Wanafunzi wa kichawi wanapokuwa internship "Field" au mafunzo kwa vitendo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
WANAFUNZI WA KICHAWI WANAPOKUWA INTERNSHIP "FIELD" AU KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO.

Anaandika, Robert Heriel

Baada ya kupokea kozi fupifupi au ndefu katika taaluma ya Uchawi na ulozi ni muhimu kwenda Internship au field au Kwa Kiswahili fasaha tunasema kwenda kwenye mafunzo Kwa vitendo for career exploration and development. Kukazia maarifa, kuimarisha na kukazia ujuzi na uzoefu katika taaluma ya kichawi. Uchawi kama taaluma zingine kama vile mambo ya Utume na Unabii au Uaskari au uanajeshi au pengine utabibu, uanasheria, ualimu n.k. unajali Kanuni za kitaaluma katika ujifunzaji na ufundishaji.

Katika taaluma za Kiroho ikiwemo Uchawi, Unabii na utume, uganga na uganguzi, kuna makundi mawili.
a) Kundi la Kwanza ni kundi la Wateule ambao wao walichaguliwa kutumikia nafasi zao tangu wakiwa katika matumbo ya Mama zao.
b) kundi la pili ni lile ambalo mtu yeyote Kwa utashi na uamuzi, na kupenda kwake anaamua kusomea taaluma ya Uchawi, Unabii, uganga n.k

Kundi la kwanza, kidogo linaunafuu Kwa sababu kwenye ujifunzaji wa mambo haya halitumii nguvu nyingi Kwa sababu Uchawi au Unabii na nguvu zake zimeunganishwa naturally tangu kuzaliwa. Hii ni tofauti na kundi la pili ambalo hutumia nguvu kubwa kujifunza. Ingawaje, kundi la pili linaweza kufurahia Kwa sababu ni uchaguzi binafsi, Wakati kundi la Kwanza linaweza kujikuta kwenye kuamuliwa pasipo ridhaa Yao.
Assume umezaliwa ukajikuta unganguvu za kipekee za ajabu ambazo ndani ya jamii yako wanaziita nguvu hizo Uchawi. Alafu ukawa hautaki Sifa hiyo. Hapo utakuwa umeamuliwa.

Kwa upande wa Unabii, Nabii kama Musa au Elisha. Hawa walikuwa ni manabii tangu kuzaliwa, lakini walikuwa na watumishi wao. Mfano Mtumishi wa Musa alikuwa ni Joshua, na Mtumishi wa Eliya ni Elisha. Au Yesu ni Nabii Kwa kuzaliwa lakini aliteua Wanafunzi 12 ambao aliwafanya mitume.
Hivyo hapo kuna Nabii Kwa kuzaliwa na wapo manabii au mitume Kwa kufundishwa.

Hivyo hivyo kwenye taaluma ya Uchawi na Ulozi au uganga na Uganguzi. Wapo wanaozaliwa natural wanaandaliwa kuwa wachawi tangu wakiwa matumboni na wapo wanaofundishwa au kujifunza Baada ya kuzaliwa.

Sasa leo Taikon atazungumzia kundi namba Mbili. Yaani wale wanaojifunza au kufundishwa Uchawi na jinsi wanavyoenda mafunzo Kwa vitendo, almaarufu kama Field;

Mchawi na mganga wanasoma kozi moja. Yaani Kwa kifupi Mchawi ni mganga na mganga ni mchawi. Uchawi unaweza Kutumika kama uganga, na uganga unaweza Kutumika kama Uchawi. Inategemea na mhusika anataka apate matokeo gani. Ila kaa ukijua mchawi na mganga ni MTU mmoja na wanachukua Kozi moja.

Kozi wanazosoma ni kama ifuatavyo kulingana na mitaala na miongozo ya kufundishia;
1. Elimu viumbe
Kisayansi walioenda shuleni wanaita Biolojia. Kozi hii inavijikozi vingi kama ifuatavyo;
I) Elimu ya Binadamu.
Hapa Mwanadamu atasomwa na kuchambuliwa ndani nje. Aina za binadamu. Hapa kitu kikubwa kitakachoangaliwa ni vitu viwili ambacho ni DAMU na NAFSI. Kwenye Topic ya Damu hapo watasoma ishu za vinasaba na lengo kubwa ni ku-trace Historia ya MTU husika, lakini pia kumsajili katika database ya kichawi. Zingatia Damu NI chakula cha Nafsi. Ndani ya damu ndipo kuna Seli za mwili, na magonjwa mengi ya kimwili na kinafsi yapo kwenye Damu. Hivyo unaweza kuona umuhimu wa Wachawi katika kujifunza mada hii. Kwenye mada ya Nafsi watajifunza ishu ya Nyota, hapa ndipo ilipohatma ya mtu. Kujua MTU huyu ananguvu Kwa kiwango gani, vipawa vyake ni vipi. Akili, fikra, hisia zote zipo katika Nafsi ya mtu.
Nafsi ya mtu ndio huzalisha mambo mawili ambayo ni Silika na hulka ambayo Kwa Lugha iliyozoeleka huitwa Tabia.
Kwa ujumla kupitia vinasaba(damu) watakuwa wamechukua Genotype na phenotype ya mtu husika. Yaani kuanzia maumbile ya nje kabisa na maumbile ya ndani kabisa.
Kwa waganga na wachawi WA kujifunza, ukiwapelekea DNA ya mtu iwe kupitia Nywele, damu au Jambo lolote lenye vinasaba, katika Ulimwengu wa kichawi DNA hiyo ikiingizwa anatokea Mtu mzima mzima kama alivyo. Unaweza sasa ukaelewa ni Kwa nini ukienda Kwa mganga kitu cha Kwanza watakachofanya ni kukuchanja chale au kama unamuendea MTU basi watataka moja ya vitu vinavyobeba vinasaba(DNA) ya mtu husika.
Na kama tayari uliwa kusajiliwa yaani DNA yako Ipo kwenye Database ya wachawi basi Hawana haja ya kukuchukua damu(kukuchanja) Kwa lengo la kukutambua, labda Kwa lengo la kukuwekea Alama ya kukukinga, yaani kukuweea kisimbuzi kama cha DSTV ambacho bila Shaka utakuwa unalipia Kwa namna mlizokubaliana(ingawaje wengine hukuchanja bila kukuambia makubaliano yoyote alafu baadaye kwenye kulipia Vifurushi vya kisimbuzi inakuletea shida)

ii) Elimu Mimea
Hapa watasoma mitishamba Kwa Aina zake na kazi zake, kulingana na kiwango cha elimu alichopo. Kila mtu unakazi yake katika Damu na Nafsi ya binadamu. Ipo miti ni Dawa na mingine Ipo ni sumu. Wanafundishwa.
Kwa mfano Ipo miti ambayo unga wake ukiutwanga ukamuwekea MTU kwenye ngozi anawashwa, hiyo hata kisayansi Ipo.
Ipo miti ambayo magamba yake yakisagwa na ikachanganywa na mifupa au madini Fulani humfanya mtu aone mambo yasiyoonekana Kwa macho ya kawaida.
Ni kama kwenye sayansi ya tiba, mfano, ukienda hospitalini ili Daktari wa Ultrasound (USS) aone vizuri tumbo la mama mjamzito au tumbo lako basi atakuambia ubanwe na mkojo kabisa, kisha ukishabanwa atapaka kikiminika flani tumboni mwako ndipo achukue USS. Halikadhalika na kwenye taaluma ya Uchawi.
Elimu Mimea itahusu Mimea kulingana na Aina zake, Tabia zake, udongo unaootea, Tabia ya nchi, Mimea ya Majini(najaribu, ziwani, Mtoni) au Mimea ya ardhini(jangwani au kwenye udongo WA kawaida)
Elimu Hii pia ni kubwa.

iii) Elimu ya madini.
Kila unachokiona kinatokana na madini. Sisi wenyewe binadamu tunatokana na madini. Viumbe wote wanatokana na madini. Taaluma ya Uchawi husoma kozi hii Kwa sababu mbalimbali.
Uliwahi kuumwa Malaria au Ukimwi lakini ukifika Hospitalini haionekani? Kuna namna mbili za kumloga MTU. Kuna kumtupia Jinni au kiumbe cha Roho mwilini mwake kimdhuru Kwa kumpa ugonjwa kama Ukimwi. Pili kuna kumloga mtu Kwa kumpa madini Fulani ambayo yakiingia kwenye Damu yake, akipimwa haionekani kama anaugonjwa wowote.
Usijesema Hilo haliwezekaniki, linawezekana.
Vifaa vya kisayansi hasa vya kibinadamu vimejengwa Kwa Akili na vinatumia Madini na kemikali. Elewa kuwa kama vile kipimo cha Malaria kisivyoweza kupima Ukimwi Kutokana na jinsi kilivyotengenezwa, hivyohivyo Ipo sayansi na madini au kemikali ambayo MTU akipewa hata kama anaukimwi akipimwa Ukimwi hauonekani.
Elimu ya madini inasaidia kutibu na kuharibu kulingana na lengo la mchawi au mganga.

Tuishie hapa Kwa habari za hizo kozi.

Baada ya Mchawi kumaliza kusoma kozi z Uchawi itampasa Aende Field kupima kama amefuzu au vipi. Hapa ndio kasheshe lilipo.
Eneo la kazi, wakuwafanyia mafunzo yake ndio changamoto itakayokuwa Mbele yake.
Kikawaida Wachawi ambao wapo Field wengi huwaita Wanga. Ni hawa wanaorukaruka usiku, kwao ndio muda mzuri. Lakini pia hupenda kuwajaribu Watu wanyumbani kwao au wakaribu Kutokana na urahisi na kutokuwa na hatari ukilinganisha na kudili na MTU wa mbali.
Kumloga mtu unayemjua ni rahisi kuliko mtu usiyemjua.

Hawa huloga pasipo Nia Mbaya ya kuharibu isipokuwa wanafanya Kwa kujifunza. Hapa hujifunza kuingilia mipango ya Watu Kwa kuiharibu kisha wakifanikisha huweza kuiweka Sawa
Mfano, kuna Pesa ulikuwa unaitegemea uipate saa tano kamili. Wao wanaingilia huo Mpango wanaichelewesha Makusudically hapo watakuwa wanapambana na kinga yako, wakiona wamefanikiwa basi huachia, kisha unashangaa Ile Pesa inaingia jioni au kesho yake Kwa kuchelewa. Basi tuu ilimradi wapo mafunzoni.
Hii ni tofauti na Uchawi mwenye Nia ya kuharibu ambaye yeye huondoa kabisa uwezekano.

Wachawi ambao ni mawakala wa nguvu hasi hutumika kujaribu Imani za Watu. Lengo ni kuwafanya Watu wamtukane Aliyewaumba. Elewa kuwa aliyekuumba Hana sababu hata Moja ya kukujaribu. Kwani alikuumba na anakujua in and out. Sasa atawezaje kukujaribu?

WANAFUNZI wa kichawi sometimes huwa na bifu na Baadhi ya Watu Jambo ambalo hupelekea kujaribu taaluma zao kuona kama zinafanya kazi Kwa kiwango gani. Wanaseti mitambo kisha wanapiga. Wakiona Ipo sawa wanahiyari ya kuacha hivyohivyo au kukuweka Sawa.

Sio vizuri kusema mipango yako, Siri zako Kwa Watu. Iwe unawajua au usiowajua.
Ingawaje Imani za kichawi na kishirikina ni Imani za kijinga na hovyo lakini kamwe usizipuuzie ikiwa unaishi kwenye jamii inayoamini mambo hayo.
Ni vizuri kupuuzia Uchawi na ushirikina kwneye jamii ambayo haina mambo hayo. Hiyo ni Hekima. Lakini ni upumbavu kutokuchukua tahadhari Kwa mambo hayo ilhali unaishi kwenye jamii ambayo Kati ya Watu 10 basi 9 ni washirikina na wanaoamini waganga na wachawi.

Namna Bora ya kuepuka Wachawi, nguvu hasi, nguvu za Giza na mambo ya kishirikina na Kuishi Kwa kutenda Wema, kuishi Kwa kumuamini aliyekuumba hata kama haujawahi kumuona. Kuwa na Siri kama aliyekuumba alivyo na Siri alivyokuficha kesho yako, ndivyo unavyotakiwa kuficha mipango na melango yako Kwa Watu wengine.

Ni Yule Mtibeli. Jichawi la Kale.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Imani pekee ndio yenye athari, ila hizi nguvu zinaoitwa kwa jina la uchawi au nguvu za kichawi au ushirikina HAZIPO izo nguvu, wala watu wenye huo uwezo wa kichawi au nguvu za kishirikina HAWAPO.
 
Uchawi upo sema inaonekana nao una mipaka
FB_IMG_16865417268092634.jpg
 
Imani pekee ndio yenye athari, ila hizi nguvu zinaoitwa kwa jina la uchawi au nguvu za kichawi au ushirikina HAZIPO izo nguvu, wala watu wenye huo uwezo wa kichawi au nguvu za kishirikina HAWAPO.

Ukishasema Imani jua tayari umejiingiza kwenye aidha Imani ya Mungu(nguvu chanya) au Imani ya kishetani(nguvu hasi)
Wahusika wapo
 
Imani ya kishetani (nguvu hasi) SIO UCHAWI. shetani yupo, na uwezo wake wote ila sio uchawi au nguvu na uwezo tunaoita wa kichawi huo HAUPO. namaanisha yule shetani malaika muasi aliyefukuzwa mbinguni pamoja na vikosi kadhaa vya malaika, huyo sio mchawi au mkuu wa wachawi, huyo ni shetani.

Na izo nguvu hasi sio UCHAWI kama kupaa au kuruka sehemu moja mpaka nyingine au kudhuru watu kwa nguvu zisizo eleweka kama ulivoeleza nk.
 
Unaelewa nini maana ya Uchawi?
Kisha unaelewa nini kuhusu miujiza?

Nisijekuwa mnajadili na MTU asiyejua hata anachokitaja?
 
Hivi hao wachawi, wakiroga huwa wanapata pesa? Au wanafaidika vipi na huo uchawi? Tupe hiyo elimu kidogo.
 
Hivi tetesi na uzushi kama huu huwaga mnaziokotea wap?

😀😀
Hivi Mkuu Kwa uelewa wako, kwenye Hii Dunia unaweza ukazusha kitu chochote kwenye Akili yako ambacho hakipo, halijawahi kuwepo au hakitakuja kuwepo?
Kama kuna MTU mwenye uwezo huo basi jua huyo ni Mungu muumbaji.

Lolote litakalopita kwenye Akili yako hata kama huwezi kulithibitisha jua Lipo
 
Ndio unaweza kuzusha na mfano mzuri ni hiki ulicho kuandika hapa kwenye uzi wako . Ni uzushi mtupu na blah blah tu
 
Unajaribu kuniita mungu Kwa Lugha nyingine.
Huwezi zusha kitu ambacho hakipo, halijawahi kuwepo, na ambacho hakitakuja kuwepo bila ya kuwa wewe ni Mungu
 
Back
Top Bottom