Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,330
- 24,213
Mambo ya kijinga huwa yanaanza hivi hivi kiutani.
Kilichofanyika Chato na UVCCM kwa mtu asiyeona mbali, utafikiri ndio siasa zenyewe lakini mambo yanaweza kulipuka beyond control.
Siasa za vyama vingi zipo kisheria na sasa ni sehemu ya katiba yetu inayotawala.
Matamshi tuliyosikia kutoka Geita, eti kiongozi wa CHADEMA, Tundu Lissu asikanyage Chato, ikifuatiwa na kuchoma moto gari la CHADEMA, lina hatarisha amani na siasa za Tanzania.
Hili haliashirii siasa za kistaarabu nchini. Rwanda mambo yalianza hivi hivi kwa chuki kuanza kutawala badala ya sera na ilani za chama husika.
CCM Taifa inabidi ilikemee hili na wahusika wachukuliwe hatua. Kutamka chuki na kuchoma magari moto haviwezi kuwa sera za CCM.
Pia soma: UVCCM Chato: Hatutaruhusu kuona hata hatua moja ya Tundu Lissu ikikanyaga Chato. Tupo tayari kwa lolote