu majibu yao hunikatisha tama. Yaani utasikia wanasema wewe baba sisi tunakuheshimu na tunakupenda na umetusomesha ila tunakuomba utuache na haya mawigi kwani ndiyo mambo ya kileo...huwa nabaki nashangaa. Angalau nashukuru jambo moja. Mabinti zangu hawajagusa mikorogo. Yaani jamani mikorogo ni shida kuliko mawigi. Mimi niliwaambia mabinti zangu kuwa wakianza mikorogo nachukua panga na kuwashughulikia sitaki ujinga huo.....

Mikorogo noma. . Sasa ukute mkorogo umekolea, wig hizo bangs mpaka haoni mbele, utachoka
 
Mi sipendi ila ndo hivyo nimekubali yaishe, maana mna sababu lukukiiiiiiiii
Mara nachoka kusuka, mara nakosa muda wa kwenda saluni, mara nachoka kuandaa nywele asubuhi, mara sijui nini daaah, basi bwana ntafanyaje sasa!!! make unalazimishwa kupenda usichopenda

Hahaha my kaka bana, but wifi akinyukaga weaves zake si huwa unamsifia hata kimoyo moyo au?
 
Hata mumwange povu kiasi gani maweaving na wigi zitavaliwa tu na wanawake as long as wana exist on planet. Kama hamjui hata wazungu hutumia weaving
 
Wamekubali, after all mawig mnavaa mtuvutie, na sis hayatuvutii Tupa Kule, kuwa simpo tu,

Nani kakwambia wanawake huvaa au kujiremba kwa akili ya kuvutia wanaume. Hyo perceptions yako ni wrong
 
Hata maua yanapendeza na harufu tamutamu, kuita nyuki, ili uchavushaji a.k.a uzazi uendelee, we unampendezea Nani kama sio sisi?
 
Hahaha my kaka bana, but wifi akinyukaga weaves zake si huwa unamsifia hata kimoyo moyo au?

Siyo kimoyo moyo namsifiaga kiwazi wazi ila ndo hivyo kinafiki, coz mnalazimisha hayo madude wanaume wengi hatuyapendi, hope umeona mwenyewe walivyotiririka humu

Mnayapenda nyie kwa nyie tu kwa kweli
 
Siyo kimoyo moyo namsifiaga kiwazi wazi ila ndo hivyo kinafiki, coz mnalazimisha hayo madude wanaume wengi hatuyapendi, hope umeona mwenyewe walivyotiririka humu

Mnayapenda nyie kwa nyie tu kwa kweli

Hahaha my kaka buana, kwa nini kusifia wakati roho haipendi teh
 
Back
Top Bottom