simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,699
- 9,590
Hivi kwa akili za kawaida tu polisi inayo rasilimalima ya kuzuia maandamano vitongoji vyote vya dar es saalam tu achilia mbali Tanzania nzima.
Aisifuye mvua imemnyea. Mkuu Lizaboni anawasifu polisi kwa kuwa imewasaidia kwa kiasi cha kutosha kuwadhibiti UKAWA na kuistawisha CCM...na hii ndio furaha ya kila mwanaCCM...kuhakikisha kwamba upinzani unadhibitiwa kwa gharama zozote zile.
Ukweli mara nyingi unauma ndugu yangu.Bado inaonyesha wazi jinsi gani polisi wanakosa weledi na uvumilivu. Waache watu waeleze hisia zao. Kilichofanyika ni uzembe wa hali ya juu. Polisi wasitumie defensive mechanism kuficha udhaifu wao. Tumewaona mitaani wakitamba na silaha nzito, tumesikia mara nyingi wakisema wana intellejensia kali, inakuwaje intellejensia ya polisi ishindwe kubaini mipango ya waharifu waliyotekeleza tukio la jana usiku? Kuwashambulia wanaotoa maoni siyo suluhisho la matatizo. Wao polisi wapambane na waharifu. Kugeukia wananchi wanaotoa maoni yao na kuelezea mawazo yao kuhusu utendaji wa kiwango cha chini cha jeshi la polisi na kuacha kushughulikia kiini cha tatizo ni kuonyesha jinsi gani jeshi la polisi halina uwezo wa kukabiriana na matukio ya kiharifu kama lile lilotokea jana.
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.
Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.
Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.
CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.
“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;
“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”
Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.
======
Wewe adui yako akipatwa na mabaya hutoshangilia? Polisi ni adui wa wananchi kutokana na manyanyaso na uonevu wanaoufanya katika jamii. ndo maana watu wanashangilia pindi polisi wapatapo matatizo.mie naona watu hao wasakwe, kwa kuws hata kama MTU unamchukia kiasi gani si vema ufurahi kwa yeye kufikwa na baya...kwanza inaonesha kuwa hawa washangiliaji wanahusika kama sivyo basi no watu wenye mihemuko ya siasa bila kujielewa. kwa mfano MTU anahukumiwa kwa kumtukana raising alafu chama Fulani kinajitangaza kupitia watu wake kuwa kitalipa faini hiyo...jibu ni moja tu kuwa chama hicho ndicho kimemtuma atukane...ningekuwa magufuli sijui ingekuwaje!