Flexi lady
JF-Expert Member
- Nov 14, 2014
- 298
- 208
Yaan mi naona heri kuvaa wigi kuliko mvuta sigara
Mimi ni mwanamke but nimejikubali usichana wangu mpaka naolewa hayo makitu siyapendi huwa napata shida kufikiri joto la Dar na hayo makitu kichwani, kwa joto hili napenda nilifika home nywele yangu maji yapite nipate kujisikia raha na mume wangu huwa ana enjoy kushika nywele zangu
njija , kuna ukweli wowote kuhusu analosema PesaNdogo ?Nawajua wadada wa hivyo, wako kibao. Wengine wanatafuta kiki kwenye majadiliano.
Yeye hapendi, wanaweka hawamhusu
Tena huyo ni bingwa sijui wanawake walimfanyaga nini, hanaga jema juu yao.
Kuna siku nilicheka sana nilimwona binti mmoja alikuwa amevaa hayo makitu iko kama kofia flani ss alikuwa ktk piki piki amepakiwa na kofia ya usalama amevaa, sasa wakt anavua yale makitu yakavulika hiyo mibutu sasa kichwani ilikuwa ni shidaaa.
Teh teh..Unachezea nywele unakutana na milima,mabonde na mibinuko isiyoeleweka..Hadi stimu zinakata
We ndo umepaniki, kuja kulalamikia mawigi ya mwanamke, kama ulikuwa hujui sio mara zote wanawake wanajiremba kwa ajili ya wanaume hiyo ni psychology ya wanawake... They are competitive among themselves.
Hata ningekuwa nimelivaa wewe halikuhusu, hata liwe la kijani teh teh
Huo ni mtazamo wake siwezi mlazimisha kila mtu akawa na mtazamo kama wangu but mimi kukaa hata siku mbili na mijasho ya Dar siwezi hapa ntaambiwa mambo ya fashion ila kwa fashion hii nilikwisha kubali inipite.
Naomba tuwe wakweli kabisa ķwa joto la Dar na jinsi watu tulivyo busy na maisha, muda ni mdogo sana, sana sana mtu ataenda weekend kusafisha wigi lake hebu tujadili mijasho ya siku mfano 3 tuu huko kichwani kweli kaharufu kana kwepeka?
Fashion wapi? Kuna mabalaa wanaficha vichwani
Wengine usafi kwao ni shidaaa
Naomba tuwe wakweli kabisa ķwa joto la Dar na jinsi watu tulivyo busy na maisha, muda ni mdogo sana, sana sana mtu ataenda weekend kusafisha wigi lake hebu tujadili mijasho ya siku mfano 3 tuu huko kichwani kweli kaharufu kana kwepeka?
unakuta mtu analijali Wig na kulifanyia usafi kuliko hata anavyoitunza papuchi yake...
Kumbe ndio zake eeeh,
Ngoja....
I wish wanaume wangeelewa kuwa sio wanawake wote wanafanya mambo kwa ajili yao. Mfano huwa tunaenda kwenye kitchen party. Je huwa tunajiremba for what! Somethings are intended only for women domains! (Japo sikatai kuwa kuna wengine wanafanya kwa ajili ya wanaume)
Tuachane tu kila mtu aishi maisha ayatakayo ikiwa hajavunja sheria.
Nafikiri mleta mada asitulazimishe kuacha tuyafanyayo, bali aombe tufanye kwa kiasi na professionally, mtu umepaka make up yako kwa proffesinal makeup artist, umetengeneza nywele nzuri, unakuwa smart and confident. Basi tu tatizo labda yale mawigi ya uswazi na makeup za uswazi, lakini pia mhusika akiwa sio mkeo kwanini ujali?
Duuu jamani unawaonea sasa.
Team Mawigi inabidi muelewe kuwa wanaume 99.99% hatupendi na hatuvutiwi na Fake Hair.
Wanawake wakifanya kila wanaloweza kufanya na nywele zao za asili wanapendeza na kuvutia zaidi.
Teh teh..Yani sometimes unakuta msichana anageuka kuangalia upande mwingine ila wig limebaki straight tu..halijafwata direction ya kichwa...