Wanasheria wa Serikali Wakwama Mahakama ya Kimataifa. Bilioni 300 Kuchotwa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,046
49,730
Yaani Bilioni 300 ambazo ni sawa na pesa ya kujenga km 250 za Lami tunaenda kuwalipa Matapeli wa Indiana Resources ambao Wanashulikiana na Mafisadi wa Serikalini.

Daa inauma Sana aisee
---

1707418227745.png
Mapendekezo au hoja mbili kati ya tatu ilizowasilishwa na Tanzania kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) yamepigwa chini.

Serikali iliwasilisha hoja hizo baada ya ICSID, Julai 2023 kutoa hukumu, hivyo walitaka Mahakama hiyo kufuta hukumu inayoelekeza kulipa fidia ya Dola 109 milioni za Marekani (Sh272 bilioni) kampuni ya Indiana Resources (IDA).

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya ICSID hela hiyo imefikia Dola za Marekani 112.9 milioni (Sh282 bilioni) pamoja na gharama za ziada za Dola 4.2 milioni (Sh10.5 bilioni) ambayo ni jumla ya zaidi ya Sh292 bilioni.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo riba ya Dola za Marekani milioni moja (Sh2.5 bilioni) itaongezeka kila mwezi hadi Tanzania itakapolipa kiasi hicho au Indiana itakapozuia mali ya Tanzania itakayoendana na thamani ya madai hayo.

Desemba 2023, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania alitoa barua ya uthibitisho kwa ICSID kwamba Tanzania ingelipa bila masharti na bila kubatilishwa kiasi chote cha fedha hiyo ndani ya siku 45 baada ya uamuzi wa mwisho wa kubatilisha. Hata hiyo ni takribani miezi miwili sasa tangu hilo litokee.

Mapitio ya Tanzania kubatilisha kesi yatafanywa Machi 15, 2024 na wadai kujibu Aprili 26, 2024. Kisha kila upande utakuwa na majibu yao mtawalia.

Mei 24, 2024 na Juni 21, 2024 kutakuwa na mkutano wa pamoja wa wiki tatu kabla ya tarehe ya mwisho ya maamuzi.

Mwananchi
 
Nadhani ni bora kushughulika na kiini cha hizi kesi kuliko matokeo ya hizi kesi .Mfano tushugjulike na watu wanaojicommit au kuingia mikataba isiyo na afya kwa Taifa .Ni ngumu sana kwa wakili anae lipwa milioni kwenda kushinda kesi ya billions .
 
Back
Top Bottom