Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

Vijana kuchezea maisha ni jambo linakuja automaticaly so huwezi kupita ujana bila kujirusha.tatizo linakuja pale mtu anapojisahau kuwa anapoteza muda
 

Mkuu umenena vema sana.
 
Wanajisahau mno
wakati kila kitu kwao ilikuwa easy
mashamba ya kuomba tu serikalini
viwanja hununui,unalipa tu ardhi unapimiwa
mi nikiwawaza hawa madingi zetu nakosa raha sana....
life yao ilikua affordable sana, sasa hivi hawana hata cha kutupa....zaidi ni lawama na kutuona sisi ndo tunakosea sana kuendeleza maisha yetu.

anyway back to your topic we have to learn and act though it will be tough enough to make us crazy.....
 

Halafu huwa naishia kuchekea tumboni wanapotoa ule usemi wao kuwa...'tatizo vijana wa siku hizi mna haraka sana'.....Nani anataka siku ya kustaafu arudi kijijini ambako huenda wala hakuwahi kukuendeleza? Manake hicho ndio kilitokea sana kwao, nyumba bure, mpaka fanicha..siku ya kustaafu anaondoka na masanduku yake tu, hata kibanda hana. Na alternative anayobaki nayo ni kurudi kijijini, kijijini nako hakujenga...and the list goes on and on...
 
Mi nafikiria tofauti kidogo hapo mazingira ya kazi hizi ni tofauti sana na wakati mwingi ndio maana utakuta watu wanaolipwa fedha nyingi bado wanshindwa kufanya mambo makubwa na mtu ambaye analipwa kidogo kutokana na mazingira ya kazi
 
gombaneni nae sasa hivi
atawasumbua mno huyo baadae...
Atawatolea laana msipompa pesa...hapo baadae
mngeanza kugombana nae sasa
wababa wengi wametawaliwa na mfumo dume, kwao kisa hela ni zao basi wanataka matumizi yao wayasimamie wenyewe. Wazzazi kama hawa huwaga wanatafuta mtu wa kumlaani baadae.

Nakumbuka baba mmoja mchaga wanae walipoona baba anaendekeza starehe na ni meneja wa sida kanda fulan walianza kuwa wakaksi wao na mama yao. Dingi kama halipi school fees kids wanabaki home, wala mama hastuuki anasema kabaisaa baba yenu awalipie.

Baba akaanza kuona maisha ya kupanga ndio bomba mama akaanza mkakati kila akirudi job, wanagombana kisaha anasaula pesa zote akiachiwa pesa ya msosi hapiki anabana dingi akirudi anaambiwa msosi hakuna pesa zimekwenda kununua site hadi akili ikamkaa sawa.

Huyu mama alihangaika hadi akaweza kununua site na kujenga tena kwa mbinde, mzee wa watu kwa ulevi sukari ikamuadabisha hajakaa sawa maini yakafeli, sasa ikaanza kuwa msala wa mama na watt lkn bora alikomaa wakapata mjengo na watt wakasoma.

Ninachoweza kusema muda mwingine mwanamke unapaswa kuwa ngangari kwa mumeo yani bora lawama kuliko fedheha. Unakaza uso kama mume haelekei.
 
Vijana kuchezea maisha ni jambo linakuja automaticaly so huwezi kupita ujana bila kujirusha.tatizo linakuja pale mtu anapojisahau kuwa anapoteza muda
 
ha haaa, umenichekesha tunapoongea pale nyumbani (mbele ya watoto wetu) kuwa tunajiandalia maisha yetu ya baadae....
Tukiwa tunapanga kitu tunajiambia "unajua tutabaki wawili tu", kwa hiyo tunaandaa kwa ajili ya wawili..... sasa wanatuambia yaani wao tunawatenga?
Babangu (RIP) namkumbuka sana wakati alipokuwa analipa ada za shule na kutuzungumzia kuhusu maisha alikuwa anatuambia tujitahidi ili asije akaendelea kulipa na ada za wajukuu zake. nakumbuka siku mdogo wangu alimkorofisha sana akamwambia unafikiri nakuambia kila siku kuhusu maisha ili uje kunisaidia? sitakuja kutegemea msaada wako baadae maana nina uwezo wa kujitegemea mpaka nakufa, ila sitapenda nikiwa nimezeeka bado nitakiwe kulipa ada za wajukuu ambao wazazi wao hawataki kukazana ili wajikwamue na maisha. Huwa nakumbuka sana hiyo statement yake
 
bora tunakubaliana kwa hili.....
yale mengine ambayo huyakubali basi nimeamua kuyapotezea, lol!


Kwenye hili sina ubishi mkubwa mwenzangu....

Mwenzenu hadi sasa, karibia vitu vingi sifanyi bila ruhusa ya bibi....ila wakati mwingine anakaba sana hadi natamani kukimbia nyumba....

Mwanamke wa hovyo ni zaidi ya kiroba cha misumali.....

Ndiyo maana nawakubali na kuwaheshimu akina na mama wenye busara zao, wakiongozwa na Bibi DC, mama yangu mazazi na wengine kibao....!!

Babu DC!!
 
Very true The Boss
hata ukiangalia kwenye makampuni makubwa,utakuta wale wenye mishahara mikubwa sana hawana hata nyumba,
mtu anaambiwa muda wa kuretire umefika ndo anaanza kuomba kuongezewa miaka kazini(contract) hapo ndo ataanza kutafuta kiwanja etc wakati miaka ya nyuma ndo walikua mapapa wa miji
1.watu tunajisahau sana honestly.
2.wrong or poor investment..na kuna wengine wameinvest kwa wanawake
3.hakuna kitu kibaya,as far as am concerned kama mwanamme mwenye wake na watoto wengi tena kila mkoa wachache wameweza kusimama
4.sababu ingine ipo spiritual zaidi,radhi ya mke au mume,wengi walio na uwezo ujanani husahau wake zao na kuinvest kwa nyumba ndogo,i do believe in karma..hela huwa zinapuputika tu
ila naona tofauti kubwa kwa vijana wa sasa.
 

Hebu shangaa na wewe
Inakuaje Mungu ahusike na mambo aliyotupa sisi?
 
Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
Maisha nilichezea leo hii nalala na njaa
Chemsha bongo kabla hujapagawa utashangaa
Chemsha bongo kabla hujapagawa utaduwaa
 
Kipaumbele kwa wakati ule ilikuwa ni nyumba , sasa gari anahitaji wakati pesa aliwekeza kwa vimada!!!!!!!!!!!!!.
 

I agree!!!!!!!!!
 
ha haaa, hapo kwenye kutaka kukimbia nyumba ndo balaa, lol!
kuna siku niliambiwa "siku hizi sitakuambia unikumbushe, maana inakuwa kero". yaani mimi nikishaona hapa kuna kitu tunataka kukifanya, then nikaambiwa nikumbushe siku nyingine mbona atajutaaaa, atakumbushwa hata anapokuwa usingizini.....
Ila ninachowapendea huwa mnakuwa na shukrani sana ..... mnajua kabisa kuwa haya yamefanyika sababu ya MKE WANGU
 
Samahani Kibibi Jongo, Eiyer na wengineo naombeni mnidadavulie hapa kwenye suala la umaskini na utajiri. Nimesoma maelezo yenu hapo juu na mmeonyesha kuwa juhudi yako ndio utajiri wako na uvivu wako ndio umaskini wako. Kuna watu hawalali katika maisha yao wao kucha kutwa wanahangaika kusaka maisha tena wakiwa na mipango mizuri ya kipesa lakini mwisho wa siku hawafanikiwi wanabakia hohehahe hili linasababishwa na nini? Pia huwa mwanadamu akipata chochote kizuri mfano wa utajiri huwa anamshukuru Mungu kwakuonyesha jinsi gani Mungu alivyompa, je wale waliokosa hali ya kuwa walikuwa na juhudi na mipango kama wale waliopata,wamekosa kwa sababu gani?
 
Last edited by a moderator:

Nimejifunza kitu hapa. Ila kubwa nikuwa watu wengi ujanani huwekeza katika starehe na uzee ukiwapata na mambo yakiwa magumu huwa wanatafuta ninani wa kumuangushia lawama zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…