pure heart
Akili yangu inakataa kuwa GGH alikuwa mario kwa JD. Wakati wanaoana JD hakuwa na hela - alikuwa maarufu tu. Mafanikio ya JD yamechangiwa kwa kiasi kikubwa sana na GGH kwa sababu GGH kazi ya umeneja aliiweza vizuri, biashara ya starehe anaijua vizuri na kwa kutumia ujuzi wake huo aliweza kumtengenezea JD njia. Kwa hiyo waliunganisha vipaji.
Kama kuna mtu mwingine ukiacha GGH aliyekuwa anasimamia kazi za JD naomba kufahamishwa. Sasa kama GGH alikuwa anaendesha "magari ya JD" alikuwa anaendesha magari ambayo ameyatolea jasho kwa kuandaa show za mkewe, kusimamia miradi n.k. Ni magari yao. Kama JD ataamua kujimilikisha mali zote kwa sababu GGH hakuchangia itakuwa ni dhuluma ya wazi wazi.
Na hapa ndipo ninapowaonea huruma wanaume wanaochuma mali na wake zao ambao usoni ndo walionekana wakifanya kazi kisha ndoa zikabumburuka. Akidai haki yake ataitwa a.k.a mario. Hata kama JD alikuwa akimlipa GGH kwa umeneja wake na GGH akawa na mali zake, naamini zipo mali zao kama wanandoa. Wao wanajua vizuri zaidi. GGH anaweza kuwa mario kwa wanawake wengine ila si kwa JD. Kaka alikuwa anajituma.
Kuhusu tabia zilizosababisha JD kumuacha mumewe mi naona ni sawa alivyofanya. Swali ni je, ndo kajua leo tabia za mumewe? Hapana. Alijua kabla hata hawajafunga ndoa ila kwa kuongozwa na wimbi zito la mahaba lililomfanya aone chongo la GGH kuwa kengeza. GGH ni kunguru asiyefugika. Ana tatizo la kihaiba. Naogopa kumhukumu kwa tabia zake mbaya maana siamini kama anazifurahia.
Atafurahia nini ndoa ya kwanza imemshinda-hayuko na mkewe wala m/wanae, mahawara ndo leo kwa huyu, kesho kwa huyu, ndoa ya pili imemshinda anajidhalilisha kwa kuvulia wanawake nguo hovyo ingawa hii inaonekana si tatizo kwa wanaume pombe nyingi Ndani kabisaa GGH hana furaha. Ni binadamu gani awe wa kike au wa kiume hapendi utulivu, upendo na amani? Nampongeza JD kuwa ameweza kutoka kwenye kifungo cha utumwa wa kihisia alichokaa muda mrefu. Namuombea GGH naye afike mahali aweze kutoka kwenye kifungo alicho nacho.
Kitendo cha kuropoka hadharani si cha kiungwana ila wenzi wengi wa kike kwa kiume huwa wanafanya hivi katika kutafuta faraja na huruma sema ndo hivyo mambo mabaya huwa ni ya kike, mazuri ya kiume.