Wanaume wa Dar buana...!

Wanaume wa Dar buana...!

Daladala imejaa, unapanda huku ukijua una nguvu na uwezo wa kusimama. Kwanini nikupishe?
Mimi huwa napisha wazee tuu. Basi kwa huruma tuu.
 
Mimi ndio mana nimeanza kuweka kibubu
mke wangu asije pata adha kama izi.

na akiwa ana mimba ama timu ya watoto
Kuanzia wawili basi ntajitahidi asipande
dala dala atumie bajaji nk.
 
Habari ya weekend wakuu...
Leo bwana kwenye daladala ya huku kwetu gomz kimetokea kisa kimoja. Aliingia kwenye daladala mama mwenye mtoto na siti ya mbele kabisa karibu na mlangoni alikaa m'baba kwa kumuangalia anaweza kuwa yupo mid/late 40s. Kando yake alisimama mwanaume mwingine wa makamo yaleyale, basi yule aliyekaa akasimama kumpisha yule mama akae. Aliposimama akaanza kumwaga povu (kumbe alikuwa ameambiwa na yule aliyesimama kuwa amsaidie mtoto ).... Wacha ateme povu eti ooh wanawake hampendani, mwenzenu anaingia mnashindwa kumpisha kwa sababu gani? Mwenzie akawa anamtuliza, walikuwa hawajamuona si unaona gari imejaa? Ye kakomaa hamna walikuwa wamemuona wanawake wana roho mbaya sana, yaani hawapendani kabisa.
Kusema kweli yule mama aliyeingia na mtoto mimi sikumuona maana nilikuwa nimejilalia zangu usingizi, na hata ningemuona nisingempisha bali ningempokea mtoto.
Ila yule baba mimi kanishangaza sana, ni kwa nini anadhani sisi wanawake ndio tunatakiwa kupisha? Kwanza yeye alikuwa jirani kabisa pale kwa hiyo badala ya yeye kupisha alitaka atokee mwanamke aliyekaa nyumba ndio apishe?
Niwaulize ninyi wanaume, hivi akiingia mama mwenye mtoto au mjamzito anayetakiwa kuwa wa kwanza kunyanyuka kwenye siti ni ninyi au sisi? Yaani sisi tunabeba mimba miezi tisa, tunalea hadi watoto wanafikia umri wa kujitegemea eti inapotokea tupo huru yaani hatuna mimba wala mtoto wa kunyonyesha bado tuna wajibu wa kuwapisha wenzetu walio katika hali hizo???! Kweli leo nimejua kuwa ni shughuli pevu kuzaliwa mwanamke Afrika, nadhani wanawake wa Afrika tuna mbingu yetu spesho maana sio kwa kazi hii tuliyonayo. Nilitaka nimtolee uvivu yule mwanaume ila nikaamua nikae kimya maana nilikuwa na my uncle mmoja naheshimiana nae na anajua mimi siongeagi kabisa nikaamua kuilinda image yangu
Hebu tuoneeni huruma

NB: Hapa nazungumza na wale ambao huwa wanapisha sio wale makauzu
Huruma yake anailazimishia kwa mtu mwingine, na mara nyingine wakina mama wenye watoto huwa wanawatumia watoto kama ngao ya kutaka kupishwa gari zinaweza kuwepo nyingi tu ila anajua mtampisha tu hivyoanaamua kujitoa ufahamu ila kibinadamu hakuna mwenye jukumu la kumpisha ila wote tunapaswa kuwa na huruma sio awe mwanamke tu au mtu fulani tu, tukio lako linafanana na safari moja natokea dodoma enzi hizo akapanda mtu mwenye ulemavu mzee akampisha halafu akaanza kumsema kijana ambaye alikuwa amelala kuwa vijana hampendani, tena mwenzio mlemavu...ni kukosea kufikiri maana kama umejitolea kusimama maneno ya nini? watakuona umesimama watakupisha pia maana hata kama anaamini kuna mungu na kuna baraka kwa mapovu hayo sidhani kama alipata hizo thawabu kwa kweli!
 
Uko sawa kabisa boss, kama hujisikii kupisha kaa tu sio unapisha huku unasema fulani ndio alitakiwa kupisha
Huruma yake anailazimishia kwa mtu mwingine, na mara nyingine wakina mama wenye watoto huwa wanawatumia watoto kama ngao ya kutaka kupishwa gari zinaweza kuwepo nyingi tu ila anajua mtampisha tu hivyoanaamua kujitoa ufahamu ila kibinadamu hakuna mwenye jukumu la kumpisha ila wote tunapaswa kuwa na huruma sio awe mwanamke tu au mtu fulani tu, tukio lako linafanana na safari moja natokea dodoma enzi hizo akapanda mtu mwenye ulemavu mzee akampisha halafu akaanza kumsema kijana ambaye alikuwa amelala kuwa vijana hampendani, tena mwenzio mlemavu...ni kukosea kufikiri maana kama umejitolea kusimama maneno ya nini? watakuona umesimama watakupisha pia maana hata kama anaamini kuna mungu na kuna baraka kwa mapovu hayo sidhani kama alipata hizo thawabu kwa kweli!
 
Mimi ndio mana nimeanza kuweka kibubu
mke wangu asije pata adha kama izi.

na akiwa ana mimba ama timu ya watoto
Kuanzia wawili basi ntajitahidi asipande
dala dala atumie bajaji nk.
Ni kweli ila si unajua riziki anagawa muumba
 
Sina kawaida ya kumpisha siti mtu mzima na akili zake aliyeamua bila kushurutishwa na mtu kupanda daladala iliyojaa akati mji una daladala nyingi tuu!
 
Wanawake tunapitia mengi mkuu, unaweza kuniona sina mimba wala mtoto ukajua niko huru kumbe tumbo la period limenikamata sawasawa au naumwa kiuno, wengine huwa wanaanza kuumwa hata wiki moja kabla ya kupaa angani. Mkuu we acha tu, siku ambazo mwanamke anainjoi maisha yake hapa duniani ni chache mno.
"Kinamama waheshimiwe kote duniani"
 
Sina kawaida ya kumpisha siti mtu mzima na akili zake aliyeamua bila kushurutishwa na mtu kupanda daladala iliyojaa akati mji una daladala nyingi tuu!
Haha kuna baadhi ya maeneo huwezi kupata siti hata iweje
 
Labda huko Dar..ila huku niliko mimi inawezekana kabisa, kama ukishindwa kabisa panda bajaji.
Juzi nimepanda daladala tukafika kituo kimoja kikubwa kuna daladala nyingi hatari, ile nlopanda mim ikawa imejaa..kuna mzee mmoja akapanda af tall kimtindo kwahyo ilikua lazima ainame, akaja kusimama jiran yangu akijua ntampisha haikuwa ivo.!
Watu wakawa wananiangaliaa nikaona mengi ya mengi nakavaa zangu earphones nakula mziki taratiibu!!
Haha kuna baadhi ya maeneo huwezi kupata siti hata iweje
 
Nonsense kabisa.......aliyemdogo humpisha mkubwa.....mwanaume yuko juu ya mwanamke kiafrika hivyo mwanamke kukalia kiti huku mwanaume kasimama ni utovu wa nidhamu..ni sawa na mtoto kukaa kitini half mkubwa asimame....
Mwanaume ni kichwa cha mwanamke, kichwa cha mwanaume ni Mungu....
 
Aiseeee....
 
Habari ya weekend wakuu...
Leo bwana kwenye daladala ya huku kwetu gomz kimetokea kisa kimoja. Aliingia kwenye daladala mama mwenye mtoto na siti ya mbele kabisa karibu na mlangoni alikaa m'baba kwa kumuangalia anaweza kuwa yupo mid/late 40s. Kando yake alisimama mwanaume mwingine wa makamo yaleyale, basi yule aliyekaa akasimama kumpisha yule mama akae. Aliposimama akaanza kumwaga povu (kumbe alikuwa ameambiwa na yule aliyesimama kuwa amsaidie mtoto ).... Wacha ateme povu eti ooh wanawake hampendani, mwenzenu anaingia mnashindwa kumpisha kwa sababu gani? Mwenzie akawa anamtuliza, walikuwa hawajamuona si unaona gari imejaa? Ye kakomaa hamna walikuwa wamemuona wanawake wana roho mbaya sana, yaani hawapendani kabisa.
Kusema kweli yule mama aliyeingia na mtoto mimi sikumuona maana nilikuwa nimejilalia zangu usingizi, na hata ningemuona nisingempisha bali ningempokea mtoto.
Ila yule baba mimi kanishangaza sana, ni kwa nini anadhani sisi wanawake ndio tunatakiwa kupisha? Kwanza yeye alikuwa jirani kabisa pale kwa hiyo badala ya yeye kupisha alitaka atokee mwanamke aliyekaa nyumba ndio apishe?
Niwaulize ninyi wanaume, hivi akiingia mama mwenye mtoto au mjamzito anayetakiwa kuwa wa kwanza kunyanyuka kwenye siti ni ninyi au sisi? Yaani sisi tunabeba mimba miezi tisa, tunalea hadi watoto wanafikia umri wa kujitegemea eti inapotokea tupo huru yaani hatuna mimba wala mtoto wa kunyonyesha bado tuna wajibu wa kuwapisha wenzetu walio katika hali hizo???! Kweli leo nimejua kuwa ni shughuli pevu kuzaliwa mwanamke Afrika, nadhani wanawake wa Afrika tuna mbingu yetu spesho maana sio kwa kazi hii tuliyonayo. Nilitaka nimtolee uvivu yule mwanaume ila nikaamua nikae kimya maana nilikuwa na my uncle mmoja naheshimiana nae na anajua mimi siongeagi kabisa nikaamua kuilinda image yangu
Hebu tuoneeni huruma

NB: Hapa nazungumza na wale ambao huwa wanapisha sio wale makauzu
Usinikumbushe mimi mambo ya kusaidia siti au kusaidia mtoto kwenye daladala.

Niliwahi msaidia mdada kubeba mtoto kufika mbele sikumuona. (Alishukia njiani halafu kuna wenzake walimuona sasa)
Nikampeleka mtoto polisi, nikaambiwa inabidi ukakae nae uache mawasiliano tutoe tangazo mamake akipatikana umlete.
Nikawaaga polisi naenda kununua vocha.
Sikurudi tena!!

Siku nyingine nikamsaidia mjamzito siti, katika kuinuka kumpisha simu ikadondoka kwenye siti akaificha kifuani, (hakuwahi kuizima).
mara ikapigiwa...sasa mlio wa simu naujua nikaanza kujisachi ....sioni simu!!! Kuskiliza vizuri inaitia katikati ya manyonyo ya mjamzito...khaaa!! Nikamuuliza vipi imekuwaje!? Eti nisameheee.

Kuanzia hapo nikajiona msaada wangu unakuwaga na gundu tu BORA MPEANE WENYEWE (WANAWAKE/WANAWAKE) msaada.
 
Ha haa!
Utaratibu wa kupisha watu kiti kwenye dala dala nilishauacha tangu mwaka 2006! Huyo unayempisha kiti, yeye pesa ambayo angenunulia gari ya kutembelea kajengea nyumba na anakulipisha kodi kila mwezi bila kupunguza hata senti moja! Why nimpishie. Kumpisha kiti mtu, labda awe mlemavu. Mzee, sijui mama mwenye mtoto, simpishi. Kama unajua una mtoto, panda boda boda ukapandie dala dala inapoanzia upate siti au geuza na dala dala upate siti. Mie nipande boda boda hadi stendi ili nipate siti afu nije kukupisha kirahisi? Huo moyo sina kwa kweli!
Mambo ya kupakatia mitoto ya watu, wengine hawajavalishwa pampas aje kukunyea au kukukojolea afu akuharibie siku bure! Kila mtu apambane na hali yake kwenye hili...
Kwa hali hii tutatoka kweli?
 
Back
Top Bottom