Wanaume wenye ndoa kuanzia miaka 9. Hawa wengi unakuta wanaanza kugonga miaka 40 na zaidi.
Baada ya kupambana sana na kazi au biashara au kupata cheo hapa ndipo kipimo kamili cha uanaume kinakuwepo wanawake rika mbali mbali hasa mabinti wenye tamaa watakupenda unajua kupendwa wewe??? Watakupenda hasaa na unasema na kuhisi miaka yote mkeo hajakupenda hata siku moja na wanao.
Hapa unaweweseka, utategwa, utasaliti, utaacha mke, utaoa mke au wake utaona wewe kila kitu utatamani hadi majirani uwamiriki.
Ni wachache wanavuka ambao watashinda kama kakazangu mpaka wameeka sasa.
Wanashinda wale ambao waliona fitina wakaweza kwa familia wakashirikisha familia hasa mke baadhi ya changamoto na vipato wakadumisha ndoa zao.
Wanaume msihadaike na hadaa za nje wengi mnatekeleza malengo ya wengine bila kujua na kutelekeza familia.
Unatengeneza BOMU kutegua ni ngumu baki njia kuu fanya mazoezi.