Nakataa MM,
Kimsingi umetoa maoni yako na yana mantiki lakini I dare say sidhani yawe applicable mpaka kwa hili coz siligroup katika mazingaombwe...
Credit should be given where it deserves
Binafsi sitashangilia hata chembe kwa kuwa, endapo leo nitaombwa kutaja taasisi moja inayopaswa kuvunjwa within a minute; basi sitapoteza hata nukta moja kuitaja TAKUKURU!! TAKUKURU ni janga, si janga la kitaifa, bali ni janga la dunia. Sawa na ambavyo mababu zetu walivyokuwa wanaitumia mibuyu, mapango na miti mikubwa kuhifadhi zana zao za matambiko na kafara; ndivyo ambavyo leo hii TAKUKURU inavyotumika kuhifadhi tunguri za rushwa na ufisadi!.......hata TAKUKURU watakapotangaza kuwa wameanza uchunguzi (na watafanya hivyo sometime next week au mapema zaidi) watu wataanza kushangalia kuwa sasa TAKUKURU ifanye kazi yake!
MMM
Sasa naona umekubaliana na mimi indirectly na unaonyesha kukata tamaa, mimi nasema kila siku tatizo sio CCM tatizo ni UTAMADUNI wetu jinsi tunavyolelewa, Utamaduni huu hauwezi kutoa kiongozi mwenye sifa ulizozitaja, hatulelewi hivyo, badala ya kufundishwa uadilifu, moyo wa kujitolea kwa manufaa ya wengine n.k tangu utoto tunafundishwa uzinzi, uongo, ubinafsi, kutumiana kwa maslahi binafsi nk na wote tumekuwa ktk hayo mazingira awe Kikwete, awe Zito, awe Ngereja au Pinda sasa kutegemea matokeo tofauti na hayo ni kujidanganya!
Mtabadilisha Katiba mnavyotaka hata mkikopi na kupaste katiba ya Marekani au Japani hakuna kitachobadilika maadamu watendaji na watu wanaopaswa kutii na kueshimu hiyo Katiba wamelelewa na kukuzwa na huu Utamaduni wetu hakuna kitachobadilika!
Maneno mengiii, ili kutaka jamii ikuone umesema jambo la maana! Ukweli utabaki pale pale wewe subiri siku ukishika nchi uje na hizo SERA zako zinazo wezekana, lakini kwa sasa endelea tu kupiga domo watu wanapiga kazi.
wamba Mhando (Mkurugenzi wa Tanesco) amejipa mkataba yeye na mke wake na kukiuka waziwazi sheria ya maadili yaviongozi wa umma ya 1998 halina shaka.
Lakini cha kushangaza ni kuwa ati Waziri anaenda kumlipua Bungeni badala ya aliyemteua kumfukuza kazi, kumtia pingu na kuhakikisha anaingia gerezani yeye na wote waliowezesha dili hilo.
Tunaona Mwendesha Mashtaka Mkuu na Mwanasheria Mkuu hawafanyi lolote kuonesha nchi yetu inasheria je yawezekana na wenyewe wamepewa "mlungula" (vijana wanaweza kuwa wamelisahau hilo neno).
Bado haitasaidia.... I REPEAT, HAITASAIDIA!! Tatizo la nchi hii ni zaidi ya Wabunge waliopo; bali ni ubovu wa maadili tulionao Watanzania wengi!! Maadili ya Watanzania yamemomonyoka kwa kasi ya kutisha ingawaje nayo sifahamu ni wakati gani yalipata kuwa mazuri.....hapa napo, wala asitokee wa kuniambia kwamba tulikuwa na maadili bora hapo zamani....kama zamani, basi ni labda kabla ya ukoloni!!Hakuna namna ya kusafisha hili isipokuwa kuvunja hili Bunge kwani limechafuka na kulichafua taifa. Sijui watalivunja vipi lakini wananchi wasiwe na imani nalo na hawapaswi kuwa na imani nalo hasa kama watuhumiwa ndani yake bado wapo. Kwani si tuliambiwa kuwa kuna wabunge walikatiwa kitu wakati wa sakata la Jairo? Wako wapi? Wametiwa pingu lini? Nyet! Halafu kweli sisi na akili zetu tukiwa wanafunzi wa zuri wa historia ya karibuni tunaweza hata kutoa pongezi? POngezi kwa kitu gani? kutaja majina? kutuambia kinachojulikana?
Nsiande,tatizo ni kama nilivyosema,kuna a serious part of politics wananchi wengi hawaijui,na ndiyo maana unatakiwa uelewe kuwa hatua za kisiasa ni tofauti na zile hatuwa za kisheria.Viongozi na ccm na culture yetu,tumezoea kuwachukulia hatua za kisiasa hata wahujumu uchumi wetu.Na ndo maana kuna mchangiaji alisema hii sheria iliwekwa kwa makusudi na watu ambao waliliona hili tatizo,na sheria ikatungwa kulidhibiti,walioziondoa,nia yao ndo hii,lakini hatuna historia ya kuwahold accountable wahujumu uchumi,wanasiasa,yes,wengine na nchi washakimbia,mafisadi?jibu ni no,wanakumbatiwa.Nakataa MM,
Ndio tumeshaona drama za kila aina baada ya kuundwa tume za kuchunguza , lakini katika hili la Nishati na Madini wameingia watu wapya ambao si wanasiasa na wakaibua madudu ambayo yamefumbiwa macho
Kitendo cha kutaja wezi wa umeme bungeni ambao baadhi ni wabunge ni ujasiri mkubwa sana
Unaposema kiini macho sikuelewi kuwa nothing is coming out of this?
Kwa hili la MEM tayari hatua kadhaa zimechukuliwa
Kimsingi umetoa maoni yako na yana mantiki lakini I dare say sidhani yawe applicable mpaka kwa hili coz siligroup katika mazingaombwe...
Credit should be given where it deserves
Huku tukifurahia the show na kila miaka mitano, tukiwaajiri tena huku tukidunduliza na kuchangishana pesa za mishahara yao kwa miaka mitano mingine, na 2015 tutawaajiri tena ili tuendelee kufurahia the comedy show!.Hakika hiyo ndiyo hali halisi ya siasa za nchi hii. Utendaji wa serikali ni Komedi, bunge ni Komedi, na hata mahakama ni Komedi. Wananchi ndiyo tumekuwa hadhira yao.