Mbona mnaenda nje ya mada? Hakuna mtu anayetamani NOAH ya mtu. Walisema, ACCACIA wameshikwa pabaya na kwamba hata iweje, Kabudi amesema hawanabudi kutulipa mipesa ambayo kila Mtz angeweza kununua NOAH yake mpya. Sasa unaposema ati wanaume wanao lilia NOAH za bure, una maana gani? Zile pesa ambazo tungelilipwa kama tulivyoambiwa, hata wanawake nao wangelinunua wakitaka. Hakuna mtu aliyelilia hizo pesa ni wanasiasa wetu walitutumainisha.
Kwani hukusikia tena jana kuwa tumepewa 14,000/= kila mtz? Ziko wapi? Zimeyeyuka nazo. Hakuna anayelilia, tumeshajua kuwa ni namna tu ya kuvuruga akili zetu tusiwaze ya TL.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.