Wanasiasa waliosema wamehama vyama vyao na kujiunga na CCM kwa kuwa wananafurahishwa na Magufuli, siku Magufuli muda wake ukiisha wataenda nae Chato?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Hakuna kitu kilichokuwa kikinishangaza - kama sio kuchefusha, kama kumsikia mwanasiasa, mwanaume au mwanamke mzima ambaye tunatumaini ana akili timamu na za kutosha, akitamka hadharani kwamba ameamua kutoka chama chake kwa kuwa eti amefurahishwa sana na Magufuli!

Hivi kweli hawa wanasiasa hawaoni aibu kutamka maneno kama haya mbele ya watu?

Wote siku zote tumeamini kwamba mwanasiasa anakuwa mwanachama wa chama fulani kwa kuamoni itikati au sera za chama hicho. Lakini mwanasiasa kuonyesha kwamba yeye suala la itikadi au sera za chama sio muhimu bali mtu fulani baki katika chama ndio anamvutia kiasi cha kuacha chama chake, huo ni ulevi na ujinga wa kisiasa ambao unatia hata aibu kuusema hdharani.

Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kwamba kuna watu katika siasa ni malaya wa kisiasa (political prostitution). Naamini kabisa alikuwa akiongelea watu kama hawa pia. Na baadae aliongelea kwamba kumpenda mtu na kutumia mapenzi hayo kwa mtu binafsi kama msingi wa kufanya uamuzi wa kisiasa haifai kabisa, kwa kuwa kupenda kwa namna hiyo kunapaswa kuhusianishwe na kutoleana posa! Alisema peleka posa tukacheka bila kuelewa aliwaza mbali sana.

Mimi nilitegemea kwamba wanasiasa hawa, hata kama ni kweli walihama vyama vyao kwa kufurahishwa na Magufuli, basi angalau wangekuwa na aibu ya kutuambia "nimehama chama changu kwa kuwa nimeipenda CCM na sera zake", sio "nimehama chama changu kwa kuwa nimempenda Magufuli". Huwezi kuwa mwanasiasa mwenye akili sawasawa ikiwa unahama chama chako kwenda CCM kwa kumfanya Magufuli ndio CCM.

Hebu fikiria, wewe unahama Chadema au CUF, na unajiunga na CCM kwa kuwa unafurahishwa na Magufuli. Sasa siku Magufuli akimaliza muda wake, au hata akishindwa uchaguzi wa 2020, utaenda aye Chato ukasaidiane kazi za nyumbani kwake na Mama Magufuli? Au tutarajie kwamba Magufuli akiondoka ikulu basi hawa wanasiasa itabidi watutangazie tena kurudi vyama walivyotoka kwa kuwa Magufuli sio raisi tena?

Kwa kweli akili ni nywele.
 
Mwenyekiti yeyote wa CCM baada ya Magufuli, akiwa na akili nzuri itabidi awaweke mbali kabisa hawa wanasiasa waliohamia CCM kwa sababu ya kufurahishwa na Magufuli. Walimfuata Magufuli sio CCM!
 
1590742880822.png
 
Watu wanaangalia kuvuna chao Sasa hivi waliopata nafasi. Mtu aliyepata kuvuna kwa miaka kumi kwa hyo aache hiyo nafasi aanze kuwaza sijui meko akistaafu itakuaje
 
Watu wanaangalia kuvuna chao Sasa hivi waliopata nafasi. Mtu aliyepata kuvuna kwa miaka kumi kwa hyo aache hiyo nafasi aanze kuwaza sijui meko akistaafu itakuaje
Na kama wamemfuata Magufuli basi ni wazi watamfuata hadi Chato! Sasa watakuwa wakifanya nini Chato hilo ni swali la majibu mengi!
 
Taarifa kwa waliohama ni kwamba wote hawatateuliwa na CCM hata wakishinda kura za maoni!
 
wamefata chama chenyekuleta maendeleo.
Chadema hata ofisi hawana pamoja na Lowasa kuwahonga pesa za kutosha.
 
CCM Ina vyeo vingi mtu hata akishindwa ubunge viko kibao serikalini na kwenye chama .Hamna shida
Mleta mada ya CCM tuachie wenyewe
 
Tunaweza kuwa naye kwa kipindi kirefu zaidi ya mnavyotarajia, ni kujipanga kisaikolojia
 
Namna wanavyo address hii issue ya wahamiaji inakatisah tamaa wafia chama, watu wanakuja leo kesho wana mashangingi ya Serikali - hata kama ningekuwa mimi roho lazima iniume aisee!!
 
Mla mla leo bwashee, the future is uncertain.... don’t calculate it too much.
 
Back
Top Bottom