Wanaume embu nisaidini hili

Wanaume embu nisaidini hili

Asante,
Hujasema kama hilo Swala ni lako/linakuhusu wewe mwenyewe ama ni la mtu mwingine,
Ila, Ili nisikuchoshe kwa maswali zaidi naomba niseme:

Nionavyo mimi,
Hapo kuna kitu (sababu) tena inaweza kuwa kubwa tu na ambayo inautafuna mti wa uhusiano husika chini kwa chini na pengine mti huo ushaoza kabisa unasubiria kisababu hata kidogo tu udondoke kabisa.

MASHAKA
Kauli hizi:
1."Sihangaiki na wewe" anayodai mhusika kupewana huyo jamaa yake.
2."Pamoja na kuwa nina udhaifu nimeomba msamaha...."

Zote zinaonyesha udhaifu, kutokujiamini,kutokujitambua, na kutokujielewa pia kwa upande wa Mwanamke, .

Aidha,"Sihangaiki na wewe",maana yake; Huenda pia Mwanamke ana vijitabia-tabia ambavyo jamaa kachoka navyo na ndio maana ameamua kumpotezea.
AU tena Kakuchoka, Huna thamani tena kwake kama mwenza,.
Na Hii kama unaakili timamu ndio ushapatiwa tiketi ya daraja la kwanza kwamba CHAPA LAPA.unasubiria reporting time tu.
(Yaani kajisababu kadogo hivi, Ili wewe ndio uonekane chanzo cha mparaganyiko)
NG'ATUKA. NDIO ITAKUUMA LAKINI ITAKUFARIJI KUWA UMEACHA NA HUKUACHWA.

-As for, "Kuomba msamaha"- Huku ukijua kuwa wewe ndiye uliekosewa;
Mdada yeyote akinilete kesi ya aina hii,
Nitamsamehe tu kama mtuhumiwa ana ndoa nae lakini u-gelfrend/boyfrend?-Naweza hata kukunasa vibao.
Hii ndio sifa kubwa ya mtu asiejiamini na mwenye adabu ya uoga, Ni sifa mbaya,mbaya,mbaya.na haifai hata kidogo kwa Mwanamke.

Hunijui, sikujui lakini;
However you look, Whatever you have and regardless of Your individual weaknesses.
You have to Know that; You are blessed With a unique beauty and have dignity as well.
Asitokee Mpuuzi yeyote kwa sababu yoyote ile akapelekea ujione hujatimia, hunathamani Au hufai kama Mwanamke.
Kwani ana nini chamno? Jiulize kabla hujawa nae ulikuwa huishi? Ulizaliwa nae? Je Duniani yupo pekeyake?
Kama ishu ni kuwa anakufurahisha na pengine ukiachana nae utakosa furaha lakini furaha yako isiishie kuondoa utu wako, utulivu wa akili na thamani yako kama mwanamke.Yapo mengi ya msingi unaweza kuyafuatilia kwa mustakbali wa maisha yako ya baadae kuliko kuhangaika na kuumiza kichwa kumfikiria mtu ambae hata sababu ya kero zake huielewi.

Umelielekeza swali lako upande wa jinsia ya Wanaume, pengine ukiamini ndiko utakapopata majibu sahihi,
Naomba nikukosoe kuwa pengine hukua sahihi sana.
Majibu sahihi zaidi utapata kwa wanawake wenzako ambao siajabu utakutana na ambao walikumbwa na madhila ya aina yako.


SULUHISHO
Lamsingi,
Wahusika wakae/waonane ana kwa ana na sababu ziwekwe upenuni.
Zama hizi uwe umeolewa au hujaolewa si za kukimbizana na Mapenzi,
Kama mmoja kamchoka mwenzake muambiane tu kama mlivyoambiana wakati wa kutongozana.

Mwisho, Nakualika Usome Siginecha yangu.

Asante kwa ushauri mkuu
 
maswali yako magumu sana, nimeshindwa kujibu hata moja

yaani wewe ungekuwa mwalimu wanafunzi wangekukoma
 
habari zenu wanajf .....
kuna jambo linanitatiza sana limenikuta mara kadhaa na hata baadhi ya rafiki zangu. nimejikuta na maswali mengi kutokana na hilo jambo:
  • mnaposema unataka niwe hot maana yake nini? au unataka niweje?


  • mwanaume upo mbali na mimi may be mkoa mwingine alafu unaniambia sihangaiki na wewe.. wakati muda wote najitahidi kupiga simu kuchati ? kwa hapa huwa mnataka tufanye nini?


  • ulikuwa mbali penzi lililegalega umekuja karibu unaamua kuniacha kuna kuwa kuna nini hapo jamani?


  • unapopigiwa simu upokei alafu baada ya mda unakuja kupokea au unapiga ujaulizwa unaanza kunifokea na kunigombeza huwa hapo unaficha nini ?


  • pamoja na kuniambia kuwa naudhaifu huo nakuomba msamaha na kutaka kurudiana na wewe bado unakataa tena kwa nguvu zote. najiuliza ni kwamba katika mazuri yote nayo jitahidi kufanya uoni unaona, visababu vidogo?
wanawake mnakaribishwa ila nilitaka wanaume ndo wanijibu ...jamani napata wakati mgumu sana hata kufikiri kuanza upya katika mahusino mengine nahisi ni yale yale tu..... wapenzi wangu nipeni maujanja nifanyaje mimi.... ila theory practical nitafanya mwenyewe....

naombeni msaada wenu please..
asante mbarikiwe

bila shaka huyu ndiye wa kumlaumu.
Ndoa unaitafsiri vbaya kutendwa au kutoelewana sio kwamba ndo kukufanye uichukie ndoa.
 
Uwe na mvuto kimapenzi. Yaani ujiweke vizuri.

Kwa mfano, ukiwa umejaaliwa ile chakula ya mtoto, si mbaya mara moja moja kuonyesha ubunifu. Onyesha ule mgawanyo (cleavage), nifanyie shimmy, vaa sketi zenye slit....

Ukivaa viatu vya kokoko basi badili mwendo...tembea kaa Naomi Campbell kwenye catwalk

Kuwa msafi, nukia vizuri, floss meno, kuwa na meno meupe, paka viondoa harufu (deodorant) - kama antiperspirant zinakupa shida basi uwe unaweka armpit pads kuzuia jasho kuvuja kwenye kitop chako...


In a nutshell, be a lady in the street but a freak in the sheets.

Hahaaaaaaaaa nimeipenda hiyo ya viatu vya kokoko na mwendo wa naomi loo
 
Wanaume ni wabaya wanyama wauwaji wanyanyasaji

hii thread yako ilikuwa inanijia kichwan kila siku skujua kwann umelalamika hivyo lakin nilipoona kaulizako humu nikaona ngoja nikuibulie hapa.
Bila shaka huyu mtu uliyemlalamikia hapa ndiye kakufanya uchuki raha ambayo wenzako wanaipata. Jaribu ingia ulimwengu wa wapendao.
Bebe wangu christine ibrahim anajua hilo
 
Last edited by a moderator:
hii thread yako ilikuwa inanijia kichwan kila siku skujua kwann umelalamika hivyo lakin nilipoona kaulizako humu nikaona ngoja nikuibulie hapa.
Bila shaka huyu mtu uliyemlalamikia hapa ndiye kakufanya uchuki raha ambayo wenzako wanaipata. Jaribu ingia ulimwengu wa wapendao.
Bebe wangu christine ibrahim anajua hilo

Not men only myself naweza jipa raha
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom