WANAUME: Nimewainulia mikono!!

WANAUME: Nimewainulia mikono!!

Hapewi mtu hapa naenda kumsikiriza halafu nakuja kukwambia atakachoniambia
Angalia asije kukuwekea sembe kwenye kinywaji ukajikuta umesinzia ghafla, ukiamka unakuta tayari sahani imetumika. Maana mtu mwenyewe huyo alishatajwa kwenye orodha ile ya wafungwa wa China.
 
Angalia asije kukuwekea sembe kwenye kinywaji ukajikuta umesinzia ghafla, ukiamka unakuta tayari sahani imetumika. Maana mtu mwenyewe huyo alishatajwa kwenye orodha ile ya wafungwa wa China.
Nilishtuka nikamwambia siendi ng'oo, maana alikuwa kumbe na mpango wa kunikaba nikienda nisitoke, hanipati imekula kwake hiyo
 
Usije kuta alishakiandaa kirungu chake kabisa, sijui itakuwaje. Hahaaaaaaaaaaaaa..imekulaje kwake.

halafu wewe ........................ dogo nitakutolea tusi habati mbaya humu kuna BAN unachonga sana kama redio ya mbao bana
 
Hahhaaaa.... ndio ishaishia hapo mkuu, haya tunakusubiri kwa hamu!!!

Afu usiwe unapotea sana kiasi hiko :lol:
Okay, now let me say this,

Kawaida kwa mazingira ya kiafrika hasa, kuolewa kwa mwanamke ni prestige na heshima kwake mwenyewe na kwa familia yake (Mama hufurahi zaidi binti yake anapoolewa nadhani hata kumzidi baba) Hii inatokana hasa na mazingira tunayoishi ambayo msichana asiyeolewa mpaka kufikia umri wa miaka 30 na kuendelea huonekana ana kasoro fulani au kuchukuliwa kama mtovu wa heshima (nachelea kutumia neno malaya)

Sasa, hali hii imewafanya wanawake wengi kuwa na destiny ya kuwa wake za watu kwenye akili zao (Ingawa notion hii imeanza kubadilishwa na baadhi ya wasichana wa kisasa ambao either huamua kuishi maisha yao au kuamua kuwa na watoto tu bila kuolewa. Hata hivyo pia perception ya jamii kwa kiasi kikubwa humchukulia kama malaya au mtovu wa heshima.

Kwa sababu hizo hapo juu na zile za kutaka kufanya harusi kama ya fulani, hupelekea wengi wao kutaka kufunga ndoa na kuwa tayari kumuachia mtu yoyote ambaye atakuwa tayari kuwaoa. Wakati mwingine bila kuangalia mambo mengine tangulizi kabla ya ndoa ambayo huenda yanapelekea wapenzi wao wa muda mrefu (kwa kesi ya huyo rafiki yako) kuchelewa au kuonekana kama hawana mpango wa kufikia hatua ya ndoa.

Sasa labda niongelee kidogo for the case of vijana wa kiume wa siku hizi. Wengi wao wana hofu ya kuingia kwenye ndoa kwasababu wanaangalia zaidi vitu vifuatavyo;
  1. Uwezo wa kuwa na mke hasa kumuhudumia (Hapa mara nyingi wanaangalia kama wasipoweza kuwapa kila wake zao wanachokihitaji je hawatawasaliti na wanaume wengine?)
  2. Namna gani wataweza kufanya harusi kubwa kama ya fulani ili wasiingie aibu ya harusi yao kuwa ya kawaida bila kuangalia hasa maana ya ndoa na essence ya sherehe kwenye ndoa.
  3. Kutoaminiana (Hii ina apply kwa pande zote mbili) hasa kwa siku hizi ambapo uaminifu umekwisha kabisa kwa pande zote mbili.
  4. Mahari, this is an issue ingawa pia nyingine ni woga tu kwa hadithi wanazosikia vijiweni.
Sasa ukiangalia hizi utagundua kwamba kuna pande mbili zenye a very different move, wakati mwanamke anataka kuingia kwenye ndoa mwanaume yeye hasa mwenye nia ya dhati anakuwa anaogopa kuingia kwenye ndoa kwa kuangalia sababu hasa nilizozitaja hapo juu. Na ndipo hapo unakutana na majitu yanayotumia weakness ya wanawake kama huyo rafiki yako kutimiza azma yao.

charminglady, tafuta novel moja inaitwa Nothing Lasts Forever ya Sydney Sheldon ina story fulani kama inaendana na hiyo ya rafiki yako.

Nipo mkuu angalau hata nisipocomment huwa nasoma na kutabasamu mwenyewe pale ninapokuwa nimebanwa na majukumu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom