Story ya kweli. Una miaka minne, umbali ni dar kwa arusha .... yamejirudia sana matatizo kila siku.... nadhani matatizo yakizidi ni tatizo kwa kweli na unachosha mwili na roho pia
Asante,
Hujasema kama hilo Swala ni lako/linakuhusu wewe mwenyewe ama ni la mtu mwingine,
Ila, Ili nisikuchoshe kwa maswali zaidi naomba niseme:
Nionavyo mimi,
Hapo kuna kitu (sababu) tena inaweza kuwa kubwa tu na ambayo inautafuna mti wa uhusiano husika chini kwa chini na pengine mti huo ushaoza kabisa unasubiria kisababu hata kidogo tu udondoke kabisa.
MASHAKA
Kauli hizi:
1."Sihangaiki na wewe" anayodai mhusika kupewana huyo jamaa yake.
2."Pamoja na kuwa nina udhaifu nimeomba msamaha...."
Zote zinaonyesha udhaifu, kutokujiamini,kutokujitambua, na kutokujielewa pia kwa upande wa Mwanamke, .
Aidha,"Sihangaiki na wewe",maana yake; Huenda pia Mwanamke ana vijitabia-tabia ambavyo jamaa kachoka navyo na ndio maana ameamua kumpotezea.
AU tena Kakuchoka, Huna thamani tena kwake kama mwenza,.
Na Hii kama unaakili timamu ndio ushapatiwa tiketi ya daraja la kwanza kwamba CHAPA LAPA.unasubiria reporting time tu.
(Yaani kajisababu kadogo hivi, Ili wewe ndio uonekane chanzo cha mparaganyiko)
NG'ATUKA. NDIO ITAKUUMA LAKINI ITAKUFARIJI KUWA UMEACHA NA HUKUACHWA.
-As for, "Kuomba msamaha"- Huku ukijua kuwa wewe ndiye uliekosewa;
Mdada yeyote akinilete kesi ya aina hii,
Nitamsamehe tu kama mtuhumiwa ana ndoa nae lakini u-gelfrend/boyfrend?-Naweza hata kukunasa vibao.
Hii ndio sifa kubwa ya mtu asiejiamini na mwenye adabu ya uoga, Ni sifa mbaya,mbaya,mbaya.na haifai hata kidogo kwa Mwanamke.
Hunijui, sikujui lakini;
However you look, Whatever you have and regardless of Your individual weaknesses.
You have to Know that; You are blessed With a unique beauty and have dignity as well.
Asitokee Mpuuzi yeyote kwa sababu yoyote ile akapelekea ujione hujatimia, hunathamani Au hufai kama Mwanamke.
Kwani ana nini chamno? Jiulize kabla hujawa nae ulikuwa huishi? Ulizaliwa nae? Je Duniani yupo pekeyake?
Kama ishu ni kuwa anakufurahisha na pengine ukiachana nae utakosa furaha lakini furaha yako isiishie kuondoa utu wako, utulivu wa akili na thamani yako kama mwanamke.Yapo mengi ya msingi unaweza kuyafuatilia kwa mustakbali wa maisha yako ya baadae kuliko kuhangaika na kuumiza kichwa kumfikiria mtu ambae hata sababu ya kero zake huielewi.
Umelielekeza swali lako upande wa jinsia ya Wanaume, pengine ukiamini ndiko utakapopata majibu sahihi,
Naomba nikukosoe kuwa pengine hukua sahihi sana.
Majibu sahihi zaidi utapata kwa wanawake wenzako ambao siajabu utakutana na ambao walikumbwa na madhila ya aina yako.
SULUHISHO
Lamsingi,
Wahusika wakae/waonane ana kwa ana na sababu ziwekwe upenuni.
Zama hizi uwe umeolewa au hujaolewa si za kukimbizana na Mapenzi,
Kama mmoja kamchoka mwenzake muambiane tu kama mlivyoambiana wakati wa kutongozana.
Mwisho, Nakualika Usome Siginecha yangu.