Mkuu, labda kama anachokihofia ni kwa sababu za kidini, kwamba atakuwa anazini kwa kuwa na jamaa kabla ya talaka. Ila kama ni kwa sababu za kisheria, adhabu atayopata muoaji mpya ni kulipa fidia kwa mume halali, ambapo mtu kama unampenda unaweza tu kufanya, kwamba nitamuoa na kulipa hiyo fidia kama jamaa atadai.
Nafikiri sababu hasa ni za kidini, ndio maana hata suala limechukua muda mrefu huko bakwata, wakati lingeenda baraza la kata tayari angekuwa ameshapata barua yake na kuingia mahakamani kuomba talaka. Nimewahi kuambiwa kuwa wanawake wa kiislamu hutishiwa kuvuliwa uislamu wao ikiwa watapeleka masuala ya ndoa nje ya bakatwa, kwa hiyo wengi huogopa hilo na kuendelea kusubiri process za bakatwa. Njia rahisi kabisa ilikuwa ni kwenda baraza la kata kwa ajili ya suluhu