Wanaume wa JF mna shida gani?

Wanaume wa JF mna shida gani?

OK ntaanza kozi kukujali na kuwa na mapenzi ya dhati na kutimiza wajibu wako afu ntakuja PM kukubembeleza ole wako uniletee shobo za gharamagharama ndo utanijua mimi ni nani.
Khaa yaani uje uniigizie hayo yote halafu utegemee nikukubali kizembe tu hivyo? Lazima nikuchape gharama tena nikutie hasara kabisa eboh!
 
Asante
Unapokwenda msikitini au kanisani then mahubiri yakawa yanalenga kuacha wizi ilihalibwewe sio mwizi, huwa unamwambia shehe au mchungaji kwenda kuhubitia wezi pekee?

Pia soma uelewe, nimesema wapo wachache sana wenye unafuu.
 
Sijasema wanaume wote mkuu, ila ni wengi wao maana najua wapo wanaume wengi tu ambao hawanaga hata muda wa kubishana kuhusu mapenzi na mahusiano wako busy kwenye majukwaa ya siasa na elimu huko.

Mimi nawaongelea wale wengi wao wanaochangia mada za mapenzi na mahusiano yaani hadi kuna wengine nimewakariri maana ndiyo mabingwa wa kubishana na wanawake humu na maneno yao ni matusi na kejeli tu kwa wanawake they always speak ill of women so sijamaanisha wote
Umewanyanyapaa wanaume wote wenye app ya JF, ukimuona mwanamme ana app ya JF tu unamuona hamnazo.

Unapiga vita chauvinism kwa reverse chauvinism!
 
Ni shida kwa kweli kazi ipo
Na ukitaka ujue kuwa wamefanikiwa ktk hilo angalia ni wanawake wangapi wanao uwezo wa kuwaambia pale wanapokosea zaidi ya wale wa praise and worship team.
 
Tunaomba fanya analysis pia kwa wadada wa JF,(wewe pia ukiwemo)

Unachopaswa kukumbuka ni kwamba,hao wanaume na wanawake wa JF ndiyo hao hao waliopo mtaani,hawa wa humu hawana dunia yao peke yao!

Kubwa zaidi ni kwamba,katika jamii yoyote,kuna watu wa aina mbali mbali,wapo wenye busara zao,na wapo wenye mizaha mingi,na wapo wajinga wajinga,lakini pia wapumbavu hawakosekani, na hii sio kwa wanaume tu,hata wanawake!

Kwa mfano,tazama mada za baadhi ya wanawake walio wake za watu hapa MMU,wanavyojiachia kuelezea nia au namna walivyotombwa na wanaume wasio waume zao,tena kwa kujisifia kabisa,(hayo ni maadili?)

Kikubwa si kuwalaumu wanaume,tuseme ukweli kwamba kizazi hiki kimepotoka,na shetani amefanikiwa sana kukiponda ponda, namna ya kutoka hapa sio nyepesi,inahitaji nguvu kubwa,ukatili kidogo,na uvumilivu wa hali ya juu sana, vinginevyo kwa siku za usoni,hali itakuwa mbaya zaidi!
kumuelewesha chizi utajipa kazi
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa huu mtandao not so long, mwanzoni sikuweza kujiunga kwasababu sikujua namna ya kufanya hivyo. Baadae nikikutana na mtu ambae pia ni mtumiaji wa huu mtandao ndio akanipa ABC's za namna ya kujiunga.

Nilikuwa naiona kwenye suggestions ninapogoogle jambo, nikavutiwa nao sana. Ila nikajikuta nakuwa msomaji tu na nilitamani sana kuwa mmoja wa members humu. Hatimae nikafanikiwa.
Nilijiunga na nikaendelea kuwa msomaji tu hadi hapo nilipoamua kuwa mchangiaji pia. Ila nilivutiwa sana na jukwaa la MMU na CC.

Kwa muda wote nimekuwa nikishindwa kuwaelewa members wa kiume wa humu ndani. Ni wako na tatizo gani? Ni malezi mabovu,stress,kukata tamaa,elimu duni(nieleweke sio ya darasani tu) au tatizo ni nini haswa?

Wengi wao sio wastaarabu kabisa, mtu aweza kuleta mada yake badala wachangie kwa hoja wao ni matusi tu na hii ni hata jukwaa la siasa ambapo ningetegemea kuwakuta wenye weledi na hoja madhubuti kama ilivyo sifa ya mtandao huu(home of great thinkers)
Kuna siku nilileta uzi nikashambuliwa sana kwa matusi, nasikitika niliwajibu kulingana na level yao ya thinking ila i was not proud of it at all.

Hivi nyie binadamu wenye kuitwa wanaume haswa wa humu ni kwasababu gani hamna maadili na hamjielewi?
Hii inatupatia picha wazazi watarajiwa kuwa makini sana na watu tunaotaka wawe baba wa watoto wetu, hivi kama baba wa familia anakosa maadili na upeo namna hii ataiongoza vipi familia yake?

Kuna wakati nikiona mwanaume ana app ya jf kwa simu yake namtafakari sana, namchukulia kitofauti kidogo. Nashukuru mdogo wangu sio member humu.
Wapo wachache atleast ukisoma unafarijika kuona kuwa angalau bado tuna akina baba bora kwenye jamii zetu. Tambueni nyie ni wachache kwa idadi duniani, kwahiyo mnapaswa mjitafakari sana je mnastahili kuitwa wanaume au ni viumbe wenye uume tu?

Kuitwa mwanaume tayari ni jukumu, hivyo tangu ukiwa mdogo unapaswa kukuzwa hivyo. Sasa kama mlipitia malezi mabovu kutoka kwa wazazi its about time dunia iwafunze.
Acheni kujisifia mambo ya kipumbavu, mna jukumu kubwa sana hapa duniani, kumbukeni mlipoteleza kisha mchukue hatua.

Ipeni JF heshima yake kama ilivyo kauli mbiu yake.


UPDATES:
Ukitaka uamini kuwa nililoandika ni kweli tupu bila ya chenga basi soma comments za kwenye huu uzi.
Hongera sana kwa kuwa unatupenda hukutaka kuwa mnafiki,,, huu ni upendo mkuu asante sana..
 
Khaa yaani uje uniigizie hayo yote halafu utegemee nikukubali kizembe tu hivyo? Lazima nikuchape gharama tena nikutie hasara kabisa eboh!
we mwanamke probably ni Mbaya!
 
Jamii Forum ya wastaarabu iliisha mwaka 2013 baada ya hapo nadhani hata Moderators ni kama vile walijiachia mno ili watu wengi wajiunge. Jamii Forum ilikuwa kama familia members wanajuana japo siyo physical na walikuwa wakiheshimiana. Bans zilikuwepo kama mjuavyo hakuna kijiji kisicho na wazee. Kwa sasa Jf ina vilaza wengi kuliko wenye akili.
 
Mkuu mimi nikikutajia hizo id utanipa hiyo vocha ya 10,000?
kwani kina evelyn salt na Money Penny ni wanaume hao?? wapo kifungoni ebu jiulize wamefata nini huko rumande? endelea tu kudhani wanaume tu ndio wenye shombo..

Kuna wanawake physicaly nawajua na wana ID za kiume..wanashombo hata za samaki zina afadhali..we kaa ukituhukumu wanaume tuliojiweka wazi kua ni wanaume..Kuna watu humu wana jinsi mbili mbili,tukisemwa wanaume Anakaa kwa wanawake,wakisemwa wanawake anarudi kiumeni..

Asee member wa JF sio kama wa Insta au badooo...Lawama zako ziweke kwa wote usitaje JINSIA kabisa maana ukiweka jinsia basi usi include wote Mtaje muhusika wako unae mlenga ila kusema "wanaume wa jf" unakosea.

ukitaka kujua unakosea

Nitajie ID 10 ambazo huwajui kwa kuwaona Live(physicaly) ila umewajulia huku JF ambao wewe unasema ni WANAUME...ukiweza taja ID 10 za wanaume nakupa vocha ya 10,000.

Nataka tu ufahamu kuwa JF member wachache sana walio amua kujiweka live kuwa ni ME au KE...wengi wao wanacheza nafasi zote KE na ME.
 
wanaume less than 27 years ndio wasumbufu humu…...nyie mliomjibu mtoa mada mbovu mbovu..tajeni umri wenu humu kama mnabisha???!!!!??? topic kaiwasilisha vizuri bila kujeruhi hisia zenu wanaume..naona wachache wamekua wastaarabu na kuelewa topic...nyie wengine mmezoea kujibishana kwa matusi na sisi ma singo mazas, basi mmekaa tayari tayari kumtukana dada wa watu..proving what she says about you.
 
umefungua uzi ambao kwa upande wangu naona ni pumba so kwann usikosolewe? Hizo ndio challange lazima uzipitie pindi unapotetea hoja ambayo unaona ipo sawa kwako ko lazima upiganie kombe, sio kukimbilia lawama,,, haya ulitukanwa wapi lete ushahidi,,, Mi najua we hujatukanwa bali umebishana kwenye uzi ukazidiwa hoja ndio ukaona kama unaonewa WANAWAKE tunawajua
 
Asante, mimi ni mgeni humu lakini natamani ningeijua JF tangu mwaka 2010 nikajiunga maana huwa nakutana na baadhi ya nyuzi za miaka hiyo na ninaona namna watu walivyokuwa wanachangia kiustaarabu kulinganisha na sasa yaani najutia sana kuchelewa kuijua JF
Jamii Forum ya wastaarabu iliisha mwaka 2013 baada ya hapo nadhani hata Moderators ni kama vile walijiachia mno ili watu wengi wajiunge. Jamii Forum ilikuwa kama familia members wanajuana japo siyo physical na walikuwa wakiheshimiana. Bans zilikuwepo kama mjuavyo hakuna kijiji kisicho na wazee. Kwa sasa Jf ina vilaza wengi kuliko wenye akili.
 
Back
Top Bottom