Wanaosema Wasukuma ni Wakarimu, wana upendo halafu muda huo huo wanapenda ushirikina na Uchawi, hawajui kile wanachokisema

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Bila Shaka mpo Pouwa!

Miaka na miaka nimekuwa nikisikia Watu wakisifia baadhi ya makabila Kwa Sifa nzuri, moja wapo ya Makabila yanayosifiwa ni pamoja na Ndugu zangu Wasukuma(kwani Mimi ni Mnyamwezi). Sifa wapewayo ni Upendo, ukarimu na kuwa Watu Wema.

Lakini muda huohuo utasikia Wakiimbiwa kuwa wanasifa Mbaya ya kupenda Uchawi na ushirikina.

Sasa huwaga najiuliza, hivi hawa wanazungumza kile wanachokijua au wanabwabwaja kupitisha siku ziende.

Hivi tangu lini MTU anayependa Uchawi na ushirikina akawa na upendo, ukarimu na Wema. Uchawi upi huo na upendo Kwa maana ipi?

Kwa msio na uelewa tuu, niwajuze; haiwezekani MTU mchawi na mshirikina akawa na Upendo, ukarimu na akawa Mwema. Haijawahi kutokea na kamwe haitokuja kutokea.

Ukishakuwa mchawi automatically unakuwa MTU mwenye Roho mbaya, mkatili, mbinafsi na usiyejali lolote.

Hata hivyo Katika Taaluma za Uchawi moja ya ethics(maadili ya Kazi Yao ni pamoja na hivi).

1. Wachawi na washirikina huigiza ukarimu, upole, upendo na Wema kuficha Tabia zao za ndani.
Mshirikina na mchawi aliyekwiva sio mtu wa kupenda magomvi, mara nyingi NI wapole na unaweza kumfanya chochote na asijibu mapigo. Lakini ninakuhakikishia ukimpa mgongo utaisoma namba kama upo Dhaifu.

Ukisikia Watu wenye kelele nyingi, matusi, sijui kupigana pigana mara nyingi hawawezi kuwa wachawi au washirikina.
Wazee WA haya namuachia Mungu, Sawa wewe mjanja, anyway yameisha. Thubutu!

Watu Wema na wenye upendo mara nyingi wapo very straight, na NI rahisi kuwachukia

Narudia ukishakuwa mchawi na mshirikina, automatically haupo kundi la Watu Wema, Wakarimu, wenye upendo na zaidi huwezi kuwa miongoni mwa jamii zenye Akili.

Nawasilisha
 
Inamaana gani Mkuu?
Screenshot_20230814-124734_Chrome.jpg



Sio kila msukuma ni mkarimu na wala sio kila msukuma ni mchawi.
 
Hakuna binadamu mkamilifu wote wanamapungufu ni kweli wasukuma wana ukarimu lakin pia wanamapungufu yao kama binadamu wengine

Sema unalazimishaga content sana alafu asilimia kubwa ni pumba

Hoja yangu ni kuwa huwezi kuwa mkarimu alafu hapohapo unasifa ya Uchawi. Wapi huelewi kijana.
 
Back
Top Bottom