Wanaume tuwe wasafi jamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume tuwe wasafi jamani!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kigarama, Oct 6, 2011.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna Mambo sisi wanaume lazima tuyaache na tujue jinsi ya kuwa wasafi.

  1. Mtu soksi zinanuka kwa sababu ya kuvaliwa kwa muda mrefu haoni kama ni tatizo

  2. Hotelini mtu anasukutua na kutemea mate au kohozi kwenye sink linalotumiwa na watu wote. raha mustarehe

  3. Una Soksi ina bonge la tobo kwenye kisigino na kwenye dole gumba lakini bila ya aibu unaivua mbele za watu.

  4. Unaingiza dole lako kwenye pua na kutoa Kamasi au ugando wa kamasi bila ya wasiwasi mbele za watu

  5. Unafanya kazi Gereji hufui nguo zako hadi tofauti kati yako na Grease za gereji inakuwa sawasawa na Ziro

  6. Unajijua una kikwapa lakini kunyoa nywele zako za kwapani inakuwa ni mgogoro mkubwa.

  7. Unakula kitimoto, unakunywa bia na vitu vingine kadha wa kadha,lakini mswaki kwako mwiko!

  8. Huwezi kuoga mpaka ujue unakwenda kwenye kideti kipya.

  9. Domo lako unajua kwamba linanuka lakini wewe ndiyo kinara wa kutaka kunong'oneza watu.

  Update:

  10. Mtu mkewe akisafiri wiki nzima basi na yeye hatandiki kitanda chake wiki nzima. Huo ni u-smart au ni uchafu?
  11. Kila ukikutana na kichochoro au kigiza kidogo, mzee lazima umwage "kojo" tena lenye harufu kali. Jiheshimu!

  Hizi ni tabia ambazo baadhi yetu wanaume tunazo ila wengine wanazitetea eti ndiyo "ugumu" jamani tuwe wasafi kwani usafi nao ni sehemu inayochochea mapenzi.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280

  hapo kwa red ningeomba ufafanuzi yakinifu.....huwa pananichanganya sana.....
   
 3. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  dah sjui nikupe nini wewe??
  ahh umeongea fresh jaman...lijitu linanuka kwapa utasema kaficha tope la choo

  ahh kuna njemba moja iyo olevel ebwna ehh sjapata mfanoe yule bwana alikuwa anapenda kunihug kila akiniona na akishanihug anataka aninongoneze et ata masomo mema ye anataka anisemee kisikion sasa BALAA LAKE ILO KWAPA jaman ahh yaan akipanua mkono utasema kuna jalala limefunguliwa...na izo njino zinavyonuka jaman,...dahh afu anapenda kuzungumza chngereza mda wote bas watu wakawa WANAMPONDA AHH HAUNA LOLOTE MWINGEREZA GAN DOMO LINATEMA..raha ya chngereza domo livutie..
   
 4. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  aisee...vingine hata vinachefua!
   
 5. JICHO LA 3

  JICHO LA 3 JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  heeeeeeeeeeeeee?ya leo kali.........ila nadhani wamesikia kwa mjumuisho huu wasipofanyia kazi ni viburi.
  jf na darasa tosha
   
 6. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280

  Umeandika vizuri lakini inaelekea una visa na kitimoto, we ni jihad au mujahidina, basi umeharibu yote mazuri uliyoyaandika. Kwani Kitimoto ndicho kinaudhi mdomo!!!
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Oct 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Roziiiiiiiiii......achi achi achia bodi

  Achi achi achia bodi....

  Umedata wee binti.
   
 8. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280

  We Rose ni mwanamke kweli au geresha ya jina unafoka sana
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Oct 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Wewe katika yote umeona la kikwapa tu?
   
 10. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kwasababu yakiwa marefu sana yanachangia harufu ingawa WENGINE UTAKUTA ANA LINYWELE ILOOO LAKIN WALA HALITEMI...ahh lakin sasa ufuge jaman..yaan mwngne asubui anaomba kabsa BANIO LA NYWELE LA MKEWE APATE KUBANA AYO MANJUNJU...manake mpk shat linafanya kumbana jaman khaaa puuh stak mie!!!!!!!
   
 11. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna watu kwa asili wana kikwapa na kikwapa ni ugonjwa wa ngozi na wataalamu wa magonjwa ya ngozi dermatologists wanajua jinsi ya kushughulika nalo. Tatizo kuna watu wanajua kabisa wana kikwapa lakini kwa vile wanajidai wako Bize basi kunyoa ni mpaka watu wawe wameshapiga sana chafya kwenye daladala.
   
 12. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hahahaha Rose umenichekesha sana,na hizo jino hukawii kuona mabaki ya maharage na mchicha lol
   
 13. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  vp kakugusa nin?
  unayo?..ntakupa banio langu la nywele usijali...
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Oct 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Walahi tena nyoko alikudondosha ukaangukia kichwa ulipokuwa mtoto!
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  imbombo ngafu haaaaa pole kwa kuachwa dada,uliyavumilia mwanzo haaaaaaa
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hiyo nasikia ni dawa ya kuua mbu
   
 17. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  dahh ulijuaje mama?
  yaan akicheka unamwona dagaa mzima mzima kasimama kwenye njino zake ..dah hatari sjui ilikuwaje panapo denda na mkewe manake naskia ashaoa...
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Oct 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hahahaa mimi sijatoa bado senti zangu mbili kuhusiana na personal hygiene. Nikizitoa lazima kutakuwa na onyo la PG-13.
   
 19. JICHO LA 3

  JICHO LA 3 JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Teheteheteheteheh,,,,,:loco: MBAVU ZANGU MIE.. BASI KUMWAMBIA LIVE UNAOGOPA UNABAKI KUGEUKA PEMBENI TU.
   
 20. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Hao wanaume wenye tabia hizo ni wa huko kwenu,.....ambako hakuna maji,sabuni,maduka ya kuuza miswaki na dawa,hakuna leso,...etc,..huku kwetu hayo mambo hayapo_na hao kina Preta na Rose1980 wanao kussuport nafikiri mnaishi nao huko...waambie waje kwetu wataona tofauti
   
Loading...