Granta
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,082
- 6,425
Mkuu mara nyingi sana sisi watz na waafrika kwa ujumla, Neno 'SINA MTAJI" ndio excuse kubwa ya kuhalalisha umasikini wetu. Mimi napingana kabisa na excuse hii. TATIZO LETU KUBWA ni kukosa LENGO na NJIA (plan) pamoja na UTASHI wa kufikia Lengo Hilo.
Hebu fikiria, Leo ni jumapili. Je, kuanzia j3 hadi jumamosi umetumia kiasi gani cha fedha kwenye matumizi yako ya kawaida? fedha umetoa wapi?? Huko huko ulikotoa fedha uliyotumia kuanzia jumatatu hadi leo, ndio kwenye mtaji wako, haijalishi ni kiasi kidogo kiasi gani! Wakati nasomea degree yangu ya Business Administration, mwalimu wangu alinifudisha strategy ya kuanzisha biashara ni hii "start small, think big"
Mkuu, una uhakika watu hao wanafanya matumizi yeyote kuanzia j3 hadi j2...? Watu hata hela ya kula hawana zaidi wanakula kwa wazazi ama ndugu...
Tambua tu watu wanaposema hawana mtaji ni kuwa hawana kitu kbs, japo sio wote ila karibu wote hali ndio hii...!
Sasa tunashangaa hao watoto wa vigogo badala ya kujiajiri maana wana means ya kupata mtaji ndio kwanza wanatafutiwa ajira NONO...
MI nalaumu yule ambaye yuko na ajira na akashindwa kufanya mambo mengine akabakia tu kutegemea salary...!