Wanaosali Jumuiya vs wacheza pool table, kuna tofauti?

Kweli mtu huweza kudharaulika kwa maneno yako tu kutoka kwenye kinywa chako, hivi jamani ikapita siku bila kupost ishu humu jf vidole huwa vinawasha hadi mtu uandike ujinga wa hivi, yani imeonesha kiasi gani pooltable linavyokuuma tangu ukatazwe kulicheza,kiasi gani ni mvivu wa kufikiri, hizo dakika zote ulizotumia kuandika huu utumbo ungezitumia kuwaza jambo la maendeleo maana ishu za kuingilia imani ya mtu si jambo la maendeleo.
Polepole tu ndugu usijerudi hapa na hoja pia jumamosi na jumapili watu wasiende kwenye ibada wafanye kazi.
Viroba hivi jamani vijana tunaangamia.
Unamfananisha mcheza pool na mtu anae sali jumuiya.
 
Tatizo lako ni bangi unayovuta.Nimekuambia yanafanyika mengi ya msingi.
Wako wengi wasioweza kufika makanisani kuna vilema, wazee na watu wa aina mbalimbali wanaotaka huduma ya Kanisa na wanashindwa kuifikia kwa sababu nilizozitaja hapo juu hivyo uwepo wa jumuiya unawatimizia mahitaji yao ya kiimani.
Ndio iwe kila week-end?Mkiwaombea mkiwa makanisani mungu hatasikia sala zenu?Ni vilema wangapi mnawapita barabarani pasipo kuwasaidia?
 
Ndio iwe kila week-end?Mkiwaombea mkiwa makanisani mungu hatasikia sala zenu?Ni vilema wangapi mnawapita barabarani pasipo kuwasaidia?
Kufanya tufanye sisi wewe unapungua wapi?
Endelea na upagani wako huko tuache na jumuiya zetu hazikuhusu wala hazikupunguzii chochote.
 
Ndio iwe kila week-end?Mkiwaombea mkiwa makanisani mungu hatasikia sala zenu?Ni vilema wangapi mnawapita barabarani pasipo kuwasaidia?
Maandiko yanasema kesheni mkiomba maana hamjui siku wala saa atakayo rudi mwana wa Adam, sasa wewe unataka uwapangie watu siku na muda wa kuabudu.
Hivi wewe ndugu ni mzima kweli, imani yako ni mfu, na wewe ndie wale mnao hudhurua ibada na hizo jumuiya kama sehem tu ya utaratibu lkn humaanishi.
 
Wanafiki wakubwa nyie na ndio mnaoogoza kwa uzinzi na uasherati.Mnajidai kuheshimu imani zenu wakati matendo yenu bora hata ya mpagani.

Nasisitiza hizi Jumuiya za kila Week-end kuzunguka kwa mtu mmoja mmoja na kuchangishana ni miradi tu ya kukusanya pesa huku watu wakilazimizhwa kushiriki hizi Jumuiya.

Wengi wanashiriki kwa kulazimika tu kutokana na mashariti mlioweka ambayo hata kwenye Biblia hayapo.

Fanyeni kazi na si kukutana huko kwa mara kwa mara kwa ajili ya Jumuiya hizo kuliko pitiliza.

Jumuiya hazitawafikisha mbinguni.

Toomuch of everything is harmful!
Kubaki kimya nayo ni busara ndugu! Naona kama uunazidi kuharibikiwa!
 
Maandiko yanasema kesheni mkiomba maana hamjui siku wala saa atakayo rudi mwana wa Adam, sasa wewe unataka uwapangie watu siku na muda wa kuabudu.
Hivi wewe ndugu ni mzima kweli, imani yako ni mfu, na wewe ndie wale mnao hudhurua ibada na hizo jumuiya kama sehem tu ya utaratibu lkn humaanishi.
Kitakachotuhukumu ni matendo yetu na wala si kukesha kwenye maombi na makanisani.Unaweza kukesha kanisani na kwenye maombi lakini ukirudi nyumbani wewe ni mchawi, mzinzi, muongo, mfitini,mwizi,mchonganishi n.k.
 
dah pole,, eb jifikirie upya
Pamoja na kushiriki hizo jumuiya,niambie ni kwa kiwango gani unaheshimu "amri kumi za mungu"?

Je,ukitenda dhambi huwa unajutia dhambi zako au unasubiri Jumapili ijayo ukatubu na Jumatatu yake unaendelea na dhambi ile ile huku ukisubiri Jumapili nyingine ukatubu?

Tunaishi kwa neema ya mungu lakini wengi wetu dini imetushinda tumebaki na imani tu vichwani mwetu imani ambayo hatuiheshimu kivitendo bali kinadharia tu.
 
Mikutano ya mitaa/vijiji hamshiriki ila Jumuiya ndio muhimu zaidi huku kila siku tukilia umasikini.Tutafika?Kwanini hizi Jumuiya zisifanywe kimtaa wala mara moja kwa wiki kuliko kuzunguka nyumba hadi nyumba kila week-end?Tujali muda.
Kwani we umelazimishwa kusali au zinakuuma nini??
 
Kitakachotuhukumu ni matendo yetu na wala si kukesha kwenye maombi na makanisani.Unaweza kukesha kanisani na kwenye maombi lakini ukirudi nyumbani wewe ni mchawi, mzinzi, muongo, mfitini,mwizi,mchonganishi n.k.

Matendo pasipo imani ni sawa na kazi bure ndugu nazidi kuamni kuwa wewe si muumini wa kweli bali ni mshiriki tu.
Muombe sana Mungu wako akutoe kwenye hicho kifungo, kunamtu humu amekufananisha na mpagani na mm naungna nae mkono.
 
we Salary Slip kitu ambacho hujajua nikuwa :

jumuia inamalengo makuu ya kujuana majiran mnaosali pamoja na inapaswa iwe si zaid ya yumba kumi na tano!

je? kuna ubaya gani kusali kwa kutembelea kila nyumba!? naona umeishupalia sana!! vipi huna makochi sebleni au? usoiogope wanakuja na viti vyao mkuu!!
 
Kama wanafanya kila weekend tena jjioni kuna tatizo gani? na hao wanajumuiya utakuta ni watu na kazi zao wameshaajiriwa serikali ametoka kazini saa 8 au 9 kuna tatizo baada ya hapo akifanya maswala yake binafsi kama ya kiroho au kijamii? subiri wakifanya hiyo saa 3 asubuh mpaka saa 6 j3 mpaka ijumaa ndo tutaangalia tuwasaidie vipi hizo jumuiiya ziwe za kuswali na baada ya hapo kuanzisha miradi ya jumuiya wajikwamue bila ya hivyo wana haki ya kufanya chochote, tena ni bora hao wako na mungu kuliko hao wa pool wako na shetani, na kupanga deal za kishetani ambazo zote zina madhara kwa jamii, halafu nikuulize kitu hivi hiyo mikutano unayosema ya mitaa huwa inafanywa? hao wenyeviti hasa wa dar labda kama kuamka ni sasa ila wengi wamelala fofofo sijui kuhusu vijijini.
 
Ndugu mtoa post KUSALI ni muda wa saa moja hadi mawili ila KUCHEZA POOL ni siku nzima halafu hii ni kamari
 
"Omba vyote kwenye hii dunia, lakini usiombe kuwa na ubongo wa Mende kama mtoa mada"
Omba vyote kwenye hii dunia lakini usiombe kuwa mnafiki kama msali jumuiya asiempenda hata jirani yake na tena akimkisema vibaya pembeni.
 
Mkuu Salary Slip umemshika ta*ko mama mkwe kazi nayo. Tatizo watu hawapendi kuambiwa ukweli.

Mi siongezi, acha wakushambulie.
 
Matusi makubwa kulinganisha wacheza pool na jumuiya.
Wanajuiya wanasali muda usiozidi saa mbili ili baadaye waendelee na shughuli zao.
Nadhani una chuki na dini ya wanajumuiya.
 
Huo muda wa kila-week end kukutana nyumbani kwa mtu ni bora tungetenga na muda wa aina hiyo tukutane katika mitaa yetu kwa shughuli za kiuchumi au kupanga mipango ya kimaendeleo katika mitaa yetu.


mkuu kama wewe ni mkatoliki kweli hayo maneno ungeyasema kwenye jumuiya yako ili mpange utarAtibu muafaka, ila naamini umetumwa tu na wale wapinga kristo, kila la heri huko uendako
 
Back
Top Bottom