Wanawake 1,000 wafunga siku 3, wamuombea Dr. Magufuli

Wanawake 1,000 wafunga siku 3, wamuombea Dr. Magufuli

Wenye roho mbaya, wivu na chuki wanapo isikia hii habari wanatamani kupasuka
Teh! Teh! Teh!
 
WANAWAKE 1000 WAFUNGA SIKU TATU, WAMUOMBEA DK MAGUFULI

Wanawake zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumuombea Rais John Magufuli huku wakiwa wamefunga siku tatu mfululizo.
Pia wanawake hao wanaoiombea nchi amani na kuiepusha jamii na mmomonyoko unaodaiwa kuwa sababu ya kuongezeka maovu ikiwamo ufisadi na mimba mashuleni....http://www.mwananchi.co.tz/…/1597578-4026338-131…/index.html

Watu washaanza kuwa INDOCTRINATED ............. siyo bure!!
 
Wanaacha kuwaombea waume zao,wanamuombea mume wa mwenzao,akili matope,kama nu mke wangu siku hiyohiyo angeondoka amfuate

Sent using Jamii Forums mobile app
hata wakifunga mwaka mzima magufuli keshasema hakuna mtoto wa kike atakayepata ujauzito halafu aendelee na shule. nashauri waendelee na shughuli zao

Captain John Komba hakukosea kutunga kale kawimbo ka "Na mvimbe mpasuke....., Mtajiju wenyewe......"

Mtapasuka kwa kumchukia Magufuli
 
Wanawake 4,000 wakutana Ruvuma kula na kufurahi kwa kumpata Tundu Lissu kuweza kuzungumza ukweli wa kile kinachoendelea nchini. Wanawake hao wameshangaa kuona wanaume wote wamekuwa waoga kiasi cha kumuachia Tundu Lissu tu kuweza kupambana na goliathi. Wameapa watazunguka nchi nzima kuhakikisha wanahimiza wanaume na wanawake wa nchi nzima kuaacha kuogopa kukemea ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi kwa kisingizio cha kuleta maendeleoa. Pia wametaka wakulima nchini kusimama kidete kwani wakulima ambao ndio wananchi walio wengi wanaendelea kuwa masikini kwa kitendo cha serekali kutokujali sekta hiyo inayobeba wananchi wengi. Wemesema wanashangazwa sana wanaposikia kuna kiongozi anayepigania wanyonge huku akipunguza bajeti ya kilimo kwa kiwango kikubwa na kulipa jeshi hela nyingi kupambana na upinzani. Hawakuishia hapo bali walisema wanashangaa kiongozi wa wote kutumia nafasi ya kufungua miradi ya maendeleo ya kodi toka wananchi wote kufanyia chama chake siasa za wazi huku akigomea vyama vingine kufanya kazi zao za kisiasa kwa mujibu wa katiba. Wanawake hao watagawanyika katika makundi sita kuzunguka nchi nzima kueneza ujumbe usemao "madai ya maendeleo isiwe kisingizio cha uonevu na kunyima uhuru wa kujieleza kwa wenye mitazamo tofauti"

NB: Hapa tunakosoa kistaarabu bila kejeli wala matusi.
FAKE NEWS
 
Afadhali wafunge kwani Mungu atajibu maombi yao .Ila wasilalamike.Wasome kitabu cha Daniel au Ester pale watu walipomloloa Mungu kwa kifunga kama taifa alitendi haki umwadhibu Mkuu.Yangu macho tu
 
Wana waume kweli hao !!?? Maana huyo mume wakumuaga siku tatu kwenda kufunga na kuombea mtu .na yeye binafsi ujawahi kufunga na kumuombea .labda mume suruale tuu huyo itakuwa kama yupo !!
Wanaume wa kiroho wanaelewa mkuu.Kwa wanaume wa kipagani hii ni ngumu kuelewa na kumeza, kwa kuwa mafahali" wawili hawakai nyumba moja.Sijui kama utanielewa mkuu.
 
kuna wenzao walioolewa na wafanyakazi hususan walimu wanasaga meno kutokana na waume zao kutopandishwa madaraja wala nyongeza yoyote kwenye mishahara yao. Mungu mwenyewe anajua ni wepi atawakubalia dua zao
 
Wanawake hao watakuwa wamekodiwa ,mbona sijaona aliefunga wala kutaja magufuli,
 
wanamuombea kwa nani? kama wanamuombea kwa Mungu wa haki wajue wanapoteza muda wao
 
Wembe ni uleule uliomnyoa shetani. Hongereni jeshi kubwa mmeonyesha njia, wanaume(Taifa kubwa) bado wanafukiza uvumba. Bravo JPM, chapa kazi. Wasioitakia mema Tz wajinyonge na tamaa zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom