Nimejaribu"ku-google"tusi linalofaa kukutukana nimelikosa,ila kwa ujumla unapaswa kupuuzwa zaidi ya upuuzi wenyewe.Acha kiburi cha kiitikadi,kuwaita watanzania wenzako "ng'ombe pori" ni jambo lisilovumilika na ni kielelezo cha dhahiri namna serikali hii ya mwendokasi ilivyofanikiwa kuwagrade raia wake katika matabaka mbalimbali.
Ni ujinga usiomithirika kuliona jeshi letu likitulazimisha tulipigie makofi hata pale tunapolishuhudia dhahiri likitumika kama "kipaza sauti" na mlinzi wa propaganda za serikali.
Jeshi lililozikimbia kambi zake na kuvamia bila kibali maeneo ya wazi na kuanza kuyatumia kama kambi za mafunzo na mazoezi kamwe haliwezi kuvumilika.Ni upumbav wa kiwango cha PhD kuendelea kuliamini jeshi hili lililoacha misingi ya kuanzishwa kwake na sasa limeamua kujisajili rasmi kama tawi la chama cha mapinduzi.
Inasikitisha pale serikali na Taasisi zake kudhani inaongoza misukule isiyoweza kufikiri,serikali haiwezi kupiga marufuku kila kitu alafu akadhani imeweza,kuwazuia watu kujadili mustakabali wao ni hatari zaidi kuliko kuwapa fursa ya kuongea na kutoa hisia zao za ndani.Wako wapi wenye hekima wawezao kuushauri utawala huu uliojiapiza kupambana na kila anaouhoji?
Kabla jeshi la policcm halijaanza kupambana na wale linaowaita wachochezi na wanaolibeza mitandaoni ni vema likajitafakari mwenendo wake kama ni wa haki na unastahili kuheshimika.Linapaswa kwanza kuzivunja kambi zote za mazoezi ya kivita zilizoko mitaani na barabarani na lirudi kambini likafanyie mazoezi yake ya ukakamavu huko.
Kitendo cha jeshi "kutoroka kambini" na kufanyia mazoezi yake barabarani kimeonesha udhaifu mkubwa sana wa kiuweledi na kiintelijensia,kufanya mazoezi ya kijeshi barabarani huku yakiambatana na maonyesho ya silaha za kivita ni kuwapa fursa maadui kufahamu uimara na udhaifu wa jeshi lako.Huu ni upumbav wa karne na ni kielelezo cha mwisho kabisa cha utawala ulioingia madarakani kwa hila jinsi unavyojaribu kukikimbia kivuli cha hila zake kwa kuzuia kila fursa inayoweza kuhoji uhalali wa serikali yenyewe.
Sasa ninaanza kuamini kuwa PhD ya "malaika mkuu" ni PhD ya kipekee sana,aina hii ya utawala inayoruhusu askari kuandamana katika misururu mirefu barabarani wakiwa wameambatana na zana za kijeshi ni mfumo mpya wa utawala ambao haupatikani popote duniani isipokuwa nchi ya wadanganyika.Kiongozi aliyezuia mikutano na maandamano ya kisiasa kwa kigezo kuwa mikutano na maandamano hayo vitawanyima wananchi muda wa kufanya Kazi,je maandamano ya policcm katikati ya miji na majiji hayaathiri ufanyaji wa Kazi wa watanzania?
Ngoja niishie hapa ila natabiri vituko Na vioja zaidi huko tuendako.