Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

Nakataa MM,

Kimsingi umetoa maoni yako na yana mantiki lakini I dare say sidhani yawe applicable mpaka kwa hili coz siligroup katika mazingaombwe...

Credit should be given where it deserves

Mkuu Nsiande, humu jf, tuna tatizo na wengine wetu wana uoni wa uni-direction, vision yao ni kuona only the bad side of things and nothing good, hivyo kukosa moyo wa fadhila, shukrani au appreciation!. Hata lifanyike jema lipi, wao hawalioni ni lawama tuu, na manunguniko! no appreciation!, na kiukweli huku ni kutoukubali ukweli!. Kama kitu fulani ni kweli, its a fact, kutoukubali ukweli ni kujifariji tuu nafsi lakini ukweli unabaki ni ukweli!.

Ila pia lazima tuendelee kukubali kutofautiana in good faith, ili kujiridhisha tuna tofautiana sana nguvu za uoni na uelewa baina yetu, wakati sisi wengine tukilaumu panapostahili lawama, na appreciation pale kwenye jema, wengine wetu ni lawama tuu, hakuna jema lolote!. Ila pia nakubali, jema kwangu, linaweza kabisa kuwa ni nothing kwa mwenzangu kama ilivyo concept ya maji kwenye glasi kati ya half full na full half!.

Paskali.
 
BADILI TABIA

Mkuu umesema yote niliyotaka kusema.

Jana nilikuwa namwambia mtu aliyoyasema mwanakijiji kuwa Waziri anaigiza. Kuna matukio yote uliyoyataja hakuna kilichofanyika.

Kwani Muhongo aje kutuambia haya wakati ni mambo yanayofahamika. Basi Muhongo awe rais wa nchi.

Kama sisahau kuna kipindi Mhando alitaka kujiuzulu lakini JK kamng'ang'ania. Madudu ya TANESCO hata ikulu hunufaika. Si Muhando na wachache tu.

Naona prof Muhongo kaja kupoteza vita, kauli yake ya " Tufunge mjadala huu " ni hatari.

Mwayembe alitufurahisha hivi hivi lakini matokeo zero.
Pinda aliwahi kukasirika tukafarijika lakini matokeo zero.
JK na kadhalika lakini matokeo ni zero.
 
Last edited by a moderator:
Naomba wapinzani wataje kwa majina wezi ambao ni wabunge na wengine.
Hili labda itasaidia.
 
Ukitaka ugomvi na watawala wa nchii watajwe kwa majina ghfla CCM na viongozi wa serikali wataungana pamoja kuwapinga wanaowataja kwani si lengo lao kudeal na ufisadi lengo hasa ni kutuhadaa ili CCM iendelee kutuwala.
 
duh..kweli mkuu uchambuzi wako ni mzuri sana...........lakini naomba kuchangia

Sera za CCM yaweekana kuwa ni mbovu ni kweli lakini kama bado kutatokea watu makini wenye uwezo wa kuzisimamia hata hizo mbovu lazima mabadiliko yaonekane. Mfano mzuri ni SERA ZA NYERERE kuhusu mfumo wa kijamaa nyingi hazikua nzuri au practical kwa ulimwengu wa sasa lakini NYERERE kwa kuwa alikua mtu makini nchi ilikua mbali sana na tulifika point hata uchumu wetu ukawa the best east and central africa na kipindi hicho dola ilifika piont ikawa ni sawa na TSH 5 tu.

Pia chukulia mfano wa america katiba yake ni moja ya katiba mbovu duniani lakini every one dreams to live in US and every the americans are proud to be Americans.

Tatizo kubwa la hii nchi ni watu wanaoweza kupima mambo kwa jicho la tatu na kuona mambo ambayo sisi raia wa kawaida hatuyaoni....
 
Mzee Mwanakijiji,

Ahsante sana kwa riwaya yako; labda umesahau jambo moja la msingi; wakati wa Mwalimu pamoja na kuwa tulikuwa chini ya cham kimoja bado alisisitiza na kuwakumbusha watanzania usimpigie kura mtu eti kwa sababu ni jirani yako, hivi sasa siasa ni biashara umegusia suala la wanasiasa kugeuza nafasi zao kufanya biashara ajabu umeongelea kwa upande wa CCM tu umesahau kuwa mwenyekiti Mbowe anafanya biashara na chama bila hata kufuata taratibu, uozo huu upo kwa wanasiasa wengi, nashauri tu waganga wa kienyeji warudi kwenye matunguri, wachungaji warudi kuhubiri, wanafanyibiashara warudi kwenye biashara siasa waachiwe wanasiasa wa kweli wenye uchungu na Taifa hili.

Chama
Gongo la mboto DSM
 

.......hata TAKUKURU watakapotangaza kuwa wameanza uchunguzi (na watafanya hivyo sometime next week au mapema zaidi) watu wataanza kushangalia kuwa sasa TAKUKURU ifanye kazi yake!

MMM
Binafsi sitashangilia hata chembe kwa kuwa, endapo leo nitaombwa kutaja taasisi moja inayopaswa kuvunjwa within a minute; basi sitapoteza hata nukta moja kuitaja TAKUKURU!! TAKUKURU ni janga, si janga la kitaifa, bali ni janga la dunia. Sawa na ambavyo mababu zetu walivyokuwa wanaitumia mibuyu, mapango na miti mikubwa kuhifadhi zana zao za matambiko na kafara; ndivyo ambavyo leo hii TAKUKURU inavyotumika kuhifadhi tunguri za rushwa na ufisadi!

 
Sasa naona umekubaliana na mimi indirectly na unaonyesha kukata tamaa, mimi nasema kila siku tatizo sio CCM tatizo ni UTAMADUNI wetu jinsi tunavyolelewa, Utamaduni huu hauwezi kutoa kiongozi mwenye sifa ulizozitaja, hatulelewi hivyo, badala ya kufundishwa uadilifu, moyo wa kujitolea kwa manufaa ya wengine n.k tangu utoto tunafundishwa uzinzi, uongo, ubinafsi, kutumiana kwa maslahi binafsi nk na wote tumekuwa ktk hayo mazingira awe Kikwete, awe Zito, awe Ngereja au Pinda sasa kutegemea matokeo tofauti na hayo ni kujidanganya!

Mtabadilisha Katiba mnavyotaka hata mkikopi na kupaste katiba ya Marekani au Japani hakuna kitachobadilika maadamu watendaji na watu wanaopaswa kutii na kueshimu hiyo Katiba wamelelewa na kukuzwa na huu Utamaduni wetu hakuna kitachobadilika!


OOp, Mimi ni mtanzania,sijakata tamaa kama wewe,na bado naamini TZ bado ina watu wa aina yangu wengi sana,tutaitafuta nafasi tutaipata na tutalitumikia taifa,taifa limetegemea uongozi kwa wale wenye uwezo mkubwa kujipendekeza kwa watawala hivyo kupewa nafasi na kutayarishwa kuwa watawala na hatimaye wameweza kututawala kwa ujinga wetu tumebeki tukiwashangilia kwa na kuishi kwa matumaini kama fisi ategemea mtembea kwa miguu adondoshe mkono kwa kuwa mikono inayumba mbele nyuma akitembea.
Naamini wakati unakuja na sasa umekeribia zaidi ambapo nchi itakuwa mikononi mwa watu ambao kilicho bora kwa kwao ni maisha bora na sio mali nyingi, Afrika kwa sasa inaongozwa na watawala wanaoamini juu ya mali nyingi tena mali binafsi na SI katika maisha bora kwa wanachi wote kwa ujumla.

TUSIKATE TAMAA TUNAYO NAFASI YA KUANZA UPYA NA KUOKOA TAIFA.
 
Maneno mengiii, ili kutaka jamii ikuone umesema jambo la maana! Ukweli utabaki pale pale wewe subiri siku ukishika nchi uje na hizo SERA zako zinazo wezekana, lakini kwa sasa endelea tu kupiga domo watu wanapiga kazi.

Good,wewe unawakalisha idadi ya kutosha ya watanzania waliotufikisha hapa amini muda wenu unakaribia ukomo. Najua ni vigumu kuamini kwa kuwa mnajiamini kuwa vyombo vya usalama vipo chini yenu, taasisi muhimu katika uchaguzi zipo chini yenu na nkubwa zaidi ni imani kuwa watz wengi wengi bado wanaabudi tshits na kofia,hakika unajidanganya...
 
wamba Mhando (Mkurugenzi wa Tanesco) amejipa mkataba yeye na mke wake na kukiuka waziwazi sheria ya maadili yaviongozi wa umma ya 1998 halina shaka.

Lakini cha kushangaza ni kuwa ati Waziri anaenda kumlipua Bungeni badala ya aliyemteua kumfukuza kazi, kumtia pingu na kuhakikisha anaingia gerezani yeye na wote waliowezesha dili hilo.

Whaaaat??!! Unafahamu fika kwamba hilo haliwezekani kwa mfumo uliopo sasa na halitakuja kuwezekana hata kama CCM itaondoka madarakani! Nchi yetu inafuata mfumo wa Utawala Bora, ambao moja ya nguzo zake kuu ni Utawala wa Sheria!! Katika Utawala na Utawala wa Sheria hilo katu haliwezekani kwani hadi hivi sasa Mhando ni mtuhumiwa tu na hadi pale itakapothibitika beyond reasonable doubt kwamba yanayosemwa dhidi yake ni sahihi ndipo ushauri wako unaweza kuwa na mashiko! Kama hivyo ndivyo, tufanye nini basi? KATIBA YA KIDIKTETA; Dictatorship Constitution itakayolenga ku-shape maadili mabovu ya Watanzania. Katiba ambayo, kila penye neno GOOD GOVERNANCE, pawe replaced na APPROVED BENEFICIAL DICTATORSHIP GOVERNANCE!

Tunaona Mwendesha Mashtaka Mkuu na Mwanasheria Mkuu hawafanyi lolote kuonesha nchi yetu inasheria je yawezekana na wenyewe wamepewa "mlungula" (vijana wanaweza kuwa wamelisahau hilo neno).

Hiyo nayo ni kansa nyingine isiyopaswa kuwamo ofisini japo kwa dakika moja ya ziada! Wabunge wetu wameshapoteza mwelekeo ingawaje sifahamu ni wakati gani wabunge wetu walipata kuwa kwenye mwelekeo sahihi....hapa wala asitokee mtu wa kuniambia waliokuwa sahihi ni wale ambao walikuwa enzi za utawala wa Mwalimu!! Hata wabunge wa upinzani nao hawana jipya....wanachopenda kuibua bungeni ni yale tu ya ufisadi wa moja kwa moja (Direct Corruption)! Wanasahau kabisa kwamba Indirect Corruption nayo ni mbaya pengine kuliko hiyo Direct Corruption. Wabunge wetu hawa, awameendela kulala usingizi wa pono kana kwamba kinachofanywa na TAKUKURU pamoja na Mwendesha Mashitaka ya Umma (DPP) nayo si ufisadi! Sijapata kusikia, wabunge wakikata kutoa hoja binafsi dhidi ya utendaji mbovu wa DPP na TAKUKURU!! Au kanuni za bunge haziruhusu kuwajadili watu hawa?! Leo hata kama utachukuwa Baraza lote la Kikwete na kulipeleka mahakamani; bado thamani yao haiwezi kulinganishwa na thamani ya Felesi (DPP) na mwenzake Hosea(wa TAKUKURU)

Hakuna namna ya kusafisha hili isipokuwa kuvunja hili Bunge kwani limechafuka na kulichafua taifa. Sijui watalivunja vipi lakini wananchi wasiwe na imani nalo na hawapaswi kuwa na imani nalo hasa kama watuhumiwa ndani yake bado wapo. Kwani si tuliambiwa kuwa kuna wabunge walikatiwa kitu wakati wa sakata la Jairo? Wako wapi? Wametiwa pingu lini? Nyet! Halafu kweli sisi na akili zetu tukiwa wanafunzi wa zuri wa historia ya karibuni tunaweza hata kutoa pongezi? POngezi kwa kitu gani? kutaja majina? kutuambia kinachojulikana?
Bado haitasaidia.... I REPEAT, HAITASAIDIA!! Tatizo la nchi hii ni zaidi ya Wabunge waliopo; bali ni ubovu wa maadili tulionao Watanzania wengi!! Maadili ya Watanzania yamemomonyoka kwa kasi ya kutisha ingawaje nayo sifahamu ni wakati gani yalipata kuwa mazuri.....hapa napo, wala asitokee wa kuniambia kwamba tulikuwa na maadili bora hapo zamani....kama zamani, basi ni labda kabla ya ukoloni!!

Hata kama bunge litavunjwa bado haitasaidia kwani endapo uchaguzi mwingine utafanyika watakaorudi tena bungeni ni Watanzania wale wale waovu wa maadili wasio na japo chembe ya soni!! Watanzania ambao hata viongozi wao wa kiroho nao ni wauza mihadarati! Unatarajia nini kutoka kwenye jamii chafu kama hiyo?! Jamii ambayo warekebishaji maadili nao ni mapusha?! Jamii ambayo, vijana ambao zamani walizaniwa kwamba kwavile wana muda mrefu wa kuishi basi wao wanaweza kuwa na uchungu na nchi yao lakini kinyume chake, nao wame-prove kwamba ni mafisadi wa kutisha, kuogopwa, wasiopaswa kuaminiwa hata kwa kuwapa michango ya sadaka!! Suluhisho la jamii mbovu kama hii ni KATIBA YA KIDIKTETA ambayo GOOD GOVERNANCE itakuwa replaced na APPROVED BENEFICIAL DICTATORSHIP GOVERNANCE! Katiba ambayo, hivi sasa Mhando ingekuwa tayari imeshamtupa korokoroni wakati akisubiria uchunguzi kukamilika.....!! Ni lazima atupwe korokoroni na kukaa huko ili asije kushambuliwa na wananchi wenye hasira! Ingekuwa yupo korokoni kwa usalama wa maisha yake! Ni kama muuaji....muuaji anaachwa korokoroni si kwa sababu ameua bali anaachwa huko ili asije akadhuriwa na ndugu wa marehemu!
 
Hamna lolote... Negative thinkers.. Dah kila kitu CCM haifai utadhani migwanda ndio ya maana.!! Sisi tunapiga kazi changamoto hazikosekani..
 
Nakataa MM,

Ndio tumeshaona drama za kila aina baada ya kuundwa tume za kuchunguza , lakini katika hili la Nishati na Madini wameingia watu wapya ambao si wanasiasa na wakaibua madudu ambayo yamefumbiwa macho

Kitendo cha kutaja wezi wa umeme bungeni ambao baadhi ni wabunge ni ujasiri mkubwa sana

Unaposema kiini macho sikuelewi kuwa nothing is coming out of this?

Kwa hili la MEM tayari hatua kadhaa zimechukuliwa

Kimsingi umetoa maoni yako na yana mantiki lakini I dare say sidhani yawe applicable mpaka kwa hili coz siligroup katika mazingaombwe...

Credit should be given where it deserves
Nsiande,tatizo ni kama nilivyosema,kuna a serious part of politics wananchi wengi hawaijui,na ndiyo maana unatakiwa uelewe kuwa hatua za kisiasa ni tofauti na zile hatuwa za kisheria.Viongozi na ccm na culture yetu,tumezoea kuwachukulia hatua za kisiasa hata wahujumu uchumi wetu.Na ndo maana kuna mchangiaji alisema hii sheria iliwekwa kwa makusudi na watu ambao waliliona hili tatizo,na sheria ikatungwa kulidhibiti,walioziondoa,nia yao ndo hii,lakini hatuna historia ya kuwahold accountable wahujumu uchumi,wanasiasa,yes,wengine na nchi washakimbia,mafisadi?jibu ni no,wanakumbatiwa.

Serikali kwa kujitapa na uhuru wa habari,halafu habari hizo kupuuziwa na kutokuchukuliwa hatua,hapo inaondoa ile seriousness ya kujuwa lipi ni kweli na lipi si kweli,ile mentality ya mashaka ya habari zinazoletwa nayo imeondoa ile dhana ya kuwahabarisha wananchi ili wachukuwe hatua stahiki kuhusiana na mustakabali wa nchi yao,badala yake,ccm wameweza sana kuitumia hii kuwapumbaza wananchi wake.Yani ishakuwa sawa na kusema "miluzi mingi humchanganya mbwa"

Kila siku tunaambiwa gazeti hili ni la kuamini na lile hapana.Statement hizo hutoka kwa wanasiasa pale wanapotaka gazeti flani ndo liaminike na wananchi.Magazeti flani flani hutokea kuaminika,lakini umaarufu baadaye nao unapotea.

Bottomline ndo hiyo,kwamba hizi kelele tunazifurahia,lakini bado haionekani kwamba furaha hiyo ndo chachu ya mabadiliko ama ni burudani tu kwa wasomaji?
 
MMM,

Nakubaliana na uchambuzi wao. Hata hivyo, hutendi haki kwa kambi ya upinzani. Kwenye hotuba yao wameyataja masuala yote makubwa zaidi ya hilo la TANESCO wa wameeleza matatizo ya kisera yaliyopo kwenye utawala wa CCM kuhusu nishati na madini. Hotuba imeeleza pia njia pekee ni kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo mzima wa utawala. Naamini wasingeweza kusema kwamba kwa kuiondoa CCM na kuchagua CHADEMA kwa kuwa ingeanza kusemwa kuwa wanafanya kampeni bungeni. Hebu fanya uchambuzi wa mwanzo na mwisho wa hotuba hiyo utapata majibu. Tatizo ni kuwa suala la TANESCO na Mhando ndio limeonekana hoja muhimu wakati kulikuwa na mengi.

serayamajimbo
 
Hakika hiyo ndiyo hali halisi ya siasa za nchi hii. Utendaji wa serikali ni Komedi, bunge ni Komedi, na hata mahakama ni Komedi. Wananchi ndiyo tumekuwa hadhira yao.
 
Hakika hiyo ndiyo hali halisi ya siasa za nchi hii. Utendaji wa serikali ni Komedi, bunge ni Komedi, na hata mahakama ni Komedi. Wananchi ndiyo tumekuwa hadhira yao.
Huku tukifurahia the show na kila miaka mitano, tukiwaajiri tena huku tukidunduliza na kuchangishana pesa za mishahara yao kwa miaka mitano mingine, na 2015 tutawaajiri tena ili tuendelee kufurahia the comedy show!.
 
Mkuu MM nakupongeza sana kwa analysis nzuri,it is really an eye opener,jana nilishtuka kusikia watu wakisema prof.muhongo anastaili kuwa waziri mkuu,sijui kipya ni kipi walichokiona,kweli nimekubali tunaongozwa na matukio.We need to change our mind set.
 
70 Reactions
Reply
Back
Top Bottom