Wanataka kuufuta Mfuko wa wafanyakazi wa WFC, hivi Serikali haioni hata aibu?

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
653
1,058
Wewe ni Waziri mzuri ndiyo. Unajitahidi kufanya kazi zako vizuri - hulali usiku na mchana ndiyo maana ukafanikiwa hadi kuifukuza corona. nchini mwetu. Uko vizuri sana.

Mwanzoni mwa juma lililopita Tarehe 21 Julai 2020 baba mdogo wangu anayefanya kazi mgodini akawa ananipiga stori kuwa Serikali inafanya utaratibu wa kuunganisha Mfuko unaosaidia sana wafanyakazi wanaopata ajali na wanaougua magonjwa yanayotokana na kazi wanazofanya WFC na Mfuko wa Bima ya Afya NHIF. Mfuko huu wa WFC ulianzishwa miaka mitatu iliyopita na umekuwa tegemeo sana kwa wafanyakazi wengi na hasa wa migodini na wanaofanya kazi kwenye majengo na mabarabarani.

Ukweli kabisa kabisa Serikali hapa inataka kuchemka kabisa. Ba mdogo Mabula kaniambia anayeshinikiza Mifuko hii kuunganishwa ni Waziri wa Afya ambaye anataka Mfuko wake ambao umeshindwa kuwasaidia wafanyakazi wa umma kupata huduma za afya akifikiri kuwa Mfuko wa WFC utasaidia kuondoa shida zilizopo kwanye Mfuko wa NHIF.

Mpaka sasa hivi tayari Serikali kupitia Bunge imeshapitisha Sheria ya kuunganishwa mifuko hiyo na Sheria bado inasubiri kusainiwa na Rais tu ianze kutumika. Mimi napenda kuto angalizo kuwa Mfuko huo wa WFC haupaswi kuunganishwa na NHIF kwa kuwa itaturudisha nyuma kabisa enzi mtu akiumia kazini analipwa shilingi 108,000/-.

Yeye Waziri na Viongozi wengine hawatarajiwi kupata ajali kazi na hata kazi wanazofanya haziwezi kuwaletea magonjwa. Serikali juzi juzi waliunganisha mifuko na kuwapunguzia mafao wafanyakazi. Leo tena wanataka kuufuta Mfuko wa wafanyakazi wa WFC - hivi Serikali haioni hata aibu?

JPM wewe unatoka mikoa ambayo ina migodi mingi - inakuwaje leo unataka kutunyanganya Mfuko huu? Hivi unajua bughdha wanazopata wale wanaoutumia bima za NHIF - hivi unajua wale wanaoohudumiwa na WFC wanasimulia nini kuhusu Mfuko huo?

Tafadhali sana sana Magu kama unapenda wafanyakazi wako usifute huo Mfuko na wala usiunganishe hiyo Mifuko. Kama tatizo ni uongozi wa Mfuko huo wewe ni Rais weka watu wengine wausimamie ingawa kiukweli huo Mfuko unatusadia sana sisi wafanyakazi. Waziri Ummy anafuata tu maelekezo hawezi kukushauri vizuri lawama zitakuja kwako!
 
Mkuu Kuna mlundikano wa taasisi nyingi zinazofanya kazi sawa..

Acha ziunganishwe tu, maana majukumu yao yataendelea kufanyiwa Kama kawaida tatizo ni kuacha sheria zifanye kazi
 
Mkuu Kuna mlundikano wa taasisi nyingi zinazofanya kazi sawa..

Acha ziunganishwe tu, maana majukumu yao yataendelea kufanyiwa Kama kawaida tatizo ni kuacha sheria zifanye kazi
Mifuko imekuwa mingi na makato pia ni mengi kwa mwajiri na mtumishi. Bora kuiunganisha
 
Mkuu Kuna mlundikano wa taasisi nyingi zinazofanya kazi sawa..

Acha ziunganishwe tu, maana majukumu yao yataendelea kufanyiwa Kama kawaida tatizo ni kuacha sheria zifanye kazi
Wewe hufanyi kazi wewe ndiyo maana unabwabwaja kwa usichokijua
 
Endeleeni kuchagua Raisi na wabunge kutoka CCM mpaka akili ziwakae sawa.

Watu wanadhani mtu kama Abbasi Tarimba au kimei(kama atapitishwa) ndio watakuja kutetea wananchi Bungeni iwapo watafanikiwa kuwa wabunge.

Mbunge wa CCM hata wawe tajiri au maarufu kiasi gani,Bungeni hawazi kuwa na msaada kwa wananchi zaidi ya kuwa mtetezi wa serikali.
 
Wewe hufanyi kazi wewe ndiyo maana unabwabwaja kwa usichokijua
Wafute tu.
Make inaonekana waathirika wa haya mambo wapo mtandaoni. Mtaani hatuwaoni.
Wafute tu kama wanaona ni sawa.
Kwan hicho chama hakina uongozi?
Wanachama wake huwa hawakai vikao?
Au ndo ule unafiki mnapiga kura za ndio mkija huku mnaanza kulalamika.
Nasema WAFUTE .
 
Tafadhali sana sana Magu kama unapenda wafanyakazi wako usifute huo Mfuko na wala usiunganishe hiyo Mifuko. Kama tatizo ni uongozi wa Mfuko huo wewe ni Rais weka watu wengine wausimamie ingawa kiukweli huo Mfuko unatusadia sana sisi wafanyakazi. Waziri Ummy anafuata tu maelekezo hawezi kukushauri vizuri lawama zitakuja kwako!
Kwa hiyo tatizo ni kuunganishwa kwa mifuko au mafao? Maana hujasema sheria inayoziunganisha inawanyima vipi mafao yenu. Naona malalamiko na hofu badala ya hoja. Serikali kuunganisha hii taasisi hizi hasa za compliance ni jambo la kupongezwa maana inarahisisha sana kuwa compliant kibiashara.

Tanzania ina mambo mengi sana kwenye compliance na kama hii kero inapunguzwa au kuondolewa ni habari njema sana.

Nakushauri uisome hiyo sheria na uweke hoja za kinachokosekana badala ya kutetea uwepo wa taasisi, jambo linalotia shaka nia yako hasa...
 
Back
Top Bottom