Ciril
JF-Expert Member
- Jan 10, 2011
- 8,558
- 7,156
Umasikini/ujinga/ushabiki/na mengine mengi ya kufanana na hayo ndio mtaji wa wanasiasa uchwara,wezi,wenye uchu wa fisi huutumia mtaji huu kuchota mabilioni ya walipa kodi kila iitwapo leo.Kila wakati ktk vyombo vya habari taarifa za wizi ni nyingi kuliko na taarifa nzuri.Sheria kali,zitakazotekelezwa vema na kwa wakati kwa mtu yeyote atakaezivunja ndio itakuwa suluhisho.Kiongozi amepatikana na rushwa,anapigwa risasi mbele ya hadhara na kufilia mbali nnadhani hii itakuwa ni salamu kwa watakaokalia kiti.Huku kubembelezana huku (uundwaji wa tume)tutachelewa sana kufika kule tunataka kwenda.Mataifa ya wenzetu yanaendelea kwa sababu wanazisimamia sheria ipasavyo bila kumuonea mtu yeyote haya.Tanzania inayotembea ndani ya chama kandamizi(ccm)kinachotaka kubaki madarakani milele pamoja na wananchi hawa hawa wasiojua haki zao,haitajisogeza popote kwa aina hii ya mfumo m'bovu wa uongozi.Ukweli nchi hii inatia kinyaa.