Story: Fumanizi la ukubwani

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,919
14,800
OYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!

Naskia mmenimiss Kinoumaaaaaaa, muhahahahahahahahaha ( In Monster's Voice)

Sometimes its good kuadimika ili utengeneze maisha, $$$$ beeeeibeeee
Hivi lara 1 yupoooooooo na Vladimirovich Putin na data na miss chagga na Natafuta kiki Miss Dimples dillema Ambiele Kiviele MPOOOOOO?!

Merry Christmass Retrospectively kwenu wote na Happy Coming New Year 2018 in Advance

Gaaaad I miss you Guys!


Ila sio kiviiiile :p

anywho back to what am good at... hehehe... kwangu sihitaji Gris kitu cha Talent!


SEHEMU YA 1​

KIDAWA ni jina lake maarufu, KICHWA PANZI ni jina lake la nyumbani.

Shogangu huyu bwana, alidandia gari kwa mbele kwa maelezo ya kusikia toka kwa shogake mwingine akaona ige, hii kuiga vepe sasa? akafika sehemu akakwama akaniomba msaada nimsaidie anataka kujimaliza , bora afe kuliko kuendelea kuishi bila watoto na mume wake

money Penny: Kidawa Kidawa wewe, embu tulia kwanza basi, hii kesi ya nyuki pelekea malkia wake, kama sisi kwanini ujiue labda?

Mbinguni unawahi kufanyaje sasa? kuimba kwaya au?! Na mechi za kila siku unamwachia nani labda?!

Basi kichwa panzi akapoa, akatuliaaa, akaanza kufunguka

KICHWA PANZI:
Money Penny we wangu tu wala sikufichi
Hii michezo ya Yondo sister tuwaachiwe Mama zetu na Mama wakubwa na wadogo, sisi tuliozaliwa miaka ya 79-82 ni wa akina JLo.

Mume bwana alisafiri kimasomo, nchini Chinaaaa! kwa muda wa miaka miwili, kila mwaka anakuja Tz, mimi nikabaki na watoto

Basi nikaskia shogangu KISODA anajigamba, mimi nina mume lakini bado ofa za nje nachukuaaaaa, tena mume akisafiri ndio kakoseaaaaa!

KISODA akajigamba wee nikamwambia basi tumwite Money Penny atuvushe akakataaa. Nikamwambia nipe ubuyu dadalake, mama la mama, Lemutus hana shida na wewe anashida na Mange Kimambi tuuu, ila wewe ndo wewe, nikamsifia pale akajaa kichwa akaanza kushuka audio!

Akanipa maujanja akaniambia kwanza kuna MSUMENO unatafuta pa kuhemea, sumeno la kikenya, kuna BISIBISIya Kibongooo, kuna PLUG ya kibongooo wote wapo wanatafuta pa kuhemea

Nikamwambia niingize mama niingize weeee, niweke front,
KISODA akani connect na ma Sponsor hao dadeki, sponsor wana hela mjiniii afu zote safiii afu ni nyingiii babake!

Nikaonana na MSUMENO tukaongea wee tukapendana wee tukapanga na siku ya ku-do!. Baada ya wiki 2 tuka do na kinga lakini, akanipa laki 3 nikaondoka nikajua nimemalizana nae!

Cheee! Msumeno sijui alinogewa basi kila siku simu simu kama customer service, oh nataka kukuona and shit, nikaenda round ya pili tukanyooshana nikasepa akawa bado ananigandaa

Nikamuvuzisha majeshi kwa BISIBISI, aisee Mbongo Mbongo sijui Mangi yule maana ni shida anang'ang'ania Mkenya atasubiri miaka 1000
Nikajaribu kumkwepa wapi ila mchaga nomaaa, anatoa hela mpaka nikashangaa!

Mmachame gani anarusha hela kama DJ KHALID?!

Basi Penny, nikawa napokea kwakweli kati ya MSUMENO na BISIBISI, anaeongoza kwa kutoa pesa BISIBISI no 1.

Huku mume anapiga simu anatuma hela za familia, hizi za pembeni sasa kudadeki naziweka kwenye akaunt, si unanijua mtoto wa Kitanga,

Nikaenda kumcheki PLUG, kiru! Plug nomer sana, plug ana ma care hatarious, plug anakufungulia mlango wa gari, anakufungia, ukifika anakuchum, mechi usiseme si unajua Wanyakyusa tena, ila huyu mnyakyusa k/nyoko kitandani nilisalimu amri

Basi mume akarudi zake Tz likizo nikaficha namba ya simu ya madhambi yangu, aliporudi shule nikarudisha majeshi, nikaweka line ya Airtel kufungua simu nina sms za kutosha, Mpesa pending zimerudi, Kha nikaona sio ishu, nikawarukia hewani
Wakazirudisha pesa

Kashehe imenikutia hapa. Wakati mume yupo masomini buana, me nikaenda out na BISIBISI, mmachame masifa hatari, kufika dinner mara whuuuuuuu, goti chini will you marry me, nikasema tobaaaaaaa!

Watu hotelini wakaanza kujaa, mara wachukue ma selfie, makofi kibao, hapa hapa dar DVD imechezwa Chinese Dragon restaurant... nikaona isiwe kesi, nifunike Kombe mwana haramu apite, nikakubali kupunguza attention ya watu hotelini

Baada ya mwezi mmoja PLUG akaniomba tuonane, me kama kawaida chek noris navua gwanda (pete za ndoa) tupa kuleee, nikajisogeza tukaenda Tabata Green View Hotel, kula na nini tukazama kwenye mechi, kuamka asbh jamaa sijui ndo ulimbukeni au sielewi ak- propose tukiwa kitandani watupu!
Mmh nikaona hapa sass ni balaa, kwa mauno gani mpaka niwe proposed in 2 month friendship? tena ya kujiiba?!
Nikakubali na fake smile yangu kumridhisha na mahaba lukuki, kurudi nyumbani pete nikaiweka kwenye sanduku chiniii!

MSUMENO sikuwahi kumwona kabisaa, akaja akaibuka mwezi wa 6 wakati naendelea kuzipanga karata zangu sawa kati ya PLUG na BISIBISI, naona simu whuuuu! Cri cri cri cri nikapokea najua mume kumbe MSUMENO, tukaongeaa anasema alienda kwao Kenya visa iliisha ilikuwa ghafla na kamata kamata ya serikali akaona aende bila kuaga, appologies kibaaaao nikamwambia usikonde, pole sana,

leo uko wapi mpenzi, mimi niko posta, njoo basi Serena Hotel hapo nikiangalia watoto wote wapo shule, watarudishwa na school bus,

Ofisini Boss katoka mapema, nikaamua kujistretch mpaka Serena Hotel, Lunch nene nini, akachukua room, tukapiga uzinduzi mpaka saa 3 usiku nikarudi home
Kesho anataka tenaaaa, nikampaaaa
Kila siku anatakaaa nikamwambia bwana weee, usinipande me sio kichongeo cha kuchangamsha dyu dyu ichongeke nimechookaaa

Huku BISIBISI na PLUG nao wapo mwake kama nusu ya Eifl Tower Paris wanawaka sio kidogo oh baby nataka kukuona kwako, oh baby nataka kulala kwako, mimi nawadanganya baba mkubwa mkali sana, kwanza hawaamini proposal za nje wanapenda protocals

BISIBISI akaniambia niambie lini nilete wazee

PLUG nae wimbo ule ule wa ndoa ndoa ndoa!

Nilipoharibu ni hapa sasa, baada ya purukushani ya mwaka na miezi 3, KISODA yeye kakomaa kwenye hili game hata anitafuti, siku nipo zangu natoka Bank MSUMENO huyooo,

ah baby nakuona umependeza sana, ile anataka kunikumbatia mara BISIBISI huyooo, anashangaa mbona nashikwa shikwa kimahabaaa flan hivi?! hapo tupo posta mpya CRDB Azikiwe branch kwa nje, shoga nilipaona peusi ghafla, kila mtu ananiuliza, huyu nani huyu nani

Mlinzi akaja: Tadhali hii sio sehemu ya maongezi, naomba mpishe maongezi yenu pelekeni kule mbele kwa mbeleee

Tukasogea mpaka parking ya Azikiwe kila mtu anataka maelezo, pete niliovaa ya PLUG naulizwa hii pete ya nani, kufekisha siwezi, mateja wale wapiga debe washaanza kujaaa,

Wale mabwana wametukakanana mimi nipo kimya kama dada yao kumbe bibi yao, huyu anatukana kikenya huyu matusi ya kibongo mara nikaona gari hiloo, PLUG ananiita we mrembo twende basi mbona umemalizana na bank haujaniambia twende bwana, tobaaaa! Nilihisi moyo umesimama penny!

Ile nanyanyua mguu niende kwa PLUG nikavutwaaa less wig langu,unakwenda wapi we malaya, nikavutwa less wig la kubond likaanza kusogea pembeni noma, yani ilikuwa ni balaaa! PLUGF akapaki gari, akaja kunitetea basi ni sheedah, haelewi kinachozungumzwa anaona hawa mabwana kama wenda wa zimu, mara likaja bus la mwananyamala nikanyata wiiiiii mpaka kwenye buss uzuri lilikuwa limejaa, nilipoingia tu ndani nikachuchumaaa, namwambia dereva ondoa gari plz nakufaaa dereva plz dereva, akawa anashangaa huyu mwanamke vepe?

namwambia ondoa gari kuna majambazi yananifuatilia si unaona nimechuchumaaa, basi dereva kweli akanihurumia akaondoa daladala, hapo nashukuru Mungu, wale majamaa kugeuka hamna demu, wanajaribu kunitafuta hawajui nimeenda wapi, mimi nawachungulia kwenye daladala lililojaa huku nacheka sasa dereva anashangaa,

kwakweli Penny sijui iliendeleaje ile kasheshe lakini mimi namba ya simu niliitupa barabarani kabisaa

Nikakaa miezi michache mbele mume akarudi (moja kwa moja) for good hapa ndo niliona rangi zote duniani

Siku tumetoka zetu out tunarudisha penzi on a date night, mara PLUG huyooo,

PLUG: Enheee nimekutafuta mwizi wangu, yani leo upo na bwana mwengine tena? aki we kweli ni shida!

Mume: we unamtafuta mke wangu kama nani?!

PLUG: Mke?! Mkeo kivipi labda? ivi kwani we dada umeolewa?

Mimi: ndio, mimi ni mke wa mtu, wewe kaka vepee, kwani wewe nani unapamia tu wake za watu barabarani au umenifananisha?! mimi sikujui au unataka nikuitie mwizi?!

PLUG: we dada si nimelala na wewe juzi tu, na nimekuvisha pete ya uchumba, akaanza kutaja mahoteli yoooote, mume ananiangalia mimi nimekaza uso, namsikiliza kwa hasira namwambia mume bwana vichaa skuhizi ni wengi sana achana nae tuondoke, pete gani anaongelea pete yangu ya ndoa si hii baba nanihii we kaka hii pete yako au? uso mkavu kama hindi la kuchoma

PLUG aliniangalia hakuamini jinsi nimemruka, basi Mume akanishika kiuno huku anamwambia PLUG acha ubwege tutakuitia mwizi nyau wee, tukaondoka tumemwacha PLUG anatuangalia

Baada ya miezi 3 mbele tena, kumbe wale mabwana walikutana wakakaaa wakaongeaaa wakapanga na kupangua, kumbe ule ule usiku nilikutana na PLUG aliichukua PLATE no ya gari ya mume wangu, si wakamsaka wakapata no yake wakamwita, ndio kumweleza kiiiila kitu Mume haelewi anaona kama movie ya Isidingo isioisha, mtoto wa Kitanga nilipatikana nikakumbuka kuwa Kisoda ni Kisoda hawezi fanana na Kichwa panzi

Mume kuja anauliza kila kitu mimi nakataaa katu katu tunagombana sio kitoto, anauliza pete zikowapi kumbe nilishayeyusha kwa sonara muuudaaaa hela zipo benki

Nikapigwaaaa weee, mimi bado uso mkavu, si hana prove, ni maneno na kapicha kamoja tumepigwa na hotel manager ile sikuile nilivishwa pete, nikamwambia ah huyu kama nimesoma nae anapenda kunitania tania hapa aliniita tukaongee, akaniambia kuna demu wake anataka kumfanyia surprise, ni kaka mmoja mcheshi tukawa tunataniana pale we domo zege hauwezi kumvisha mtu pete, akaniambia ngoja nikujaribishe uone ndio hapa akanijaribisha na manya kushangaa ilo tu mume wangu hamna kitu cha ziada, hawa wanaume wanataka kutugombanisha tena nikikutana na huyu rafiki yangu atanikomaaa!
Mume wangu sijafanya haya yote waliosema

Sasa katika pigwa pigwana vipondo visivyoisha toka kwa mume nikamponyokaaa ndio breki ya kwanza kwako Money Penny wangu

Hii kesi ya Kenge lazima nilete kwa Mamba AMBAYE ni wewe Penny:

Doh! eti ingekuwa ni wewe ungemsaidiaje KICHWA PANZI?

MUENDELEZO BONYEZA HAPA FUMANIZI - .

 
Hii story , imefanya asubuh yangu kua nzuri , nakupitia hii story nategemea siku yangu nzima ya Leo ikwishe vizuri.

Aiseee Money Penny ,,, Tushituane sehem ya PILI !!!.sitaki niikose !!
 
Ulikuwa wapi!??
Nilipigwa Ban from June to Dec nikafungua website yangu nikawa naandika stories akaja mtu akainunua hii ya fumanizi orijinal story Juzi Dec 15 nimesaini dola 10,000 sawa na Tsh 22,400,000

Akitengeneza movie napewa 10% ya mapato yote

Subiri kitabu kitoke nitawatonya pa kuvipata

Mlango mmoja ukifungwa JF mwengine Mungu anaufungua kwa website
 
Amen.. Be Blessed Chile!
Nimeona skuhizi unaandikaga thread Hongera sana
Yaaahh ,ulipotea sana my chickade ! Duuuhhh...yeah siku izi naandika andika thread kuchangamsha majukwaa!.

Hakika when door A is closed ..Huwa kuna namna tu ambayo Door B itatokea !!..

You are always strong , determined so keep it up Kitty !!.
 
Yaaahh ,ulipotea sana my chickade ! Duuuhhh...yeah siku izi naandika andika thread kuchangamsha majukwaa!.

Hakika when door A is closed ..Huwa kuna namna tu ambayo Door B itatokea !!..

You are always strong , determined so keep it up Kitty !!.
Thank u darling
Hongera sana hivyo hivyo na wewe utafika
 
Wha!aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaat Pole sana and Hongera saaaaaaana.

Ilove yoooouu Money penny jamanii mimi:(:(
Nilipigwa Ban from June to Dec nikafungua website yangu nikawa naandika stories akaja mtu akainunua hii ya fumanizi orijinal story Juzi Dec 15 nimesaini dola 10,000 sawa na Tsh 22,400,000

Akitengeneza movie napewa 10% ya mapato yote

Subiri kitabu kitoke nitawatonya pa kuvipata

Mlango mmoja ukifungwa JF mwengine Mungu anaufungua kwa website
 
Back
Top Bottom