Wanaume wengi ni sumu katika mahusiano

Wanaume wengi ni sumu katika mahusiano

Nimesikiliza mahojiano ya alokuwa mke wa Mwaka,kiukweli wanaume wa kitanzania waachane na habari za kuoa wake wengi hawawezi kabisa kuwamudu na kujimudu wao kiakili,mwanamke alikuwa mkeo kakuzalia watoto unataka wakaishi wapi ukiwanyang’anya nyumba,na nyumba ulimpatia hivi wanaume hamuwezi mpa kitu mwanamke kwa roho moja?

Mnataka ukimpa kitu muwe nae pamoja tu awe chini yako,kama hamuwezi muwe mnaacha kutoa maana ni wachoyo na mna roho ndogo na hamuwezi majukumu ya kulea mwanamke na watoto,wanaume wengi pia wapo kama Mwaka mkiachana anataka kukukomesha ujute kumfaham mtu akichoka mwache aende zake. Pia Jaribun kuwaheshim mama wa watoto wenu na kuwasitiri, vizazi vilivyopita viliwaharibu sana vijana wa kiume kwa kuwafundisha kuwa mwanamke hana thamani na kuwadidimiza wanawake.

Ukiangalia wanaume wengi huwa hawaheshimu wake zao ni wachache mno ila wengi wao wakatili,wenye roho mbaya wanaume wakiacha sawa ila wakiachwa wao kosa kubwa wanataka mwanamke aishi ndoa ambayo haifurahii ,mume anakaa mwaka mzima hagusi mke na umeoa wake wengi kisa kuonesha jamii we rijal hivi kwanin wanaume wengi wenye kasoro hujitutumua sana mbele ya jamii.MBADILIKE
Kwani aliyekuambia hayo aliyosema mke wa Dr Mwaka ni ya kweli mpaka utoe conclusion kwa wanaume wote?? Je umemuuliza Dr Mwaka yanayomsibu au ndio nyie mnaosikiliza kesi upande mmoja na mnatoa hukumu?? Halafu hii kauli ya "mwanamke amekuzalia" huwa mnaitoa wapi kama kumbe mnawazalia wanaume watoto mbona Kuna kesi nyingi za nyie kuwang'ang'ania watoto?
 
Unaona Sasa ?.

Wewe unachojali ni kupelekewa moto .

Hakika ni kuwa mke anaweza kuomba talaka kutoka kwa mumewe katika hali zifuatazo:

Ikiwa anapata dhara kutoka kwa mumewe kama kumpiga, kutomtimizia tendo la ndoa kwa sababu yoyote ile, kughibu kwa muda bila kuwa na habari kumhusu na kadhalika. Hii inatokana na msingi wa Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliyesema: "Haifai kudhuru wala kulipana madhara" (Ahmad, Ibn Maajah, ad-Daraqutwniy).
Ikiwa mume hana istiqaamah katika Dini kama vile kuacha Swalah na kufanya maasi mengine mengi na makubwa.
Ikiwa mume hamtimizii mkewe haja zake za msingi kama kumtizama kwa chakula, malazi, matibabu na kadhalika.
Ikiwa mke hampendi tu mumewe, anaweza kuomba Khul'u (kujivua kwenye ndoa) na katika hali hii mke atabidi amrudishie mumewe mahari yake aliyompatia wakati wa harusi.
 
Yeye anasema wanaume wa kitanzania au wa kiafrika sawa. Hao wakizungu wanaoweza kufanya hui ujinga wako Nchi gani?
Huyu Dada ana mawazo mazuri lakini kwa hii ya leo amepotoka sana.
Anachukulia maisha poa sana.

Wanaume tunapata pesa na mali kwa hustle kubwa sana, zingine ni hatari kabisa ndio maana hatutakagi ujinga hata uende Marekani ni hivyo hivyo.

Yule dada hataki mali za mwaka hiyo nyumba alimpa akamuandikisha mke na hajadai mali za mwaka
 
Ndugu zangu Wanaumez msikubali kufa Kwa presha kisa Wanawake


Wanawake wa Sasa ni makatili sana , wachache mnooo Wana uanamke Ndani mwao, wachache mnoooo wanaoweza kuvumilia Kwa Ndoa .


Na hivo basi, msiwaonee huruma ,Bora wakuite katili ,Roho mbaya, ila nenda naye uso Kwa uso !!.


Utaishiiiiii sana
 
Wanawakez wanaume wa Sasa wameamka .

Kwanza ndo maana hatuoi.

Na mtakubali shooooo, nyie Si majeuli???.

Mtakubali tuuuu
 
Yeye anasema wanaume wa kitanzania au wa kiafrika sawa. Hao wakizungu wanaoweza kufanya hui ujinga wako Nchi gani?
Huyu Dada ana mawazo mazuri lakini kwa hii ya leo amepotoka sana.
Anachukulia maisha poa sana.

Wanaume tunapata pesa na mali kwa hustle kubwa sana, zingine ni hatari kabisa ndio maana hatutakagi ujinga hata uende Marekani ni hivyo hivyo.

Wanaume weusi kawaida kukandamiza wanawake mmezoea ila sasa hiv wanawake sio kama wa zamani
 
Okay sawa. Mwaka naye atulie tu hata akilazimisha hakuna pendo tena pale

Dada kavumilia muda mrefu kaomba talaka kimya kimya mwaka jeuri hataki kutoa na anaoa na anaweza asikanyage kwa mke mwaka mzima na Haitoi matumizi nani anavumilia,angempa talaka kimya kimya tu isingekuwa shida ila hataki
 
Wanaume weusi kawaida kukandamiza wanawake mmezoea ila sasa hiv wanawake sio kama wa zamani
Tena Bora wa zaman, tuliwaonea huruma Kwa jinsi walivyotuheshim.

Mwanamke aliachika alafu humsikiii anamsema vibaya Mwanaume.


Siku hizi mkiachika mnaaita wandishi wa habari ,kututangazia madhaifu yetu, ili mtukomoe ,Wanawake wengine wasitupende.
 
Back
Top Bottom