Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

Ewe MM, post yenyewe umeipost sehemu ambayo watu ni washabiki wa matukio, maneno yako yataingilia sikio la kulia na kutokea sikio la kushoto.
Watu hapa wanapiga kelele nyiingi ila hawaelewi hii sinema hata kidogo, hawajui wao ndio waliwao. Anyways, ngoja wawapasie na watoto wao.
 
nilishawahi kusema hii ni nchi inayoongozwa kwa matukio,ikitokea tukio flani halafu likapambwa vilivyo na vyombo vyetu vya habari watanzania tunahamishia na kuweka rehani akili zetu zote huko ktk hilo tukio na kusahau tukio lililopita,kilichotokea sio cha ajabu ila kina symbolize nnachokieleza and that is how life goes on in Tanganyika.sijui baada ya tukio hili ni lipi litafuatia....tukae mkao wa kula tukisubiria tukio lijalo.
 
Naungana moja kwa moja na mtoa hoja hapo juu. Ni hoja yenye mshiko na yenye mausia ya kweli kwa mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii.

Hata mimi sidanganyiki na mazingaombwe haya ya kila kukicha. Watuhumiwa ndo hao hao wanaotutawala na hakuna wa kuwakamata kwani ndo wao dola na dola ni wao.

Kuna mama mmoja alinifurahisha wakati akichangia hoja ya wizara ya nishati na madini: Alianza kwa kusema ilii bajeti hii iungwe mkono inabidi ABCD ifanywe na wizara na akabainisha mapungufu yaliyomo, lakini alipokuwa akihitimisha mchango wake akadai anaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

Ni lini wabunge wataacha mazingaombwe ya kutumikia vyama vyao kwa kudai wanalinda maslahi ya chama huku wakiwakandamiza wananchi? Nadhani kwa sasa wabunge wanawakilisha vyama vyao na si wananchi waliowachagua. Ama wanataka niamini kuwa walifikishwa madarakani na nguvu ya chama chao na si kura? Chezea sisiem, ukipingana na waziri wako unapoteza ulaji uchaguzi ujao...... Wabunge wamekuwa watumwa wa wezi kwa kutetea matumbo yao na ya watoto wao.

Mimi si mmoja wao na nitabaki kama nilivyo mpaka Tanzania itakapokaa kwenye right track.
 
Watu hawa hawa walioshangilia la Jairo - mwaka mmoja uliopita - wanajikuta wanashangilia la Mhando mwaka mwingine... ikawa asubuhi ikawa jioni siku ikapita!
 
Ndio Maana Kuna Watu wawili huwa Nawakubiligi sana na Ninaamini watakuwa wa Mwisho kuni disappoint Tundu Lisu na Dr. Wilbroad Peter Slaa. Hawa Jamaa wameshachora a Clear Line Kati yao na CCM. Ili Upinzani uweze Kujenga Uhalali wa Kupewa Nchi ni Lazima Wachore Mstari Usio na Shaka kati yao na Watawala waliopo.
 
Watu hawa hawa walioshangilia la Jairo - mwaka mmoja uliopita - wanajikuta wanashangilia la Mhando mwaka mwingine... ikawa asubuhi ikawa jioni siku ikapita!

Bado kazi ipo...lakini kinachinipa moyo jana sio leo na wala haitakuwa kesho. Unajua hata meli kubwa inageuzwa kushoto au kulia kwa gear ndogo ndogo sana. Hivi ni kweli hizo gear hazijaazwa kuguswa guswa?
 
Asante Mzee Mwanakijiji kwa uchambuzi mzuri. Kilichoendelea ktk Bajeti ya Madini na Nishati ilikua mipasho na kuumbuana. Nilihuzunika zaidi pale waziri naye alipohamaki na kujikuta anajitumbukiza ktk mipasho.
 
hata aliyeturoga anashangaa uwezo wa dawa yake ya kutupumbaza,maana sie ni bendera fuata upepo uvumiako.mkuu mmm ukiangalia kwa undani nature yetu watz ni unafiki,na hata watawala wanalitambua hlo,wanafaham kuwa hatuna muda wa kufikiri i thnk to thnk is a hard task to be taken wit tanzanian,no tym to reason.mungu atusaidie tujitambue!
 
Baada ya Bunge Utamuona Prof. Muhongo akijiunga na Nape, Magufuli, Mwakyembe, Wasira Kuzunguka Nchini kuelezea "Mafanikio ya Kuwataja Wahujumu Tanesco Bungeni", Wataeleza Namna Wabunge wa CDM wakiongozwa na Zitto "Walivyokula Mlungula" Kutaka kusafisha Mafisadi yakiongozwa na Mhando.

Nothing new to expect the Failed CCM Government Bwaha ha ha haa

...and whats more interesting is the mere fact that - under CCM, we have experienced both scenarios of A FAILED STATE (Socialism 1967 - 1985) and A FAILED MARKET (Free Market 1986 - 2012), and still, hakuna anaeliangalia hili kwa umakini, sio CCM wala CHADEMA. I remain to wonder jinsi gani bado CCM inapata the legitimacy and the justification kuendelea kutawala na Chadema wanajifunza nini katika hili.
 
Hii movie ya leo imeenda fasta hadi ikaniacha sielewi elewi...nikastukia tu kamati inavunjwa,nikiwa bado najiuliza nini kinaendelea...nilikuwa nawatupia jicho makamanda ni kama walimwagiwa maji hawajui wafanyeje...inshort hadi sasa sielewi huu mchezo unaelekea wapi.
 
Mkuu MM nianze tu kwa kuzidi kukukatisha tamaa zaidi na ili bunge letu la ajabu, bunge letu mimi napenda kuliona kama kipindi cha Exhibition niseme sabasaba trade fair ambako watu wanaenda kuoneshana sanaa na kurudi nyumbani.

Ukisikiliza vizuri utagundua kuwa kuanzia spika na wabunge wake ufanya maigizo. Spika ufika hatua anawaonya wabunge eti waongee kwa upole hata kama wana uchungu kwa kuwa wanaonekana TBC/media. Hapa anawaonya wasihaibishane kwa kuwa wanaonekana!

Pili , Tanzania kwa ujumla si tlp,chadema ,si CUF , si sisiemu, wote wamekuwa 'wanamazingaombwe'. Pia na sisi watanganyika na wazanzibar tumekuwa wanamazingaombwe kwa kukubali mazingaombwe. Sheria mbovu zinatungwa na kufutwa kila mara kwa kuwa utawala uliopo umekosa umakini na sheria kuafikiwa kwa kukomoana kiitikadi,sijui utawala unaomsikiliza au shetani au mungu au Mungu,hapa sijui ni yupi asa wanamfuata.

Sikatai kuna watu kwa maneno yao wanaweza kuwa wakombozi ila wakiwa katikati ya wachafu wanakomboa nani? ni sawa na wanambizi wanaokoa wafamaji na kuwaweka katika melikebu iliyotoboka kitako! Tangu nisikie ufisadi miaka ya 80 mpaka leo ni nani hasa aliyewahi ku fisadi akaonja haki yake? Sheria zipo lakini zinashikwa masikio na wakubwa. Nitayakumbuka maneno ya mh Ezekiel Maige aliyewaonya mawaziri leo akisema, jihadharini mjue mnawanyima wakubwa ivo jiandae sawasawa, hapa anamaanisha kuwa uko juu kuna viwavi majambazi watawala!! Hivi waziri awanyime wakubwa,ni wakubwa wapi hao?ni nani zaidi ya waziri?sijui kama tunapata jawabu apa!

Tuseme tu kama Kafulila alivyosema, hii nchi imebakwa!apa si tusi ina maana imedakwa/imenaswa na wacache. Mwaka 2008 nilipata video aliyokuwa anatoa press mh rais akiwa amekaa katikati mwa bendera mbili, moja ya marekani na nyingine ya Tanzania akionesha the second luxury city in Africa, to be future kigamboni, nikaona madaraja likiwemo daraja la Kigamboni, nikaona military base mbili, moja ya US military base kule kigamboni, nikaona magorofa marefu, nikaona parking na ramani za zoo kigamboni mpya phase II year 2020-2025, nkacheka sana nikajisemea hii kitu imetungwa kumchamfua rais na kuwekewa maneno bandia, ila baadaye nkasikia daraja la Kigamboni, ooh tena wananchi waame kupisha mradi wa kigamboni, dah nkajua kweli nchi ilishamegwa kitambo sasa bunge na watanzania tunapiga tu muhuri/rubber stamp mkataba wa chiefu Mangungo wa Msovero eti maendeleo? Maendeleo yepi wakati kigoma,kagera, musoma hakuna barara, hospitali wala chochote? Rukwa watu wanagombania ardhi kujenga na sehemu ya kulima?watanzania wanakufa maji eti meli mbovu? Na waokoaji wanaacha kazi ya kuokoa eti usiku umeingia,bahari itachafuka ivo tutaendelea na uokoaji kesho!iyo ndo Tanzania jamani.

Nchi inandeshwa kama taasisi isiyokuwa na mkurugenzi, benki kuu inaporwa dr Slaa anafichua wanasema eti ni mzushi na mzabina zabina kama alivowahi kusema salva wa magogoni, Ni nini hii jamani? Wote waliotufikisha apa bado ni wabunge, na wale waliokosa ubunge kwenye sanduku la kura wanateuliwa kwa lazima kuwa wabunge na wengine kuwa mabalozi ktk africa na mashariki ya mbali..iyo ndo Tanzania!

Wale wote wanaopingana na uhuni wanaundiwa kesi feki. Juzi tu dr ulimboka amepishana na barabara wahitakayo,wakaamua kumzuru atoweke kama akina prof chachage, bado tumo tumo tu nasikiliza wanavorushiana pira!eti mkenya,wakati majeruhi anawataja wazi wazi wale mashetani waliotaka atoweke duniani...ni nani ataikomboa Tanzania? Kova? Gwajima au nani? Je taifa lina kiongozi kweli?mtu anakimbilia kuita vyombo vya habari eti mimi sihusiki wala sijamtuma mtu?!!apa unajianika tu....

Sisi tumewaachia wanasiasa na wanaharakati tu ndo waseme? wakulima wako wapi, wanasheria wako wapi? Walimu wako wapi? wanahabari wako wapi?wagavi wako wapi? Wachumi wako wapi?wafanyabiashara wako wapi? Wanazuoni na wanafunzi?watafiti?kweli wote tunakuwa kimya kwa sababu ya kilicho mfukoni? Na CHADEMA wanapiga kelele kwa kile kilicho katika mfuko mwingine? Au tusubiri majibu ya waziri bunge lijalo mwakani? Na akiulizwa sali jipya spika anasema ilo swali halikuwepo ni jipya ivo mh waziri usijibu! Wanatumiwa maswali wakatafute majibu, lakini std vii tunawaambia hakuna kuingia na majibu chumba cha mtihani.

Mtu akisimama anaambiwa kaa chini, huwezi kumuombea spika mwongozo wala kumpa taarifa! Je, kama kuna jambo muhimu kama lile la kuptisha sheria ya kikoloni ya kuwanyima pesa zao za pensionable schemes na wakati huo ukamnyima nafasi ya kuongea hatimaye bomu likawekwa katikati ya wafanyakazi na serikali? Nani alaumiwe? Kwa sasa kila kitu ni siasa tu,ziko wapi aspects nyingine?

Serikali haina wahasibu lakini National Audit wanaajiri watu 100 baada ya miaka miwili utadhani tuko mwaka 74, walimu wanaajiriwi wananyimwa haki yao alafu watawala wanasema marufuku kugoma, je mwali ataenda kufundisha 4 mara 4 sawa na 16 au makusudi atasema 4 mara 4 ni 19 au ata 21? Je, Dr kupigwa au kulazimishwa kurudi muhimbili ndo atatibu kwa lazima au malaria ataipa dawa ya minyoo, operation ya bandama atafanya ya utumbo?

Halafu tunadai tuna taifa apo!Tunao mafisadi wa kidini, mafisadi wa elimu ref mmsemakweli list, tunao mafisadi wa kalamu, na tunao mafisadi papa ref LIST OF SHAME,sasa hawa watu wakashtakiwe CHINA ua TUWAJENGEE MINARA au bora turudishe mkoloni? BADO TAIFA HALIJAWA TAIFA!!!!

SINEMA ILE ILE ILE, MWIGIZAJI MKUU YULE YULE ILA WASHIRIKI WAPYA ....KARIBU TANZANAIA, A LAND OF RICHNESS WITH EMPTY LAWS!
 
hongera sana mwanakijiji kwa analysis yako.....ila ni nani wa kulaumiwa na nini kifanyike....
 
Mwanakijiji,

Umesahau kwamba sasa hivi tuna taifa la kufuata mkumbo?Taifa la wanaokunwa na mambo madogo hadi kuchanganyikiwa?Taifa la kubweteka na kuridhika mapema? ukitaka kumjua mtanzania halisi wa siku hizi(kwa maana ya kuharibiwa kifikra katika malezi ya kijamii) mpe au mwonyeshe mlango wa mafanikio kidogo uone jinsi atakavyotukana wengine na majigambo kibao.

Siku hizi tunashabikia kila kitu bila kujiuliza mara mbili mbili ili mradi tu tuone umati umejaa kuzunguka eneo au kumzunguka mtu.Nimeeleweka......!
 
Kila Mtanzania wa kawaida,
anajua fika kwamba kuna uonevu,
na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu,
ubadhirifu wa mali ya umma,
ufisadi na madudu mengi makubwa.
Kubwa zaidi likiwa ni lile,
Rais wa nchi mawaziri na watendaji wa serikali ya CCM,
Kurubuniwa kwa shanga za viunoni,
na kutumia nguvu zao zote,
kuusimika upya ukoloni na ukoloni mambo leo,
uletwao na mashirika ya kimataifa,
yanayomilikiwa na nchi zile zile,
zilizo tutia katika ukoloni mika 51 iliyopita.

Nimekuwa nikifiki na kuwaza sana,
kwa nini huyu mtanzania average,
halalamiki? au akilalamika,
kwa nini sauti yake haisikiki kamwe?
kwa nini mtanzania average hachukui hatua madhubuti?
Pale mtanzania average akichukua hatua,
mtanzania average mwingine humpinga huku akitoa povu,
kujiapiza na kukenua mimeno kwa hasira za nyati?

Nimegundua kwamba,
Watanzania hatuna mahali pa kusemea,
Tuna vyama vya kisiasa,
lakini hatuna mahali petu wenyewe pa kusemea,
Tuna dini lakini hatuna mahali petu wenyewe pa kusemea,
hatuna mahali tulipo jiundia ili kiwe chombo,
chetu imara cha kusemea matatizo yetu.

Kuna umoja wa nguvu sana wa kitabaka,
wakati wa misiba lakini watu hao hao ,
wenye umoja misibani hawana umoja pale,
mmoja wao akiugua au uchumi wake ukizorota,
umoja wao ni pale mmoja wao akifa tu.

Kuna umoja wa nguvu sana wa kitabaka,
wa kuandaa maharusi ya mamilioni,
lakini kundi hili la watu halina umoja,
wa kusaidia kujenga chumi za familia,
au harambee ya kusomesha mtoto chuo kikuu,
lete pochi watu tule kama una matatizo kiuchumi,
hilo si tatizo letu.

Watanzania wanyonge hatuna chombo,
chetu wenyewe tulichokiunda kwa hiari yetu wenyewe,
chenye umbile la kamati za harusi, misiba, kipaimara,
kitchen party na utumbo mwingine,
mahali ambapo mtu atakwenda kila siku,
au walau mara moja kwa wiki,
kutoa dukuduku lake la kisiasa kiuchumi na kiutamaduni,
kwa kusudio la kuweka maoni yake hadharani,
na yeye kushauriwa au kujifunza,
na kuchukua hatua za kugeuza maneno kuwa vitendo,
juu ya jambo fulani la kijamii.

Watanzania ni lazima tuunde umoja wa kudumu,
wa kushughulikia mambo yetu ya kila siku,
umoja wa watu kwa hiari yao wenyewe,
siongelei vyama au makundi ya kisiasa,
naongelea umoja aina ya Harambee,
Msalagambwe wa mawazo,
Mugove wa mawazo.

kule Upareni ukiitishwa Msalagambwe,
unatoka na jembe lako, mundu wako,
shoka lako na kiriba cha maji huyo,
unakwenda kuitikia wito ukiwa tayari kabisa,
kutoa mchango wako bia kinyongo.

Msalagambwe hauna kadi ya uanachama,
Msalagambwe ahauna kadi ya mwaliko,
ni ile hali ya mtu kujali hali za watu wengine,
kama ajalivyo hali yake ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

Mtanzania average hajaweza kuwa na mahali pa kusemea,
ukienda Bar ukaanza kuongelea siasa watu watakukimbia,
kesho hawkai na wewe,
kisa unawaharabia starehe kwa maongezi ya kipuuzi.
Mjinga kweli Msalagambwe"
"Hajui hapa Bar watu tumekuja kuburudika?
Mambo yake ya siasa apeleka huko vijiweni kwao."
Fika Ba au Pub;
Ongelea makalio ya dada na shangazi zetu!
Weee!
Ongelea shoo ya kanga Moko,
Acha bwana!
Ongelea kupiga chabo,
Patamu hapo yakhe!
Ongelea upuuzi wowote ule, watu watakuona burudani maridhawa.

Huu ndo ujinga wetu Watanzania average.

Kuna vijiwe vya kuogelea mpira na,
kujadili wachezaji wa Mnchester,
Kuna vijiwe vya kujadili dini na udini,
kuna vijiwe vya kupanga dili za wizi,
umalaya na uharamia wa kila aina.

lakini hakuna vijiwe vya kujadili,
hali halisi ya mtanzania na matatizo yote,
hasa yanayomkabili kila kukicha na,
hana namna ya kuyatatua,
hakuna vijiwe vya kupanga mikakati,
ya kupinga maamuzi ya kihuni ya serikali ya CCM.

sijui tunasubiri United Nations,
waje kupambana katika kujinasua makuchani,
mwa serikali musflisi ya CCM?

sijui tunasubiri neema inyeshe,
toka mbinguni na kuwadhoofisha,
watendaji wa serikali ya CCM na,
kutupa nguvu ya kiiujiza sisi wanyonge,
uwezo na ujasiri wa kupambana?
Tutasubiri hadi siku ya kufa na hata vilembwe,
wetu wasipochukua hatua,
nao watasubiri hadi mauti iwapoke uhai wao.

Ukosefu wa mahali pa awali kabisa,
pa kuongelea dukuduku zetu mtaani,
ndiyo asili ya kushindwa kuchukua hatua,
thabiti za kukabiliana na ujinga mkubwa,
wa serikali ya CCM,
Ujinga unao tumaliza wazima wazima,
huku tukiwa macho na fahamu zetu zote,
na akili zetu zote na uelewa wetu wote.
Utawala wa serikali ya CCM katika uovu wao,
wana umoja msimamo na agenda za wazi,
wana mikakati safi ya kutekeleza uovu wao,
wamejipanga, wamejizatiti, wanatumia fedha kama nyundo.
wanajua udhaifu wetu, wanautumia kwa faida yao.
wanajua hatuna pa kuongelea, wanazidi kututenganisha kwa hila.
wanajua tunapenda majungu,
wanazidi kuinjika na kupika majungu kutuchellewesha.

Sisi watendwa tunaoonewa katika nchi yetu wenyewe,
hatuna umoja,
hatuna msimamo,
hatujui tunataka nini,
hatuongelei matatizo yetu,
kila mmoja wetu anajitazama yeye tu.


Tuunde vijiwe vidogo vidogo,
watu wawili mpaka saba tosha,
mtu mmoja ni budi awe member wa vijiwe viwili au vitatu,
Si lazima kukutana uso kwa uso,
tuna teknolojia ya internet na simu za mikononi,
tuna video camera.
Tuitumie teknolojia hizi za kisasa katika,
mijadala yetu ya mambo yetu ya kila siku,

Teknolojia mpya za Magazeti na printing Press,
Zilisaidia kuuondoa utawala wa mwingereza,
Marekani miaka 1776.

Teknolojia mpya ya mashine za kurudufia,
ziliuondoa utawala Tzar wa Urusi 1919.

Teknolojia ya Blue Tooth,
ndiyo imefanikisha kuuvunja utawala wa Midikteta ya kijeshi huko Egypt,Libya na Tunisia
hasa pale tawala hizo zilipo funga mitandao ya simu Cell Tower.

Wazo imara ndani ya mtandao wa Internet,
ni kama ujiti mmoja wa kiberiti,
Ujiti mmoja wa kiberiti,
una potential power ya kuwasha moto,
kuunguza himaya nzima.
Wazo imara mtandani ni sawa,
na mbegu moja ya mtama,
iotayo katika umoja wake,
na kuzaa punje elfu za mtanda,
katika msimu mmoja tu.
Watawala wa serikali ya CCM wanalijua hilo fika,
lakini inaelekea kwamba sisi wananchi wanyonge,
hatuna habari au hatuioni nguvu ya wazo imara,
ndani ya mtandao wa Internet.

Ni lazima tuunde umoja wa hiari,
uwe chombo chetu cha kujadili,
na kutafsiri kwa vitendo mawazo yetu,
na nia yetu ya kuiondoa serikali ya CCM madarakani,
pia kupeana mbinu ziendazo na wakati,
za kujijenga kiuchumi kisiasa na kiutamaduni.
 
Hivi kulikuwa na ulazima wa ku quote post yote hii? Sio kila mtu humu anatumia PC..

Nakuunga mkono mkuu wa2 wanakoti thread nzima halafu anaandika mstar 1! inaboa sana. 2kot km 2 kuna sabb za msingi.
 
Nashindwa nisemeje mkuu, inauma sana tena sana, mazigaombwe anyway mkuu MMM, Rais analalamika, PM analalamika, mbunge Analalamika, waziri na watu wote wa maamuzi wanalalamika, wananchi wenye nchi wanalalamika, mkuu ndio nchi ya kwanza kuona dunian... mazingaombwe hayataisha kamwe... Udhaifu kila kona, kwa nini hawachukui hatua??

Chukua li like hilo mkubwa kwa mistari yako Michache, baatimbaya natumia mobile.
 
Back
Top Bottom