Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

mimi sijawahi ona Police wakifanya mazoezi kwenye bara bara ya Lami na kuacha kujificha porini huko mkiambiwa mnakua wakali...nalaani sana ila sehemu hizo sio maana mbinu adui anazijua kirahisi na pia na nyinyi muache kutupia picha zenu mtandaoni maana waarifu wanaficha mbinu zao kwa nini nyinyi muwe wawazi kiasi hicho.., hili ni janga tunategemea mkae vikao vya kuleta suruhisho na kuacha kushinda huku kusoma na kujibu visivyoeleka..
 
Kwa kweli hakuna anaefurahia kifo cha mtu ila jeshi la Polisi lijitafakari wapi limeteleza na Ashukuriwe Mungu asilimia kubwa wanaishi kambini laa kama wangekua wako uraiani sijui tu
 
Tafuteni sababu halisi. Vijana wenu huko mtaani hawaheshimu sheria za uraiani wala za barabarani. Wababe wao, wenye nguvu wao, fulu tambwe. "Utanijua mie nani"? Haya mambo ndio yanajenga image mbaya kwa askari polisi kiasi mtu anajikuta hayuko salama hata kukutana na polisi kutokana na ubabe wao mtaani.
 
Haaa.. ila Mbagara, yare majambazi razima tuyakamte, razima, na huku mitandaoni atakaye dhubutu kuchochea watu tunarikamata reo reo.. na hatutaki utani mura..
Mfarme J uko vizuri, yare najua razima uyakamate.
Vijana wako ni no.1 in ze werdi, wanapiga jambazi popote pare
 
Huwezi kulazimisha upendo...upendo hujenga..... jeshi la police linalofanya kazi kwa manufaa ya jamii haliwezi kubezwa na inapokuwa kinyume chake lijie kuna sehemu limeteleza.
 
POLISI ni taasisi muhimu ikitumika ipasavyo, ni ndugu zetu tunaishi nao, tunakula nao. Tatizo lao wanajiona peculiar kuliko watu wengine. Mbona Walimu tunaishi vizuri na JAMII? Ili wadhibiti uharifu wajenge mahusiano mema na JAMII sio gaps. Pia wawe politically neutral wasiegemee CHAMA chochote cha siasa. Mbona JWTZ, wanakubalika sana uraiani? HATA wakipata tatizo JAMII ikotayari kutoa ushirikiano. Tathmini ifanywe kujua jeshi letu limejikwaa wapi.

Japo ni upumbavu kukejeri askari wetu wanapopata matatizo tuwe wazarendo
Huu ni mfano mzuri sana uliotoa. JWTZ vijana wake huko mtaani wako "cool" kabisa, wanashitikiana vizuri na raia na hawana show up. Na wengine utakaa nao miaka hata hujui kama ni wanajeshi mpaka siku uingie anga zao. Polisi wajifunze kujenga utii kwa vijana wao kama jeshi la Wananchi linavyofanya.
 
Ukijiandaa kupeleka msiba kwa jirani hali ya kuwa ndani mwako una wagonjwa UTAANZA KUZIKA wewe na majirani watakusindikiza kwa wingi sana.POLE sana kamanda Sirro,JITATHIMINI kisha waandae vijana vyema dhidi ya WAHALIFU na sio kwa mazoezi dhidi ya CHADEMA kwani tukio la jana LIMETUSHUSHA hadhi kama Taifa,kama Kanda yenye nguvu TAnzania lakini kubwa kabisa kama JESHI kuuwawa na RAIA ni aibu na fedheha kwa Jeshi linalopiga jaramba takribani wiki mbili mfululizo sasa.
My TAKE: #NikoTayariKwaUKUTA sep 1.
 
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.
Hiki kiwango cha vitisho sasa naona kama kinapitiliza mipaka! Je, Tza ni nchi yenye utawala wa kijeshi? Lakini sijasikia hilo! Je, wanataka kuzuia kabisa uhuru wa mawazo? Siamini kama tunapaswa kwenye huko...hawataki kukosolewa? Ni Mungu tu asiyekosea! Mimi si mwanasiasa lakini naona kama tunavuka mipaka. Kwa nini tuwaogope walinzi wetu badala ya kuheshimiana? Chonde chonde...nadhani kuna mtu mwenye hekima hapa anayepaswa kuingilia kati ili turudishe Tza yenye upendo watu wanaoheshimiana na kusaidiana. Naomba polisi msitujengee chuki dhidi yenu. Tumezoea kuishi na kushirikiana nanyi...chonde chonde! Naomba sasa jeshi lichunge kauli zao kwa waajiri wao-watzania ili kulinda heshima yao. Hii hali inaweza kuwalazimisha waliokaa kimya kuanza kucomment hadharani...Na Hali inaweza kuwa mbaya kwani inaweza kujengwa hisia kuwa watu fulani ni wabaya....
 
Wajiulize wamekosea wapi... Hakuna anyependa police wetu apigwe na kuuawa. Inapotekea amepigwa alafu watu wakashabikia aliye piga police waje na majibu wamewakosea nini watanzania.
Maneno kuntu
 
Polisi polisi polisi nahisi kama kunadalili ya kupoteza uelekeo !Chamsingi walitakiwa kutumia udhaifu unaosemwa na wanadau mbalimbali wa usalama na kuufanyiakazi kwa kuondoa mapungufu yaliyopo.

Na hasa hili suala la kupoteza askari na silaha. Tatizo limeanza hata kabla Ukawa na Ukuta havijaanza. Viongozi wa jeshi wanatakiwa walifanyie kazi
 
Sidhani kama maonesho yalikuwa dhahiri. Unaweza kuamini polis waliofanya zoezi mwezi kuuawa na raia wenye bodaboda? Mm niliona wakionesha kwenye TV magari makubwa, mbwa, magari ya maji washa, risasi za hewan nk, kumbe raia anawadhibiti! Ajabu kweli!!?
 
husema siku zote wakumbuke wanaishi mitaani kwetu au wana ndugu zao mitaani kwetu, wasijenge chuki na raia
 
Back
Top Bottom