Kwa kawaida mtu anayeamini kwamba, ni dhaifu, hujaribu kwa kila njia kuficha udhaifu wake, na moja ya njia hizo ni kujikweza ili kujaribu kumshusha yule ambaye anadhani anamzidi. Mtu asiye na nguvu anaweza kujitahidi kupiga kelele, kupiga mikwala na vitisho, na watu wanapomwogopa, hupata nafasi ya kuwakandamiza hadi pale inapotokea bahati watu hao wakamshtukia kwamba hana nguvu anazodai anazo. Hata hivyo, ule woga kwa mtu huyo utaendelea kuwepo kwa watu wengi.
Kwa miaka mingi mwanaume aligundua kwamba, ni dhaifu mbele ya mwanamke na katika juhudi za kufidia pengo hili alipitiliza mipaka na kujikuta anafanikiwa kumkandamiza mwanamke. Eneo ambalo mwanaume anaweza kusema ni bora kuliko mwanamke labda ni mabavu ya kimwili, ambayo kwa bahati mbaya kwenye zama hizi hayana tena maana, yamepitwa na wakati.
Ukiangalia maeneo mengine yote, mwanamke ndiye bora zaidi. Mwanamke huishi miaka mingi zaidi ya mwanaume (kati ya miaka mitano hadi kumi) na mwanamke huugua au kupata maradhi kidogo zaidi kuliko mwanaume. Wanaume wengi zaidi, kwa kiasi cha mara mbili zaidi hupata matatizo ya kiakili ukilinganisha na wanawake, huku idadi ya wanaume wanaojiuwa ikiwa kubwa zaidi kuliko ile ya wanawake.
Ni kweli, mwanaume anaweza kuringia mabavu yake, lakini huo siyo ubora ambao binadamu anatakiwa kuuringia sasa hivi, kwani unahusu zaidi wanyama kuliko binadamu. Enzi za kuuwa wanyama kwa mawe, mabavu yalikuwa na maana, si leo. Mwanaume kwa karne kadhaa amejitahidi kutumia mabavu yake kumwonyesha mwanamke kwamba, yeye siyo dhaifu. Kwa bahati mbaya mwanamke naye akadhani ni dhaifu. Yeye kukosa mabavu akadhani ni udhaifu. Kwa wakati huo ilikuwa ni sahihi kwa sababu binadamu aliishi kama mnyama. Mtu aliyeheshimiwa alikuwa ni yule aliyekuwa na nguvu za kuuwa mnyama kwa jiwe, lakini bila shaka, leo mambo ni tofauti.
Hebu ona, hadi leo mwanaume anaweza kuhatarisha maisha yake au hata kupoteza maisha akijaribu kutafuta njia za kumfanya mwanamke amwone kuwa ni wa maana. Atasema uongo, atajikweza, atajifaragua, akitafuta kukubaliwa na mwanamke. Huu ni udhaifu mkubwa na unaonyesha ni kwa kiasi gani jinsia hii isivyojiamini. Udhaifu huu na mwingine ndiyo ambao mwanaume amekuwa akitafuta kuuficha ili mwanamke asiuone, ambapo ameamua kumkandamiza kwa mabavu.
Mwanazuoni mmoja wa utambuzi alipata kusema, wale wanaume wote ambao walijitahidi kuifanya dunia hii kuwa mahali penye kupendeza, walikuwa na tabia ambazo ni wanawake zaidi wanaokuwa nazo. Walikuwa na huruma, upendo, unyenyekevu, kusamehe, kusaidia na kujali. Leo hii mwanaume ukitaka kuitwa mwanamke, onyesha huruma, onyesha upendo, onyesha usamehevu. Unaweza kuona ilivyo, kwamba, bila kuonyesha mabavu manaume anahisi kuumbuka.
Kuna wakati tulikuwa tukizungumza na ndugu yangu ambaye alikuwa anatarajia kufunga ndoa. Mmoja kati ya ndugu zangu waliokuwepo alisema, inabidi huyo mchumbako tumuone, kwa upole wako anaweza kukukalia ukimwoa. Unaona? Kinachomlinda mwanaume ni kitu kimoja tu, kuwa mbabe na mkali, basi. Hana silaha nyingine na hajawahi kuwa nayo, hivyo akiiachia hii ya mabavu, anajua atakuwa amekwisha
Binfsi sikubaliani na wewe hata kidogo kwamba wanaume ni dhaifu mbele ya wanawake. Inawezekana kabisa wewe uliyeandika hii mada ukawa dhaifu mbele ya wanawake, lakini sio wanaume wote. Ukisoma vitabu vyote vya dini, Mwanaume aliumbwa wa kwanza na MUNGU.(Labda kama wewe ni mpagani). Mwanaume alipewa ruhusa kumtawala mwanamke. Kama mwanaume ni dhaifu alipewa vipi nguvu ya utawala???? Kama wanaume ni dhaifu kama unavyosema wewe, basi leo hii dunia yote ingekuwa inatawaliwa na wanawake kwenye kila nyanja. Kama wanawake sio dhaifu, basi wasingekubali kutawaliwa na wanaume kwa karne na karne. Usiandike tu kwa kutafuta sifa kutoka kwa wanawake. Inaonekana wewe ndio dhaifu ndio maana unaandika mada ili usifiwe na wanawake! Wanaume ndio tunao tawala, Mbinguni na Duniani. Juu mbinguni yupo YESU KRISTO ambaye ni mwanaume. Hata kwa Waislam, wanaye Mohamed ambaye ni mwanaume.
Kama wanaume tungekuwa dhaifu basi tungekuwa tunakojoa tumechuchumaa, lakini tunakojoa tumesimama wima. Hata simba jike akikojoa huchuchumaa na simba dume akikojoa huwa amesimama! Kama wanaume tungekuwa dhaifu kama unavyosema wewe, basi tusingekuwa na uwezo hata wa kuwangonoa wanawake. Sisi wanaume ndio tunao waingizia libolo na wao wanapokea maji ya uhai kutoka kwetu, hapo nani dhaifu? anayeingiziwa au anayeingiza???? Tena katika kungonoana wanawake huwa wanalialia sana, hebu niambie nani dhaifu hapo???? Na kama wanaume hutumia maneno ya uongo kuwatongoza wanawake na bado wanakubaliwa na hao wanawake, hapo nani dhaifu???? Hata shetani anajua kuwa mwanamke ni dhaifu ndio maana alimdanganya Hawa bustanini. Kama mwanaume ni dhaifu, basi angedanganywa kwanza Adamu na shetani, lakini shetani alijua fika kwamba hawezi kumdanganya mwanaume sababu mwanaume si dhaifu hata kidogo.
Tukija kwenye taaluma ndio kabisaaaaa "It's a mans world". Wavumbuzi wote na wanasayansi wote wakubwa, asilimia 99.9% ni wanaume! Hapo bado utasema wanaume ni dhaifu??? Manabii wote, asilimia 99.9% ni wanaume. Wanamichezo wote asilimia 95.9% ni wanaume. Viongozi wote duniani asilimia 99.9% ni wanaume.
Swali langu hapa ni Je?, hao wanawake kama kweli sio dhaifu mbona tumewazidi katika kila nyanja?????? Kama wao sio viumbe dhaifu kama unavyosema wewe ndugu, basi wanawake wangeshaamka miaka mingi na kuitawala hii dunia ambayo sasa inafika mwisho.
Mimi nakataa kabisa tena sikubaliani na wewe hata kidogo kwamba sisi wanaume ni dhaifu. Inawezekana kabisa baadhi ya wanaume wakawa ni dhaifu kutokana na kuzaliwa na hormones za kike. Pia wapo wanawake wenye Hormones za kiume na akili kama za wanaume, lakini idadi yao ni ndogo sana tena sana. Ndugu yangu acha kujishusha, kama wewe ni dhaifu, kaa na udhaifu wako lakini usitujumuishe na sisi.