Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Hii habar mbona Title ni tofauti na body.
TITLE INAONGELEA WANAOBEDHA JESH LA POLIC MTANDAONI. BODY LINAONGELEA WAHUSIKA WA MAUAJI YA POLICE.
 
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.
Kama linafanya makosa tusiongee kuwa tutakamatwa, basi waanzie kwangu kawaida yangu sina uwoga wa kijinga kiasi hicho. Wasipende kuwalazimisha watu kutokosoa jeshi la polisi na badala yake wao kama viongozi wa jeshi hilo wajihoji kwanza ni wapi walikoanguka wasahihishe... Over
 
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.
Si kweli kwamba walilenga kuwashambulia askari. Kwa mazingira hayo inaonyesha walilenga kupata bunduki na risasi. Vinginevyo wangemimina risasi tu na kuondoka.
 
Yaani hawa watu wanataka kutufanya sisi wajinga au? Nina uhuru wa kueleza maoni yangu popote pale bila kuvunja sheria za nchi! Iwe nashabikia au naongelea jambo lolote lile nina uhuru huo! Yaani wanataka kutuchagulia maneno ya kuongea? Mimi kila siku nasema mama Ndalichako aangalie vizuri hii wizara! Yaani kuna watu wanaongea ukiambiwa alieongea hayo ni mtu mwenye cheo fulani unainamisha kichwa chini!
 
Ni haki yangu kusifia au kukosoa sasa kama wana mamlaka hiyo basi wamejipa wenyewe..!
 
Hizi nguvu za kuwakamata watu mitandaoni bora wangezielekeza kwenye kuwasaka wale manyambisi waliowaua askari wetu,akisimama polisi na mwanasiasa siku hizi hawana tofauti wote kama wako kwenye jukww la kuomba kura.
 
watu walishasema. baada ya huko kwote kunyamazishwa watakuja kwenye social network. hakuna aliyesalama .
 
"Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo." 🙁🙁🙁
 
Eti leo mchana nimetafakari utolewaji wa taarifa ya mauaji ya polisi... nimejiuliza wale walouawa ni askari?

Kuna mtu kauliza kwa nini Mkuu wa polisi aense na nguo za kiraia lakini Waziri aende na nguo za kipolisi tena mpya?

Na hata zile za ile picha ya askari anayeonekana kalala chini pia ni mpya......

Niliwaza tuu.
 
Watu mitandaoni wanahoji na wanatoa hoja zao sasa na wao polisi watoe hoja ili kuwafahamisha wana mtandao. Sio kuweka mikwara tutaingia kaburini ije kuwa jela?
 
Na aibu na huzuni....Polisi kuporwa silaha? wana haja kuongeza bidii idara yao ya upelelezi ili kuzuia matukio ya uhalifu kudhibitiwa kabla ya kutokea badala ya kufuatilia wanaokosoa utendaji wao
 
wanashindwa kutazama walipojikwaa wanatazama walipoangukia, imekuwaje chuki kwa sasa tu? kwanini isiwe toka enzi?
jitathmini upya tatizo liko wapi?
na hakuna sehemu mabavu yametumika yakafaulu hata sehemu moja,
Umenena vema comrade
 
Hv kumbe lazima kumpenda m2. Sifa njema huambatana na matendo mema!! Mm ni mdogo wake mwangosi utegemee kuna siku nitawapenda police na kuwasifia kwa matendo yao?? Tuombe Mungu atuepushe chuki isizid kusambaa. Huwez kulazmisha m2 akupende
 
Back
Top Bottom