Wanaume wa Dar buana...!

Wanaume wa Dar buana...!

Shida ni kwamba wanawake wa siku hizi hamna shukrani unaweza mfanyia kila kitu na bado akakuona fala tu,zamani kulikuwa hakuna haki sawa lkn atleast wanawake kipindi hicho walikuwa wanajua kuthamini na kutoa shukran pale wanapotendewa wema! Hii ndo sababu wengine wanaamua kuwa makazu tu!
Unaruhusiwa kuwa kauzu ila kwa nini wewe ukiwa kauzu ni sawa na mimi nikiwa kauzu inakuwa nongwa? That's my concern
 
Kuna mmoja kitambo iko aliwai niletea mdomo daladala nzima wakaanza msupport, ahahah nilinyanyuka na sentesi moja shika mia nne shuka subiri gari ingine.

Ukweli wanawake hawapendani kuanzia uko labor wanakojifungulia adi makaburini nafikiri ni ile hali ya kuoneana wivu fulani.

Mfano toka na mchepuko au mke wako then fika hotelini au mgahawani then demu akaombe kiti jirani na alipokaa binti ahahah then tazama reaction
 
Habari ya weekend wakuu...
Leo bwana kwenye daladala ya huku kwetu gomz kimetokea kisa kimoja. Aliingia kwenye daladala mama mwenye mtoto na siti ya mbele kabisa karibu na mlangoni alikaa m'baba kwa kumuangalia anaweza kuwa yupo mid/late 40s. Kando yake alisimama mwanaume mwingine wa makamo yaleyale, basi yule aliyekaa akasimama kumpisha yule mama akae. Aliposimama akaanza kumwaga povu (kumbe alikuwa ameambiwa na yule aliyesimama kuwa amsaidie mtoto ).... Wacha ateme povu eti ooh wanawake hampendani, mwenzenu anaingia mnashindwa kumpisha kwa sababu gani? Mwenzie akawa anamtuliza, walikuwa hawajamuona si unaona gari imejaa? Ye kakomaa hamna walikuwa wamemuona wanawake wana roho mbaya sana, yaani hawapendani kabisa.
Kusema kweli yule mama aliyeingia na mtoto mimi sikumuona maana nilikuwa nimejilalia zangu usingizi, na hata ningemuona nisingempisha bali ningempokea mtoto.
Ila yule baba mimi kanishangaza sana, ni kwa nini anadhani sisi wanawake ndio tunatakiwa kupisha? Kwanza yeye alikuwa jirani kabisa pale kwa hiyo badala ya yeye kupisha alitaka atokee mwanamke aliyekaa nyumba ndio apishe?
Niwaulize ninyi wanaume, hivi akiingia mama mwenye mtoto au mjamzito anayetakiwa kuwa wa kwanza kunyanyuka kwenye siti ni ninyi au sisi? Yaani sisi tunabeba mimba miezi tisa, tunalea hadi watoto wanafikia umri wa kujitegemea eti inapotokea tupo huru yaani hatuna mimba wala mtoto wa kunyonyesha bado tuna wajibu wa kuwapisha wenzetu walio katika hali hizo???! Kweli leo nimejua kuwa ni shughuli pevu kuzaliwa mwanamke Afrika, nadhani wanawake wa Afrika tuna mbingu yetu spesho maana sio kwa kazi hii tuliyonayo. Nilitaka nimtolee uvivu yule mwanaume ila nikaamua nikae kimya maana nilikuwa na my uncle mmoja naheshimiana nae na anajua mimi siongeagi kabisa nikaamua kuilinda image yangu
Hebu tuoneeni huruma

NB: Hapa nazungumza na wale ambao huwa wanapisha sio wale makauzu
Ndiyo tofauti kuumbwa na ya kutengenezwa, MWANAE kaumbwa MWANAMKE katengenezwa.
 
Unaruhusiwa kuwa kauzu ila kwa nini wewe ukiwa kauzu ni sawa na mimi nikiwa kauzu inakuwa nongwa? That's my concern

Kwa mfano uliotoa hicho kitu alichosema hyo jamaa ni fact hata ww nahic unafahamu sema labda hutaki kubali tu, nyie huwa hampendani flani so ishu hapo aliyokuwa anataka aseme haswa sio swala la kupisha kiti maana yyote yule angeweza kumpisha sema point yake ni kwanini wanawake hawaoni wakifanya hvyo mara kwa mara kama wanaume?? Kwann huwa mnachuki za wenyew kwa wenyew zisizo na msingi?
 
Kusema ukweli me kwenye gari ndio maana napendaga kukaa nyuma kabisa au mbele.

Mambo ya mtu umejichokea na foleni hizi za dar unataka uperuzi JF anakuja mzee, au mwenye mtoto. Halafu makusudi anasimama karibu yako
Nawekaga ear phone masikioni kabisa.
Kama ni asubuhi nachukua na gazeti nasoma.
 
binamuu una mbinu kama yangu
Kusema ukweli me kwenye gari ndio maana napendaga kukaa nyuma kabisa au mbele.

Mambo ya mtu umejichokea na foleni hizi za dar unataka uperuzi JF anakuja mzee, au mwenye mtoto. Halafu makusudi anasimama karibu yako
 
Kwa mfano uliotoa hicho kitu alichosema hyo jamaa ni fact hata ww nahic unafahamu sema labda hutaki kubali tu, nyie huwa hampendani flani so ishu hapo aliyokuwa anataka aseme haswa sio swala la kupisha kiti maana yyote yule angeweza kumpisha sema point yake ni kwanini wanawake hawaoni wakifanya hvyo mara kwa mara kama wanaume?? Kwann huwa mnachuki za wenyew kwa wenyew zisizo na msingi?
Sio chuki, mimi binafsi huwa naona kama wanaume wana wajibu wa kupisha nikiona midume imejikausha ndio nanyanyuka
 
Back
Top Bottom