Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,611
Mara ya kwanza niliposikia Mzee Gurumo wa Msondo Ngoma anadai ameimba zaidi ya miaka 50 na maisha yake bado ya 'kimaskini mno' niliona kuna kitu hakiko sawa... sikuwa na ushahidi tu lakini nilikuwa na uhakika kwa vyovyote vile 'atakuwa alichezea maisha ujanani'

Sasa jana walioona akifanyiwa interview na Salama kipindi cha MKASI watakubaliana na mimi huyu Mzee na wengine wengi tunaosikia
wakihojiwa na vyombo vya habari ..wakilaumu serikali kwa kutowajali. Wengi wao walipata 'golden opportunities' za kuwa na maisha bora lakini 'walichezea pesa' na 'opportunities hizo' so many times...

Mfano: Mzee Gurumo jana alisema alilipwa 'elfu ishirini' mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu' sasa pata picha huyu mzee alikuwa na pesa kiasi gani? Na mshahara wake ulikuwa 'shilingi elfu tatu' mwaka hu0 1978... wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'

Kuna Mzee mwingine alitunga kitabu riwaya 'Simu ya Kifo' alilipwa 'elfu kumi na mbili ' miaka hiyo nyumba Kariakoo zinauzwa shilingi 'mia nne' na alikufa bila nyumba wala kibanda..

Orodha ni ndefu...na wapo wengine Baba zetu, Wajomba, babu na kadhalika ukiwaona uzeeni wanavyolalamika na kuomba wasaidiwe.... utasema hawakupata chochote ujanani kumbe anasa, starehe na kuhonga wanawake ndo sababu....

Ukweli ni kwamba watu 'huchezea maisha mno' halafu uzeeni hutafuta wa kumpa lawama mara watoto, mara serikali na kadhalika....

Huyu Mzee Gurumo alikuwa sio mtu wa kupewa gari na Diamond... angekuwa na magari na majumba tele ya kuwarithisha watoto na wajukuu...
 
Nakubaliana na wewe mkuu...

Nilipomsikia akiongea + mambo mengine ninayayaona ya watu kama hawa, natamani kuwapima "size of prostate glands" ili niwape ushahidi kwamba the invested somewhere else!!

Babu DC!!

Mkuu umepotea sana

back to topic
mwenyewe jana alisema mshahara wa 'shilingii mia tatu' ulikuwa sawa na milioni ya leo
halafu akahama bendi na kulipwa mshahara wa 'elfu tatu'
karibu sawa na milioni kumi basi yaleo..
still anadai 'hakupata chochote' na mziki wake
bado 'connections' za watu mbalimbali alizopata
 
The Boss umeongea mkuu. Nilimuona kwenye hicho kipindi na nilijiuliza mengi sana kuhusu huyu mzee kulalamika now kuwa ameimba miaka yote hiyo ila bado anaomba sasa hivi asaidiwe.
Wengi wanapata nafasi nzuri sana lakini wanazichezea au wanatumia ndivyo sivyo kile wanachopata na wanaishia kuwa watu wa kuja kuomba wasaidiwe uzeeni ila wakati wa ujana ilikuwa full kujirusha.
 
Last edited by a moderator:
mfano Mzee Gurumo jana alisema alilipwa 'elfu ishirini'
mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka
kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu'

Say what...? Hizo habari za mshahara wa rais nimekuwa nikizitafuta kwa zaidi ya miaka 6 sasa bila mafanikio yoyote.

Wewe umejuaje mshahara wa raisi Mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 27,000? Enzi hizo mishahara ya viongozi ilikuwa ikiwekwa wazi ama?

Mkapa mshahara wake wakati akiwa rais unaujua? Kikwete je?
 
hiyo ni kweli mkuu sijui wazee hawa wa zamani hawakuwa na ufahamu? mimi naona walikuwa wanapata vitu vingi bure na nafuu so wakajisahau. Nina mfano hai jana tu hapa ofisini kuna mzee mmoja mfanyakazi mwenzangu wao ndo watu wa kwanza kuajiriwa hapa ofisini hiyo ni miaka ya sabini tunakaa njia moja hivi sasa jana kaniona napita zangu kuja job yeye yupo kituoni mm sikumuona sasa akaja ofisini akasema mtani kama nilikuona wewe ukiwa kwenye gari Fulani hivi ila nikajiuliza mbona gari yako ninayoijua sio hiyo? nikamwambia nilikuwa mimi basi akaanza kulalama yani sisi tulichezea maisha mtu ulikuwa unapewa kila kitu bure mwisho wa siku unachukua mwanamke jioni unaenda pumzika nae!! yani kuanzia chakula, bia, usafiri wa kurudishwa home vyote ni bure! sasa anajuta na kusema tazama vijana wa siku hizi mambo yenu yalivyo mazuri sisi tumebaki kuwakodolea macho tu! sasa nashindwa kusema mfumo uliokuwepo ni tatizo au ni akili ya mtu binafsi!
 
daa nilimsikia akisema hivyo lakini interview yake ya jana siku pata kuhitazama.

LAKINI NILIPO SIKIA HAKUWAI KUMILIKI GARI NILIJIULUZA INA MAANA NYUMBA ANAYO? HADI LEO SIJAPATA JIBU KWANINI ALISEMA GARI? HUYU MZEE NI WAZI KWAKE GARI HALIKUWA KIPAUMBELE KABISA NA ALISEMA VILE KUTAFUTA HURUMA TUU.

The Boss HEBU NIJUZE KAMA KWENYE MAONGEZI ALIONEKANA NI MTU MWENYE NYUMBA YAKE NA SIWEZI KUMHUKUMU KWA KUTOKUWA NA GARI BALI KWA KUTOKUWA NA NYUMBA YAKE BINAFSI.
 
Mwaka 1992 nilisoma kwenye gazeti la Mfanyakazi...kama unalikumbuka
na walisema 'mshahara wa Rais wakati huo ni 27,000/-
na bado nakumbuka....hilo...mishahara ya Marais wengine sikupata data
lakini unaweza fanya calculation kwa kuanzia kima cha chini
by the time Nyerere anatoka mshahara wa Rais ulikuwa mara 12 ya kima cha chini
now nasikia ni mara 58 ya kima cha chini
 
The Boss umeongea mkuu. Nilimuona kwenye hicho kipindi na nilijiuliza mengi sana kuhusu huyu mzee kulalamika now kuwa ameimba miaka yote hiyo ila bado anaomba sasa hivi asaidiwe.
Wengi wanapata nafasi nzuri sana lakini wanazichezea au wanatumia ndivyo sivyo kile wanachopata na wanaishia kuwa watu wa kuja kuomba wasaidiwe uzeeni ila wakati wa ujana ilikuwa full kujirusha.
 
Last edited by a moderator:
hiyo ni kweli mkuu sijui wazee hawa wa zamani hawakuwa na ufahamu? mimi naona walikuwa wanapata vitu vingi bure na nafuu so wakajisahau. Nina mfano hai jana tu hapa ofisini kuna mzee mmoja mfanyakazi mwenzangu wao ndo watu wa kwanza kuajiriwa hapa ofisini hiyo ni miaka ya sabini tunakaa njia moja hivi sasa jana kaniona napita zangu kuja job yeye yupo kituoni mm sikumuona sasa akaja ofisini akasema mtani kama nilikuona wewe ukiwa kwenye gari Fulani hivi ila nikajiuliza mbona gari yako ninayoijua sio hiyo? nikamwambia nilikuwa mimi basi akaanza kulalama yani sisi tulichezea maisha mtu ulikuwa unapewa kila kitu bure mwisho wa siku unachukua mwanamke jioni unaenda pumzika nae!! yani kuanzia chakula, bia, usafiri wa kurudishwa home vyote ni bure! sasa anajuta na kusema tazama vijana wa siku hizi mambo yenu yalivyo mazuri sisi tumebaki kuwakodolea macho tu! sasa nashindwa kusema mfumo uliokuwepo ni tatizo au ni akili ya mtu binafsi!

Wanajisahau mno
wakati kila kitu kwao ilikuwa easy
mashamba ya kuomba tu serikalini
viwanja hununui,unalipa tu ardhi unapimiwa
 
Nilizani nipo peke yangu ambae ameliona hilo. Nime kiona hicho kipindi leo nazani yalikuwa ni matudio. Pesa halizo kuwa anazitaja samani yake ilikuwa nikubwa sana kwa miaka ile. Mzee ngurumo hakupaswa kabisa kustafu mziki akiwa nahali hii alionayo sasa. Hakika he did not use is chance good.
 
Ni funzo kwa watu wote hasa Mungu anapokupa
maisha ni vizuri kujipanga ili kuepuka haya ya
Ngurumo maana ukweli ulio wazi unapofikia

Hatua ya Uzeeni hapo ndiyo pia maradhi kama:-

1. Kisukari
2. Presha
3. Figo
4. Kibofu na n.k

Sasa kwa style ya kuomba lazima uchine na
kutoa lawama nyingi sana kwa Watu.
 
daa nilimsikia akisema hivyo lakini interview yake ya jana siku pata kuhitazama.

LAKINI NILIPO SIKIA HAKUWAI KUMILIKI GARI NILIJIULUZA INA MAANA NYUMBA ANAYO? HADI LEO SIJAPATA JIBU KWANINI ALISEMA GARI? HUYU MZEE NI WAZI KWAKE GARI HALIKUWA KIPAUMBELE KABISA NA ALISEMA VILE KUTAFUTA HURUMA TUU.

The Boss HEBU NIJUZE KAMA KWENYE MAONGEZI ALIONEKANA NI MTU MWENYE NYUMBA YAKE NA SIWEZI KUMHUKUMU KWA KUTOKUWA NA GARI BALI KWA KUTOKUWA NA NYUMBA YAKE BINAFSI.

Nyumba sijui but uisishangae akiwa hana
mbona marehemu Mzee Kipara alikuwa hana nyumba
na alikuwa kazaliwa mjini hapa hapa Dar?
na aliajiriwa RTD...miaka hiyo
 
Mkuu umepotea sana

back to topic
mwenyewe jana alisema mshahara wa 'shilingii mia tatu' ulikuwa sawa na milioni ya leo
halafu akahama bendi na kulipwa mshahara wa 'elfu tatu'
karibu sawa na milioni kumi basi yaleo..
still anadai 'hakupata chochote' na mziki wake
bado 'connections' za watu mbalimbali alizopata

Nipo mkuu....nimebanwa kila upande kaka!!

Mbona huyu mzee hatuelezi viwanja vyake vilikuwa ni vipi??

Kuna jamaa alinambia kuwa kila mtu ana ulevi wake...ila kuna watu wanaweza kutawala huo ulevi wao na kuonekana kama ni tofauti na wengine...

These guys messed it up with starehe sasa wanatafuta mtu wa kumbebesha lawama... very bad and shame on them!

Ni sawa na wale wakubwa waliokuwa wanaishi kwenye nyumba za serikali, fully furnished, wakaja kustaafu bila hata kitanda....

Nawashauri wanyamaze na kukumbuka jinsi walivyotesa kipindi ambacho ilikuwa ndiyo zamu yao..

Babu DC!!
 
Mwaka 1992 nilisoma kwenye gazeti la Mfanyakazi...kama unalikumbuka
na walisema 'mshahara wa Rais wakati huo ni 27,000/-
na bado nakumbuka....hilo...mishahara ya Marais wengine sikupata data
lakini unaweza fanya calculation kwa kuanzia kima cha chini
by the time Nyerere anatoka mshahara wa Rais ulikuwa mara 12 ya kima cha chini
now nasikia ni mara 58 ya kima cha chini

Mfanyakazi nalikumbuka sana na coverage yake ya ile kesi mpiga picha/mwandishi wa habari (jina limenitoka kidogo) ndo iliyompaisha Masumbuko Lamwai kutoka kwenye obscurity na kuwa household name. Nilikuwa napenda sana kusoma 'Amini Usiamini'.

Je, kwa sasa umesikia huo mshahara ni mara 58 zaidi ya ule wa kima cha chini toka kwa nani/wapi?
 
Nyumba sijui but uisishangae akiwa hana
mbona marehemu Mzee Kipara alikuwa hana nyumba
na alikuwa kazaliwa mjini hapa hapa Dar?
na aliajiriwa RTD...miaka hiyo

mkuu The Boss hapo ndio ntaamini mzee huyu ni tatizo maana kama hana nyumba nilitegemea aombe mifuko ya cement au bati ili ajenge.
 
Last edited by a moderator:
Mfanyakazi nalikumbuka sana na coverage yake ya ile kesi mpiga picha/mwandishi wa habari (jina limenitoka kidogo) ndo iliyompaisha Masumbuko Lamwai kutoka kwenye obscurity na kuwa household name. Nilikuwa napenda sana kusoma 'Amini Usiamini'.

Je, kwa sasa umesikia huo mshahara ni mara 58 zaidi ya ule wa kima cha chini toka kwa nani/wapi?

Source ya hiyo niliiona kwenye article ya Issa Shivji sikumbuki gazeti...
 
Back
Top Bottom