Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 28, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Katika umaskini wetu tumejifunza kufurahia! MM​

  Kumekuwa na tabia ya "kuumbuana" huko ndani ya chama tawala. Hili halikuanza leo Jumamosi. KUanzia wakati wa Mrema, Mzindikaya na wengine hakuna shaka hata kidogo kuwa wapo watendaji wa serikali ya CCM ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao kujinufaisha. Richmond ilifunua hili, kashfa ya sukari ilifunua hili kama vile kashfa ya EPA ilivyolifunua. Hakuna geni!

  Kwamba leo kwenye wizara ile ile ambayo kila mwaka imekuwa ikikumbwa na kashfa inaibuliwa kashfa nyingine si jambo la kushangaza, na kwa hakika siyo jambo la kusema "siamini hili linawezekana". Mtu anayesema hivyo alikuwa wapi miaka mitano iliyopita? Ati leo Prof. Muhanga kusema kitu ambacho Mnyika naye alikisema jana imekuwa ni "hongera, kudos, jasiri!" wakati hapa hapa tulikuwa mwaka 2008 wakati watu walitajwa na Waziri Mkuu akajiuzulu! Wangekuwa wanajifunza yasingerudia tena!

  Ili kukamilisha onesho lao la mazingaombwe wanavunja kamati ya nishati na madini; ili kiwe nini? Wote waliokuwemo kwenye hiyo kamati bado wapo Bungeni. Hakuna mtu tuliyeona ametiwa pingu na kuondolewa Bungeni; hata TAKUKURU watakapotangaza kuwa wameanza uchunguzi (na watafanya hivyo sometime next week au mapema zaidi) watu wataanza kushangalia kuwa sasa TAKUKURU ifanye kazi yake!

  Kwamba Mhando (Mkurugenzi wa Tanesco) amejipa mkataba yeye na mke wake na kukiuka waziwazi sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya 1998 halina shaka. Lakini cha kushangaza ni kuwa ati Waziri anaenda kumlipua Bungeni badala ya aliyemteua kumfukuza kazi, kumtia pingu na kuhakikisha anaingia gerezani yeye na wote waliowezesha dili hilo.

  Siyo hivyo tu, kwamba Bungeni wabunge wanajuana nani anakula rushwa na wanazungumza wakisukumizwa siyo na uzalendo bali na vilivyomo "mfukoni" na Bunge lenyewe linashangilia kuwa "waambie hao!" halafu bado watu wanakaa kujadili bajeti hiyo hiyo. Tunajuaje hao wanaopiga kelele za "sema sema" na "waambie waambie" na wenyewe hawafanyi hivyo kwa nguvu ya mifuko mingine?! Tumeona Spika anavyoendesha Bunge tunajuaje kama naye haendeshi kwa sababu kuna mifuko kadhaa huko nyuma? Tunaona Mwendesha Mashtaka Mkuu na Mwanasheria Mkuu hawafanyi lolote kuonesha nchi yetu inasheria je yawezekana na wenyewe wamepewa "mlungula" (vijana wanaweza kuwa wamelisahau hilo neno).

  Tunaona Rais akiteua watu ambao wana mashaka na anawavumilia na kuchafua kabisa utumishi wa umma; na ukimya wake unapiga kelele? Je yawezekana na yeye yuko na huu mtindo wa kukaa pembeni kwa sababu naye anautumikia mfuko mwingine? Nani ni msafi basi kama waliozungumza na kudhaniwa wasafi kumbe na wao wamechafuka na wale ambao wanapiga kelele zaidi ya uchafu kumbe wenyewe pia ndio wachafuaji? Nani anaweza kuaminiwa? Rais haaminiwi, Waziri Mkuu haaminiwi, sasa Bunge nalo linaonekana haliwezi kuaminika. Tutaamini vipi tukiona mtu anazungumza kwa uchungu kumbe ni uchungu wa kuogopa kupoteza 'wema na fadhili'?

  Hakuna namna ya kusafisha hili isipokuwa kuvunja hili Bunge kwani limechafuka na kulichafua taifa. Sijui watalivunja vipi lakini wananchi wasiwe na imani nalo na hawapaswi kuwa na imani nalo hasa kama watuhumiwa ndani yake bado wapo. Kwani si tuliambiwa kuwa kuna wabunge walikatiwa kitu wakati wa sakata la Jairo? Wako wapi? Wametiwa pingu lini? Nyet! Halafu kweli sisi na akili zetu tukiwa wanafunzi wa zuri wa historia ya karibuni tunaweza hata kutoa pongezi? POngezi kwa kitu gani? kutaja majina? kutuambia kinachojulikana?

  Nani hajui watumishi wanavyojipa miradi wao wenyewe kwa wenyewe au kupitia jamaa zao? kwani ripoti ya CAG ya karibuni haikuonesha hili kwenye halmashauri mbalimbali ambapo madiwani kadhaa wamejigawia tenda? Kwani ni mara ya kwanza kuona mtu anauzia serikali kitu kwa bei tofauti (marked up) huku akijua kabisa kuwa bei halisi ni ya chini? Kwani ni mara ya kwanza kuona mtu anapodai mafao yake ili yafanyiwe uzuri uzuri anaweza kuongeza kidogo ili aweze kumkatia chochote mtumishi wa utumishi ili mambo yaende vizuri?

  Watanzania tunapenda sana drama! Tunakuwa kama tunasikiliza "Penzi Kitovu cha Uzembe" au "Aliyejuu". Tunasubiri wiki baada ya wiki kuangala kuna nini kipya. Wapo kweli kabisa ambao wamekaa kwenye viti vyao wanacheka kweli na kusifia kuwa "bunge letu kali sana" au "waziri huyo bomba sana". Really? Kwa lipi? Ni kipi ambacho kimesemwa leo ambacho hakijawahi kusemwa huko nyuma? Ni madai yapi ambayo yametolewa leo ambayo yanashangaza kweli kuwa yanawezekana? Kwa vile katajwa mchungaji? Mbona wengine tulishamtaja huyu na kuandika hapa achunguzwe leo watu wanashtuka?

  Tutafungukaje kama tunashangilia mazingaombwe na kupongeza viini macho? Tumeharibiwa na kitu gani kiasi kwamba tunaridhishwa na vitu vidogo kama watoto wanapopewa chuchu za plastiki kunyonya ili waache kulia! Tunapewa hizi pacifiers za maneno na tunajisahau na kuanza kuimba "Kidumu, kidumu"? Mbona hakuna jipya? Mbona ni yale yale. Shilingi ukigeuza upande wa pili haibadiliki thamani! Kinyonga akijigeuza rangi bado hubaki kinyonga! Wizara ya nishati na madini imekuwa ni kitovu cha kashfa nyingi tu lakini leo ndio watu wanataka tushtuke kuwa kuna ufisadi? Really?

  Ukiwaambia hili watakimbilia "tatizo siyo sera ni watu"! Na wapo wanaoamini hivyo kabisa. Kwamba wakibadilisha watu sera zitatekelezeka! Miaka 50 wamebadilisha watu wangapi!?

  Mojawapo ya falsafa za uongo (deceptive philosophy) zinazonezwa sana ili kuzuia watawala kuwajibishwa ni hii ya "kuona mazuri vile vile". Kwamba, wananchi wanatakiwa waone mazuri ya kuyasifia ili watawala wajisikie vizuri. Ni falsafa ya uongo kwa sababu serikali kufanya mazuri siyo hisani na wala siyo 'optional'! Ni wajibu wa serikali kufanya mazuri na haiitaji kusifiwa kufanya mazuri.

  Kwamba, serikali ikijenga barabara kwa kodi za wananchi isifiwe? Kwamba ikijenga hospitali - hata kama hazina madaktari, nyenzo au madawa ya kutosha- bado isifiwe kwa sababu ni jambo "zuri"? Kwanini umsifie Waziri kwa kufichua ufisadi? alkuwa na option ya kutofichua!? Polisi akikamata mwizi asifiwe kwa kukamata mwizi? alikuwa na option ya kutomkamata?

  Watawala wanaotumia kodi ya wananchi kuleta maendeleo na watu hao waliomba kibali kuwaongoza wananchi hawana sababu ya kusubiri wananchi kuwasifia "kwa mazuri" wanayoyafanya? Jukumu la wananchi kuangalia mabaya yanayofanywa na kuimbia serikali kwamba haya ni mabaya! Kwa sababu siyo jukumu wala sababu ya serikali kufanya madudu!

  Ndio maana nimesema hapo juu wale wanaoona kuona "upande wa pili" unaostahili sifa wafanye hivyo! Inapokuja serikali haisifiwi kwa kufanya mazuri, kwa kusimamia sheria au kwa kutumiza wajibu alioapa kuutumiza. Sasa Prof. Muhongo anasifiwa kwanini hasa? Ndio maana utaona miye SISIFII KABISA nikisikia mbunge kasema vizuri Bungeni au sijui katetea jambo gani bungeni! Ni WAJIBU WAKE! Kama anataka kusifiwa akichambua hoja au akipinga hoja atoke aje huku nje tumsifie! Aliomba kura kwenda Bungeni kuwatumikia wananchi; yeye anahitaji kutusifia sisi wananchi kwa kumtuma kufanya kazi. Yaani tumuajiri, tumlipe, tumpe marupurupu lukuki halatu tukae pembeni tuanze kumsifia kwa kuzungumza?

  Tuna matatizo gani sisi?

  Watu pekee wanaostahili sifa ni wale wanaofanya vitu kwa kujitolea na kujituma wenyewe si kwa sababu wanalipwa au wameajiriwa. WAkitaka kupongezwa vyama vyao viwaandalie sherehe ya kuzungumza vizuri Bungeni na za kufichua ufisadi. Kwa sisi wananchi hatutaki kuona ufisadi it is simple as that. Kama hawawezi kufanya kazi au kutimiza wajibu wao bila kusifiwa waache!!!

  Kwani nani kasema Tanzania kuna tatizo la umeme?

  Hadi watu watakapojua kuwa tatizo la Tanzania ni CCM na sera zake zilizoshindwa wataendelea kutumainia mabadiliko chini ya CCM kama vile watu wanaokinga mikono yao jangwani wakiombea mvua inye! Kinachoniudhi mimi zaidi na kwa kweli naanza kufikia ukomo wa kuvumilia ni hizi hotuba za wapinzani ambazo nazo zimejaa maneno ya kutarajia serikali ibadilike kiasi kwamba wanasahau kilichotufikisha hapa ni sera zilizoshindwa za CCM. Siyo udhaifu tu wa Kikwete, siyo tu ulegelege wa Bunge na uzembe wa CCM - ni sera mbovu ambazo zimekuwa na matokeo mabovu kwenye kila sekta - angalia afya, angalia Elimu, angalia Elimu ya Juu, angalia Nishati na Madini, angalia usalama. Ni ubovu ubovu ubovu tu. Halafu leo tunaambiwa juu ya ubovu zaidi tunaanza kushangilia!

  Kama kujua ubovu ni fahari basi tutengeneze mnara wa kumbukumbu za kashfa mbalimbali za ufisadi. Tuchonge sanamu za wahusika wa ufisadi huo na majina yao tuyachirize kwenye mnada huo. Kila mwaka tutenge siku ya kuwakumbuka mafisadi wetu na tuweke shada la maua. Iweje tushangilia kujua ubovu na kuambiwa ubovu ambao tayari tunaujua. Kwanini tusishangilie tukisikia Waziri afungwa miaka 400 jela; au Mbunge ahukumiwa miaka 30 jela kwa ufujaji? Kila mtu anajua hili haliwezi kutokea. Tutapewa "kesi mahakamani" tutafanyiwa mazingaombwe isipokuwa kupewa kitu halisi!

  Nasubiri kitu halisi nami nitashangilia, haya mazingaombwe yenu chezeni nyinyi na watoto wenu na mje kuwarithisha wajukuu wenu na vitukuu vyenu pamoja na vilembwe vya vilembwe vyenu! Watawasifia kwa jinsi mlivyofurahisha macho yetu!

  MMM
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Nimekusoma vizuri Mwanakijiji. Kweli mambo makubwa yanataka muda ili kuweza kujipambanua vizuri.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kufuatilia siasa za nchi ni 'hatari kwa afya yako'
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Haaahaaa! Ntahamia Ntwara nikajiunge na mabepari wanaotafuta gesi na mafuta. Labda ntaanza kuwa na fikra ya vitu vingine tofauti
   
 5. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  mhhh maneno mazito sana mkuu MMM
   
 6. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa la Watanzania wengi MMM, ni wasahaulifu na hawana maamuzi!!
   
 7. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Mkuu M.M, umeongea ukweli. Hapo ndiyo kesi imeshaisha, hukumu yake ni kutaja jina tu.
   
 8. Maliasili

  Maliasili Member

  #8
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Imetosha MMM, Don't spark anymore!
   
 9. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nashindwa nisemeje mkuu, inauma sana tena sana, mazigaombwe anyway mkuu MMM, Rais analalamika, PM analalamika, mbunge Analalamika, waziri na watu wote wa maamuzi wanalalamika, wananchi wenye nchi wanalalamika, mkuu ndio nchi ya kwanza kuona dunian... mazingaombwe hayataisha kamwe... Udhaifu kila kona, kwa nini hawachukui hatua??
   
 10. I

  IDIOS Member

  #10
  Jul 28, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nmeipenda ni analysis nzr sana hongera mtoa mada.
   
 11. M

  Msemakweli Daima Member

  #11
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Silly People in Silly Season
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  @mzee mwanakijiji,

  watanzania ni watu wa matukio, watashangilia jambo, kesho kikiibuliwa kipya wanaacha la zamani na watashangilia kilichotokea.....

  na wanasiasa wa tanzania wanajua hilo, wapi epa? richmond? wapi sanaa za miradi ya viwanja? wapi mikataba mibovu ya madini? wabunge wanajua hilo, wanajua kua baada ya kupiga makofi, bunge litaisha, bajeti itapita watarudi msimu mpya kupiga makofi, kuzomea na mipasho....

  hakuna uwajibikaji, in short hakuna wa kumwajibisha mwenzie...
  wote waliopo kwenye system, lengo lao ni moja, kuchuma kadri itakavyowezekana muda wako ukiisha unamwachia mrija atakayekufuata, afterall nani amwajibishe mwenzie? wote ni wachafu hakuna wa kunyoosha kidole....
  na ukiona wananyoosheana vidole ujue wamezidiana kete kwenye ulaji......................

  na kutokana na uozo huu sekta zote zimejaa rushwa, zimejaa kujikwapulia, kijitengenezea mianya ya kuchota, kuanzia ngazi za juu mpaka chini, kila mtu anavuta kutokana na uwezo wake....

  its a shame....


  waache na mazingaombwe yao..........
   
 13. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Sasa naona umekubaliana na mimi indirectly na unaonyesha kukata tamaa, mimi nasema kila siku tatizo sio CCM tatizo ni UTAMADUNI wetu jinsi tunavyolelewa, Utamaduni huu hauwezi kutoa kiongozi mwenye sifa ulizozitaja, hatulelewi hivyo, badala ya kufundishwa uadilifu, moyo wa kujitolea kwa manufaa ya wengine n.k tangu utoto tunafundishwa uzinzi, uongo, ubinafsi, kutumiana kwa maslahi binafsi nk na wote tumekuwa ktk hayo mazingira awe Kikwete, awe Zito, awe Ngereja au Pinda sasa kutegemea matokeo tofauti na hayo ni kujidanganya!

  Mtabadilisha Katiba mnavyotaka hata mkikopi na kupaste katiba ya Marekani au Japani hakuna kitachobadilika maadamu watendaji na watu wanaopaswa kutii na kueshimu hiyo Katiba wamelelewa na kukuzwa na huu Utamaduni wetu hakuna kitachobadilika!

   
 14. damper

  damper JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Maneno mengiii, ili kutaka jamii ikuone umesema jambo la maana! Ukweli utabaki pale pale wewe subiri siku ukishika nchi uje na hizo SERA zako zinazo wezekana, lakini kwa sasa endelea tu kupiga domo watu wanapiga kazi.
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Baada ya Bunge Utamuona Prof. Muhongo akijiunga na Nape, Magufuli, Mwakyembe, Wasira Kuzunguka Nchini kuelezea "Mafanikio ya Kuwataja Wahujumu Tanesco Bungeni", Wataeleza Namna Wabunge wa CDM wakiongozwa na Zitto "Walivyokula Mlungula" Kutaka kusafisha Mafisadi yakiongozwa na Mhando.

  Nothing new to expect the Failed CCM Government Bwaha ha ha haa
   
 16. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Always u think metaphysícs,mi nilitaka kumpa 5 prof mhongo ngoja nijipange kwanza kùmbe
   
 17. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  nani wa kulaumiwa?
   
 18. r

  raymg JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duh.............
   
 19. N

  Ndogue Ndogue Member

  #19
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwa nakufeel sana Mwanakijiji.

  Ingawa kuna mambo Nyerere alifeli, lakini alikuwa na msimamo, alichukia rushwa na hakupenda utajiri na sifa. Eti MHESHIMIWA! PTUUUUU!

  Hebu rejea hotuba yake anayosema serikali yake ilivyowabana mtoa na mpokea rushwa. Wote walikuwa 'MAGANYENGE'. Wote walipata msukosuko. Jela ilikuwa miaka mi2 na viboko 12 anaingia na 12 anapotoka akamwonyeshe MKEWE!

  Mwanakijiji, ni Watanzania wachache ambao huliangalia jambo kwa undani na mapana yake, wengine ni wepesi kudanganyika na kulichukulia juu juu.

  WENGI TUSINGEKUWA TUNACHOTEKA MAPEMA, TUNGEKUWA TUMESHAIKOMBOA NCHI HII. Mawazo uliyonayo, pia yananizonga kichwani.
   
 20. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, hatuko mbali kuufikia mpango wa mungu, kwa kupitia igizo hili jipya tuliloliona bungeni inamaana filamu haitauza tena, na kitakachotufumbua akili ni mgao mkali ujao!!! Lakini Bob Marley alitupa mistari ya maana tu, hebu tuipie.

  "TIME WILL TELL" BOB MARLEY

  Mm-mm-mm-mm-mm-hm! Ooh-oo-oo-oo-er. Mm-mm-mm.
  Jah would never give the power to a baldhead
  Run come crucify the Dread.

  Time alone - oh, time will tell:
  Think you're in heaven, but ya living in hell;
  Think you're in heaven, but ya living in hell;
  Think you're in heaven, but ya living in hell.
  Time alone - oh, time will tell:
  Ya think you're in heaven, but ya living in hell.

  Back them up; oh, not the brothers,
  But the ones who sets 'em up.

  Time alone - oh, time will tell:
  Think you're in heaven, but ya living in hell;
  Think you're in heaven, but ya living in hell;
  Think you're in heaven, but ya living in hell.
  Time alone - oh, time will tell:
  Ya think you're in heaven, but ya living in hell.

  Mm-mm. Mm-mm.
  Oh, ma ...................
  Oh, ma ...................
  Oh, ma children are cryin'.
  Oh, children, weep no more!
  Oh, ma sycamore tree, saw the freedom tree.
  All you ... have spoke:
  Oh, children, weep no more;
  Weep no more: children, weep no more!

  Jah would never give the power to a baldhead
  Run come crucify the Dread.

  Time alone - oh, time will tell:
  Think you're in heaven, but ya living in hell;
  Think you're in heaven, but ya living in hell;
  Think you're in heaven, but ya living in hell.
  Time alone - oh, time will tell:
  Think you're in heaven, but ya living in hell.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...