Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.
 
Polisi walivamiwa pale na majambazi, polisi mmoja aliruka kama Amitha Bachan akampiga binduki yule jambazi akafa, mwingine akaruka samasolt ya hatari akamuulia mbali yule jambazi.

Polisi wetu ni no. One na hatari kabisa ktk ukanda wa afrika na duniani.
Hakuna polisi anayeikuta polisi ya Tz hapa duniani
 
Hakuna anayeshabikia uhalifu wala askari wetuu kuuawa. Ukweli ni kwamba weledi wa polisi wetu ni wa chini sana na ndio maana wanakumbana ni makasa yote hii. Dawa ni kujirekebisha na kufanya kazi kwa mujibu wa taaluma yao na si kuwa wakali wanapoambiwa ukweli.
 
Polisi walivamiwa pale na majambazi, polisi mmoja aliruka kama Amitha Bachan akampiga binduki yule jambazi akafa, mwingine akaruka samasolt ya hatari akamuulia mbali yule jambazi.

Polisi wetu ni no. One na hatari kabisa ktk ukanda wa afrika na duniani.
Hakuna polisi anayeikuta polisi ya Tz hapa duniani
Comment za Hivi zitabarikiwa!!Ndo wanazotaka
 
Kwa hapa nalipongeza sana Jeshi letu la polithi kwa intelligencia hii ya kugundua kuwa kumbe wanamitandao wamelichoka.Nawaomba tu wajitahidi kuboresha hiyo INTELLIGENCIA yao iwe ina Baini na attack kama ya Jana.I salute u gayz
 
Ni ujinga usiomithirika kuliona jeshi letu likitulazimisha tulipigie makofi hata pale tunapolishuhudia dhahiri likitumika kama "kipaza sauti" na mlinzi wa propaganda za serikali.

Jeshi lililozikimbia kambi zake na kuvamia bila kibali maeneo ya wazi na kuanza kuyatumia kama kambi za mafunzo na mazoezi kamwe haliwezi kuvumilika.Ni ajabu wa kiwango cha PhD kuendelea kuliamini jeshi hili lililoacha misingi ya kuanzishwa kwake na sasa limeamua kujisajili rasmi kama tawi la chama cha mapinduzi.

Inasikitisha pale serikali na Taasisi zake kudhani inaongoza watu isiyoweza kufikiri,serikali haiwezi kupiga marufuku kila kitu alafu akadhani imeweza,kuwazuia watu kujadili mustakabali wao ni hatari zaidi kuliko kuwapa fursa ya kuongea na kutoa hisia zao za ndani.Wako wapi wenye hekima wawezao kuushauri utawala huu uliojiapiza kupambana na kila anaouhoji?

Kabla jeshi la police halijaanza kupambana na wale linaowaita wachochezi na wanaolibeza mitandaoni ni vema likajitafakari mwenendo wake kama ni wa haki na unastahili kuheshimika.Linapaswa kwanza kuzivunja kambi zote za mazoezi ya kivita zilizoko mitaani na barabarani na lirudi kambini likafanyie mazoezi yake ya ukakamavu huko.

Kitendo cha jeshi "kutoroka kambini" na kufanyia mazoezi yake barabarani kimeonesha udhaifu mkubwa sana wa kiuweledi na kiintelijensia,kufanya mazoezi ya kijeshi barabarani huku yakiambatana na maonyesho ya silaha za kivita ni kuwapa fursa maadui kufahamu uimara na udhaifu wa jeshi lako.Huu ni upuuzi wa karne na ni kielelezo cha mwisho kabisa cha utawala ulioingia madarakani kwa hila jinsi unavyojaribu kukikimbia kivuli cha hila zake kwa kuzuia kila fursa inayoweza kuhoji uhalali wa serikali yenyewe.

Sasa ninaanza kuamini kuwa PhD ya "malaika mkuu" ni PhD ya kipekee sana,aina hii ya utawala inayoruhusu askari kuandamana katika misururu mirefu barabarani wakiwa wameambatana na zana za kijeshi ni mfumo mpya wa utawala ambao haupatikani popote duniani isipokuwa nchi ya wadanganyika.Kiongozi aliyezuia mikutano na maandamano ya kisiasa kwa kigezo kuwa mikutano na maandamano hayo vitawanyima wananchi muda wa kufanya Kazi,je maandamano ya polisi katikati ya miji na majiji hayaathiri ufanyaji wa Kazi wa watanzania?

Ngoja niishie hapa ila natabiri vituko Na vioja zaidi huko tuendako.
 
Polisi mtamtafuta mchawi mpaka mwisho wa dunia, ila adui yenu sio watanzania, bali ni kukosekana kwa weledi katika jeshi lenu la Polisi.
Humuwezi kutulazimisha tuwapende au tuwape ushirikiano wakati nyie hamtutendei ilivyo haki!

Jiulizeni kwanini watanzania hawawapendi kabla ya kuanza kutishia tishia raia!
 
Wakikosolewa ndio watakuwa makini! Haiwezekani mtuzibe midomo kila mahali.

Inatakiwa jeshi la polisi lituheshimu na sisi tuwaheshimu!
 
Tatizo kubwa ni watu k
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.

Tatizo kubwa ni pale uumwapo mguu wewe ukatibu kichwa. Hivi why wasijiulize tatizo ni nini? Kwa maana hata nyumbani ukiona mtoto anaanza tabia mbaya lazima kama mzazi uchunguze tatizo ni nini? Ndipo utafute mbinu ya kurekebisha. JESHI LA POLISI CHUNGUZENI NINI CHANZO CHA KUFIKA HAPA TULIPO. WATU HAWANA HURUMA TENA NA VIFO VYA ASKARI KWA NINI? SOTE NI NDUGU TUTAFUTE SABABU KUNTU
 
Polisi wetu wanafanya kazi nzuri sana. Nawashangaa sana wale wanaolibeza
Hakika wanafanya kazi nzuri, lakini ujambazi kuuhusisha na siasa ni kutafuta excuses Kwa kushindwa kwao kudhibiti kushambuliwa na kuporwa silaha kulikoanza kuota mizizi
 
Nimezoea kuliona jeshi letu la polisi likipokea positive critcism bila kinyongo.Frankly sitegemei mabadiliko.Ni lazima watu wawe mature.Tufike mahali tuone kwamba criticism zinajenga.Hewala bwana inabomoa.
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.
 
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu
mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.
Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande,
Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili
wahalifu.
Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia
‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.
CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu
bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.
“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote

ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;
“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu

kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili
sheria ichukue mkondo wake.”
Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.

Ni kweli kabisa jeshi la polisi lazima liheshimiwe na liachwe litekeleza majukumu yake lisiyumbishwe kwa ni yoyote
 
Polisi polisi polisi nahisi kama kunadalili ya kupoteza uelekeo !Chamsingi walitakiwa kutumia udhaifu unaosemwa na wanadau mbalimbali wa usalama na kuufanyiakazi kwa kuondoa mapungufu yaliyopo.
 
Tukisema ukweli tunasakwa daaah ngoja tukae cul tusije kuwa tunachochea....Time will tell.
 
POLISI ni taasisi muhimu ikitumika ipasavyo, ni ndugu zetu tunaishi nao, tunakula nao. Tatizo lao wanajiona peculiar kuliko watu wengine. Mbona Walimu tunaishi vizuri na JAMII? Ili wadhibiti uharifu wajenge mahusiano mema na JAMII sio gaps. Pia wawe politically neutral wasiegemee CHAMA chochote cha siasa. Mbona JWTZ, wanakubalika sana uraiani? HATA wakipata tatizo JAMII ikotayari kutoa ushirikiano. Tathmini ifanywe kujua jeshi letu limejikwaa wapi.

Japo ni upumbavu kukejeri askari wetu wanapopata matatizo tuwe wazarendo
 
Back
Top Bottom