Wanaume wengi ni sumu katika mahusiano

Wanaume wengi ni sumu katika mahusiano

Nimesikiliza mahojiano ya alokuwa mke wa Mwaka,kiukweli wanaume wa kitanzania waachane na habari za kuoa wake wengi hawawezi kabisa kuwamudu na kujimudu wao kiakili,mwanamke alikuwa mkeo kakuzalia watoto unataka wakaishi wapi ukiwanyang’anya nyumba,na nyumba ulimpatia hivi wanaume hamuwezi mpa kitu mwanamke kwa roho moja?

Mnataka ukimpa kitu muwe nae pamoja tu awe chini yako,kama hamuwezi muwe mnaacha kutoa maana ni wachoyo na mna roho ndogo na hamuwezi majukumu ya kulea mwanamke na watoto,wanaume wengi pia wapo kama Mwaka mkiachana anataka kukukomesha ujute kumfaham mtu akichoka mwache aende zake. Pia Jaribun kuwaheshim mama wa watoto wenu na kuwasitiri, vizazi vilivyopita viliwaharibu sana vijana wa kiume kwa kuwafundisha kuwa mwanamke hana thamani na kuwadidimiza wanawake.

Ukiangalia wanaume wengi huwa hawaheshimu wake zao ni wachache mno ila wengi wao wakatili,wenye roho mbaya wanaume wakiacha sawa ila wakiachwa wao kosa kubwa wanataka mwanamke aishi ndoa ambayo haifurahii ,mume anakaa mwaka mzima hagusi mke na umeoa wake wengi kisa kuonesha jamii we rijal hivi kwanin wanaume wengi wenye kasoro hujitutumua sana mbele ya jamii.MBADILIKE
Pole mamaangu 🤗🤗
 
Wanaume asilimia kubwa ikitokea mkaachana furaha yao wakuvuruge ukose pa kushika yaan ukose ramani zote afu kila siku wasikie una shida ndo furaha yao hata km wameachana mwanamke akiwa na mapacha watatu ananyonyesha. Wana roho mbaya sana hawataki ex zao wapate amani
 
Kama kuna watoto hiyo kesi nyingine ila mwanamke tu kaamua tuachane aaah vitu vyangu anaviacha akatumie vya anakoenda.
Ila kama mpaka watoto kawaweka kwenye hali ngumu hapo kazingua.
 
Wanaume asilimia kubwa ikitokea mkaachana furaha yao wakuvuruge ukose pa kushika yaan ukose ramani zote afu kila siku wasikie una shida ndo furaha yao hata km wameachana mwanamke akiwa na mapacha watatu ananyonyesha. Wana roho mbaya sana hawataki ex zao wapate amani
Sasa wanalo na hivi hilo lidada lizuriii weeee sasa hivii litaolewa
 
6B5FEDE7-DC3F-4EDE-BB05-DBF7D82DBD65.jpeg
 
Back
Top Bottom