Wanaume ebu semeni hisia zenu ktk hili

Vituka

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
2,257
1,246
Ulikuwa na girlfriend, mmedumu nae kwa miaka 4, mkaachana. Mlikuwa na marafiki wengi tu, wake kwa waume, uliowatambulisha kwake na waliotambulishwa kwako. Baada ya kuachana, msichana anakutana na rafiki yako mmoja, alikuwa hajui kama mlishaachana, na baada ya maongezi anagundua hilo. Wakapeana namba za simu na kwa bahati ofisi zao ziko jengo moja. Lunch wanaenda wote sometimes, na hata mitoko ya weekend wanaweza kuwa wote (huyo mwananume ana mchumba na sometimes wanakuwa wote watatu). Siku moja mdogo wako anawakuta restaurant wanapata lunch, anakupa izo taarifa, je utajisikiaje?
 
hahaa ukisema cha nini mwenzio unawaza atakipataje.kwani rafiki nduguyo?jisikie furaha kwamba x bado ana thamani

Na ambaye anatoa povu na cheche akiona X yuko na rafiki yake tumueleweje?
 
Unamshukuru Mungu kwmba bdo yupo hai. Ss wewe unataka ujickiaje wakati mmeshaachana?
 
halafu me huwa nawaambie watu siku zote mpenzi sio ndugu yako when its over its over me hata kama tumeachana uzuri tena kwa kupeana zawadi nakueleza kabisa tukikutana hunijui sikujui hatukuzaliwa wote undugu ndo haufi
 
Sina chochote cha kujisikia,kama tulishaachana me sina neno nae aendelee tu..
 
Kama mmeachana hakuna yeyote kati yenu anayetakiwa kujiskiaje..
bygones are bygones..full stop!
 
Mkuu kama ulikuwa na mahaba ya dhati na yeye ofcourse lazima itakusumbua.. Maana deep in ur heart unajua kwamba anaendelea mbele na maisha yake wakati wewe bado moyoni yupo.. Na vile vile utakuwa unajicikia wivu kwa kuwa yuko karibu sana na rafiki yako.. Swali la muhimu la kujiuliza.. Jee.. mliachana chini ya mazingira gani..? bado wampenda..?
 
we utakuwa umepita na X wa rafiki yako unatafuta justification!!!!!!!!!!!

Sijakuelewa mkuu, X wa rafiki yako ndo nini sasa? Mwanamke alikuwa anapata luch na rafiki wa X wake, mbona unachanganya madawa
 
Sina chochote cha kujisikia,kama tulishaachana me sina neno nae aendelee tu..

Safi sana salito, ila kwa nini wanaume wengine huwa wanachukia na hawapendi? Au ndo sitaki nataka
 
Mimi ntajisikia poa tu....kwa si tumeachana,...


Off topic:wanawake kwa upande wenu je...?
 
kwa nini ujisikieje wakati mlishaachana.....?

Preta nimeuliza ili nipate opinion za wanaume wengine kwani kuna X anaumia sana na amejenga bifu na huyo rafiki yake. Ivi inauma kama vile rafiki yako akitembea na dada yako au!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom