Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Umeninukuu ndivyo sivyo ndugu, hamna sehemu nimeandika hivyo - japo huo ufahamu uliopata nimeshajua umeupata kwenye maelezo gani, sehemu nilipoandika neno 'haya' ndipo nilipokuwa nimeandika neno 'sana' zaidi ya mara mbili kwa kukazia, naamini unafahamu maana ya neno sana, maana niliyokusudia pale ni matumizi ya akili ya kuyakinisha yaliyotufikia kuchunga mipaka na nidhamu za kuhoji, ama kwenye maelezo ya chini yake nilipoandika masaili mengi - nilikusudia si jambo moja tu, ni zaidi ya moja ambayo hayapimwi kwa akili, hivyo yaweza kuwa mawili au manne au nane nakadhalika, suala la matumizi ya akili kwenye kila kitu kilichotufikia katika dini halipo kwa waislamu tu - ni moja ya misingi midogo ya nidhamu inayopatikana kwenye imani nyingi sana, kwa nini tahadhari zimewekwa? sababu wanadamu wengi ni wajinga - 85% na wana imani haba, akili finyu na maarifa madogo - wanapodadisi kwa kupindukia kuhusu jambo fulani la kiroho na utashi wao usipokinai inaweza kuwafanya wakakengeuka

Unafahamu maana ya neno imani? naamini unafahamu - japo sina hakika kama tuna ufahamu mmoja na uliosahihi, hoja ngapi zenye nguvu za uwepo wa MUNGU umewahi kuwasilishiwa na hazijakushawishi? uongofu hauji kwa hoja peke yake tu, ingekuwa ni hivyo basi watu wote walioamiliana na kuwadiriki manabii na mitume na hali wana akili timamu wangeshawishika na kuwafuata, mbona hilo halikuwa? unafahamu kwamba utashi aliojaaliwa mwanadamu na lugha zake: vyote havitoshi kueleza sifa na ukubwa wa MUNGU kwa mapana, kwa kina na kwa usahihi 100%? bila shaka unafahamu hali za watu nchini INDIA kwa misingi ya imani zao, na bila shaka unafahamu IQs na upeo mkubwa wa kupambanua mambo waliojaaliwa wahindi katika fani mbalimbali, na naamini bila shaka kwamba wengi wao wamekuzidi kwa mambo hayo makuu ambayo unaona ni silaha kubwa sana, je si haohao waliokuzidi hivyo vitu na wanazitumia akili zao kuabudu ng'ombe kana kwamba ndiyo miungu? je si haohao waliokuzidi wewe upeo wanaotumia akili zao kuabudu mawe na vinginevyo? si kila mwenye macho anaona ndugu, na si kila mwenye masikio anasikia, hivyo ndivyo mambo yalivyo, suala la kukubali linategemea na mtu, si kila moyo upo wazi na huru kupokea kweli au haki inapowasilishwa, baadhi ya mioyo imefungwa - imejikita kupinga tu, rejea juu pale kwenye maelezo yangu: haijalishi ni nini kinajadiliwa na zimesimikwa hoja zenye nguvu kubwa kuwahi kuibuka katikz historia ya wanadamu - fahamu kwamba kamwe wanadamu wote ulimwenguni hatuwezi kuwa kwenye ukurasa mmoja wa ufahamu

Si kwamba haipaswi kuuliza kwa maana hayo maswali hayana majibu - hapana, na si kwamba haipaswi kuuliza - hapana, kilichotahadharishwa ni kukithirikisha zaidi katika kufanya hilo, neno sana kwenye maelezo yangu nililitumia sehemu nyingi sana, hali inayopendeza ni kuuliza au kutafakari jambo kwa wastani 'kati na kati' na si hadi kuchupa mipaka, ngoja nikupe mfano hai: ni nchi ngapi ulimwenguni zinajinadi zinawapa wananchi wake uhuru wa kuongea? je ndivyo ilivyo? unaruhusiwa kujiongelea chochote tu pasina kuchunga matumizi ya lugha na kuchunga baadhi ya ajenda? je kukiuka kufanya hivyo hakutakugharimu kwa namna yoyote? hamna aliyekuwekea kizuizi kwenye kuuliza, kuuliza unaweza kuuliza tu, kilichowekewa tahadhari ni kuzidisha sana katika kuuliza kiasi cha kumfanya mtu kwa upeo wake mdogo atilie shaka anachokiamini - kwenye ulimwengu wa kiroho hii ni moja ya kazi za shetani, unapata picha gani unapojenga fikra za maisha ya wanadamu yasiyokuwa na sheria, kanuni na taratibu? hamna jambo lililoshushwa kisha likaachwa hivyohivyo pasina kuwekewa ABC

Suala la kukubali au kutokukubali hoja na dalili unazopewa hakufanyi suala husika kuwa ni la kweli au si la kweli, wangapi wameupokea upotofu kwa utashi wao wakiamini na kuitakidi kwamba ni kweli na haki na hali ni kinyume chake? jaalia umeshuhudia mtu akitembea juu ya maji ya bahari na ukaenda kunsimulia rafiki zako, je watakusadikisha? au hawatakusadikisha kwa hoja za UPTHRUST? je huku kukubali au kutokubali kwao kunafanya ulichokiona kuwa ni haki au si haki? nisaidie na hili: hivi wana mazingaombwe wanapompasua mtu na kumtoa kirungu tumboni huwa ni kweli au si kweli? ni jambo nililolishuhudia kwa macho yangu zaidi ya mara moja, hapo ndo utajua siyo kila ndiyo ina ndiyo kiundani na kuna baadhi ya ndiyo zimeambatana na siyo, na hiyo ni mifano michache tu, unazijui aina za logical reasoning?

Shabaha kuu ilikuwa ni kukutumia vitabu tu - hayo mengine yalikuwa ni ziada fupi
Kwanini uweke mipaka kwa baadhi ya maswali?
 
Kijana siyo muelewa kabisa. Wewe ulikuja kuchukua swali ambalo aliuliza Kiranga unakumbula hilo ?

Mimi nilimjibu vipi Kiranga ? Baada ya hapo kuna post nilianza kuuliza maswali ulijibu swali gani katila ile post ?

Kupuuza, ni baada ya wewe kuendelea kuuliza maswali ya kijinga baada ya wewe kujibiwa. Hujaelewa wapi hapo ?
We umesema kuwa aliyeanza kumuuliza maswali mwenzie kati ya mimi nawewe ni wewe

Umeleta post uliyo m-quote kiranga kwa madai kuwa ndio uliyoaanza kuniuliza mimi maswali na bado unataka tukuone sio mzushi?
 
Sasa unanikumbusha vipi kwa jambo halihusiani na tunachojadili hapa ? Maana yake hata si kwa aina ya hoja. Shida yako ni pale unapo jiona umeelewa jambo wakati hujaelewa. Kama umekiri hakiuhuisiani maana yake si aina ya hoja unayo ikusudia hapa.

Sasa nikiri vipi kwa jambo la uongo ? Hili ukitaka kuwa mjadala utajadili wewe mwenyewe, siwezi kupoteza muda wangu kujadili ujinga kijana.

Hapa kuhusu hili nimemaliza.
Halihusiani na mada kuu ila lina mahusiano na hoja uliyoitumia dhidi ya mdau na ndio maana nimekuonesha hapo ili nikukumbushe kuwa hoja ya namna hiyo ilikufanya ukimbie

Kwani mara ngapi hapa nimekuwa nikisema mwenye madai ya kitu kipo ndio mwenye wajibu wa kuthibitisha kitu hicho kipo?

Sitaki hili liwe mjadala nimeliweka kama kumbushio tu probably utajifunza kuwa maswali ya namna hiyo hayajibiki kwasababu hata wewe yalishawahi kukushinda
 
Jibu maswali niliyo kuuliza, naona unaendelea kurudia jambo ambalo nomeshatoa ufafanuzi zamani sana.
Wewe ndio uliyeleta hii mada na wewe ndio mwenye jukumu la kutoa ufafanuzi

Vitu vilivyo nje ya uwezo wa binadamu ni vitu gani?
 
Kwanini uweke mipaka kwa baadhi ya maswali?
SCARS e, mimi ni nani wa kuweka mipaka kwenye hayo mambo aisee? Unamaanisha kwenye maelezo yangu umebainikiwa na ushiriki wangu kwenye hiyo issue? Unajua swali lako ni sawa na kuuliza: kwa nini uweke mipaka kwenye maisha yetu baada ya kutuumba? Hayo maswali anayetakiwa kujibu ni CREATOR na si mimi ndugu, mimi nimewasilisha ufahamu tu wa yale yaliyofunuliwa kwenye maandiko matakatifu, sijaweka mimi hiyo mipaka

Si kwamba mipaka imewekwa kwenye kuuliza maswali - hapana ndugu, naomba kuwa makini kwenye kusoma maelezo yangu tafadhali, nilichoandika juu ni hichi: mipaka imewekwa kwenye kuzidisha na kuzidisha kuuliza maswali kulikopindukia 'baadhi ya maswali', mbona kwenye maelezo yangu vivumishi natumia sana, nimeviandika kwa wingi sana lakini cha ajabu unakuwa kana kwamba huvioni au haufahamu vina maana gani kwenye maelezo, si sawa


Si kwamba nakupangia kuuliza au cha kuniuliza - hapana, lakini kwa jinsi nilivyokuwa nimeandika kwenye post zilizopita kwa aliyenielewa kwa 100% naamini angeniuliza swali lifuatalo - kwa nini imewekwa mipaka kwenye 'kukithirisha' kuuliza maswali 'mengi' kwenye baadhi ya mambo? Jibu langu lingekuwa - tafadhali rejea post iliyopita: majibu yake niliyagusia kwenye maelezo, na si hivyo ulivyoniuliza, hamna sehemu nimeandika 'watu wamezuiwa kuuliza baadhi ya maswali' pasina kugongelea vivumishi vya kutosha, naomba nieleweke tafadhali japo si lazima
 
We umesema kuwa aliyeanza kumuuliza maswali mwenzie kati ya mimi nawewe ni wewe

Umeleta post uliyo m-quote kiranga kwa madai kuwa ndio uliyoaanza kuniuliza mimi maswali na bado unataka tukuone sio mzushi?
Poa.
 
We umesema kuwa aliyeanza kumuuliza maswali mwenzie kati ya mimi nawewe ni wewe

Umeleta post uliyo m-quote kiranga kwa madai kuwa ndio uliyoaanza kuniuliza mimi maswali na bado unataka tukuone sio mzushi?
Poa.
 
Na hii ndio maana ya ukaidi.

Wanaipinga Quran kwa sababu wanasema haijatoka kwa mungu, lakini hata kama inatoka kwa mungu ndio tayari wameshaipinga.
Mbona simple Tu...si uthibitishe kuwe hiyo Quran imetoka Kwa mungu
 
daah mkuu kwa hoja nilizokupa hapo juu na wew umeshndwa kukosoa lakn bdo unabisha bas wew hautakuja kukubal mpaka UONYESHWE NDIO HUYU HAPA EB MSHIKE MKONO nahisi hapo ndio utakubali kama kweli M/MUNGU yupo
 
SCARS e, mimi ni nani wa kuweka mipaka kwenye hayo mambo aisee? Unamaanisha kwenye maelezo yangu umebainikiwa na ushiriki wangu kwenye hiyo issue? Unajua swali lako ni sawa na kuuliza: kwa nini uweke mipaka kwenye maisha yetu baada ya kutuumba? Hayo maswali anayetakiwa kujibu ni CREATOR na si mimi ndugu, mimi nimewasilisha tu yale yaliyofunuliwa kwenye maandiko matakatifu

Si kwamba mipaka imewekwa kwenye kuuliza maswali - hapana ndugu, naomba kuwa makini kwenye kusoma maelezo yangu tafadhali, nilichoandika juu ni hichi: mipaka imewekwa kwenye kuzidisha na kuzidisha kuuliza maswali kulikopindukia 'baadhi ya maswali', mbona kwenye maelezo yangu vivumishi natumia sana, nimeviandika kwa wingi sana lakini cha ajabu unakuwa kana kwamba huvioni au haufahamu vina maana gani kwenye maelezo, si sawa


Si kwamba nakupangia kuuliza au cha kuniuliza - hapana, lakini kwa jinsi nilivyokuwa nimeandika kwenye post zilizopita kwa aliyenielewa kwa 100% naamini angeniuliza swali lifuatalo - kwa nini imewekwa mipaka kwenye 'kukithirisha' kuuliza maswali 'mengi' kwenye baadhi ya mambo? Jibu langu lingekuwa - tafadhali rejea post iliyopita: majibu yake niliyagusia kwenye maelezo, na si hivyo ulivyoniuliza, hamna sehemu nimeandika 'watu wamezuiwa kuuliza baadhi ya maswali' pasina kugongelea vivumishi vya kutosha, naomba nieleweke tafadhali japo si lazima
kufanya maelezo marefu yawe mafupi naomba unithibitishie Mungu yupo
 
Mtiririko wako una hitilafu kubwa sana. Hitilafu ya lazima chanzo cha kwanza cha ulimwengu kiwe mungu. Kwanini ulazimishe umungu kwenye kila hali? Hakuna hali ya kwamba mungu akakosekana? Anayesema hydrogen atoms mungu wake hizo atoms. Atakayekuja kusema strings utasema mungu wake ni strings? Au weak force? Quantum dynamics? Undefined probabilities?

1. Uchawi ni nn? Uchawi unafanyikaje? Unaathiri vipi vitu na watu? Kiimani na kisaikolojia au ina athari za kihalisia? Wewe ndio wale wanaodhani ukiomba kabla ya kuanza safari au mtihani utafika salama au kufaulu? Unadhani mtu akikuendea kwa mganga ufilisike utafilisika kweli bila wewe kusababisha au sababu ingne isiyohusiana na uganga uliofanywa? Nawe ni mmoja wao? Kama ni hivyo pole sana mkuu.

Lakini tuendelee. Ukielewa na kufata taratibu za kitafiti na uchunguzi utagundua hakuna uchawi, wala bahati, wala mkosi, wala miujiza wala viumbe visivyofata sheria asilia. Hakuna anayepaa tu hivihivi. Hakuna anayepona ghafla bila uhalisia wa kibaiolojia. Hakuna anayekufa pasipo sababu za msingi. Hakuna anayedhuriwa kichawi au kwa nguvu zisizopimika. Kila kitu duniani lazima kifate sheria asilia. Hakuna njia ya mkato. Uchawi haupo. Upo kichwani mwako tu. Hakuna haja ya kuongelea sana hili liko wazi sana kwa wenye kufatilia kiundani mambo ya kwenye jamii zetu.

2. Mungu ni nini au nani? Kwa maana za kibinadamu za kawaida hakuna ushahidi wa uwepo wake. Mungu ana ufahamu? Kama ndio basi atoms haziwezi kuwa miungu. Hazina ufahamu wowote. Kama mungu hana ufahamu basi pengine atoms kweli(unajua kuna vipengele ndani vinavyoathiri na vidogo zaidi ya atoms?) ndio miungu yetu. Miungu hii haihitaji imani za kuombwaombwa au kujengewa mahekalu, kutengewa muda na siku fulani na taratibu fulani ili ziridhike kututimizia mambo yetu hapa duniani. Sadaka zetu zitasaidia nn atoms? Ibada zinakuwa hazina maana. Dini zitatakiwa kutoweka kwenyw jamii watakaoelewa miungu hii. Hoja yako ya atoms ni miungu inafaa kupuuzwa mara moja.

Kuna wanasanyansi wana hoja zao kwamba kama uwepo wa kitu mungu unawezekana basi sio mungu aliyehai na kuwepo kila saa na sehemu. Kuna jina wanapenda kulitumia kuongelea hili kundi la imani; Deism. Yaan madai ya hii ni yawezekana alitenga mafiga matatu akainjika chungu akasepa. Kwahiyo mkono wa mungu kwenye dunia hii wala ulimwengu kiujumla. Hayupo tena alishaondoka akatusahau yapata bilioni kadhaa ya miaka. Hapa hakuna mambo ya miujiza, maono, uchawi sijui mapepo, mikosi, bahati, nyota yako sijui na takataka zingine.

Mimi binafsi, kama walivyo wanasayansi na wasio wengi, nasema ulimwengu ulianza bila ya uwepo wa mungu. Kuweka hoja kwamba alianzisha au yupo siyo suluhisho. Bali ni kuongeza tatizo jipya kwenye mtiririko wa suala hili la chanzo cha ulimwengu. Sana sana unaongeza maswali zaidi. Alitoka wap? Ametengenezwaje(hakuna kisichokuwa na mwanzo wa hivihivi tu. Kama ulimwengu lazima uliumbwa basi hata huyo muumbaji wake aliumbwa. Tusizushe umaalumu kama kinga ya hoja)‽ Kwann aanzishe?(Jibu liwe la maana sio ili "aabudiwe" utaanzisha kingine kwann aabudiwe? Bila kuabudiwa hajatimia?) Kwann alilipua muda husika? Alilipuaje? Alikuwa na lengo la kufikia hapa tulipo sasa?

Ukikaa peke yako na imani zako jitathmini sana na mwisho ujikubali kwamba unaamini lakini hujui unachokiamini hata ukisoma likitabu gani la imani haisaidii!
Yote uliyoongea hayana mashiko.Eti uchawi haupo,mimi nilishawahi kumuona mchawi akiwa katika kazi zake.

Bado utarudi pale pale tu nikikuuliza hiyo big bang theory ilisababishwa na nini na hizo atoms zilitokeaje?
 
Nasubiri uthibitishe ya kuwa Allah hayupo.
Huelewi hata falsafa za uthibitisho.

Asiyepo, hathibitishiki kwamba hayupo.

Kwa sababu hayupo na uthibitisho unakwenda sana kuonesha vilivyopo.

Ila, naweza kukuthibitishia Allah hayupo kwa "proof by contradiction".

Kama vile ninavyoweza kukuthibitishia kwamba hakuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika Euclidean geometry.

Mungu wako, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anakuwa contradicted na dunia tunayoiona inayoruhusu mabaya kuwepo.

Mungu huyo angekuwepo, logically kusingewezekana kuwepo na mabaya yoyote.

Na mabaya tunayaona yapo.

Hilo linathibitisha Mungu wako hayupo.

Ni hadithi za watu tu.

Kukubali uwepo wa Mungu huyu, ni sawa na kukubali kwamba kuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika planes za Euclidean geometry
 
u
Mungu mjuzi wa yote ambaye anaweza kujua yaliyo mbele ya wakati kabla hayajatokea hana sababu ya kutoa adhabu

Mungu kaona mtu huyu ataenda kuua mtoto asiyekuwa na hatia

Na wakati huo ana uwezo wa kudhibiti tukio hilo lisifanyike

Na anasababu ya yeye kudhibiti kwasababu kwanza hilo tukio halimpendezi lakini ni mwenye upendo wote

Ukisema kwamba Mungu kamuacha mtu huyo aue mtoto asiye na hatia ili kuonesha amempa mtu freewill ya kufanya atakalo.

Kutakuwa kuna mambo mawili
  1. Mtoto aliyeuliwa ametumia vipi freewill ya kuamua kuuliwa au kuto kuuliwa?
  2. Upendo wote wa Mungu uko wapi kama hadi mtoto mdogo asiye na hatia yanamfika mabaya na yeye anaacha yafanyike bila kuzuia?
Honestly kwa jinsi ulivyomtetea Mungu umemfanya muuaji wa mtoto asiwe na hatia na mwenye hatia awe ni Mungu

************
Mfano wako wa mzazi kum-refer na Mungu ni irrelevant

Kwasababu mzazi hana uwezo wote wa kumfanya mtoto aishi katika njia ya kumpendeza yeye.

Na ndio maana anakuwa mkali pale anapoona mtoto hafanyi kila anachokitaka yeye, huyu mzazi hana namna nyingine ya kumfanya mtoto aishi katika misingi ambayo anaitaka yeye bila mafunzo ambayo nayo sio effeciency na ndio maana hufikia hatua ya kumuadhibu kwasababu hana mbadala

***********
Umesema Mungu alishajua yote kabla hayajatokea lakini anaendelea kuwa onya msifanye vitu fulani, anatuma mitume ili msifanye vitu fulani shortly he still expecting something new to his creatures

Yani anaelewa utaua mtoto asiye na hatia, na kuelewa kwake lazima kutimie kwa asilimia zote

Lakini bado anakuonya kuwa usiue

Je mtu huyo anauchaguzi wa kusikia onyo hilo na kuamua kutoua?

Hiyo ndio Logical fallacy ambayo lazima utaiangukia kipindi unamtetea Mungu kwa kujaribu kui solve problem of evil

*****************
Umesema freewill lazima ihusishe mabaya bila mabaya hakuna freewill

Kwamba una maanisha Mungu hausiki na mabaya bali mabaya yanatokana na uchaguzi wa watu kupitia freewill waliyopewa?

Kama watu hufanya kile ambacho Mungu kawaumba waweze kufanya kwanini waadhibiwe kwa hicho ambacho Mungu kawaumba waweze kufanya?

Kama Mungu aliweza kujua kuwa hiki kijusi kitazaliwa nakuwa mtoto, kitakuwa, na kuwa muuaji mkubwa na Mungu akaendelea kukiruhusu kiendelee kuishi tumboni na kuki support hadi katika hatua za kuazaliwa mpaka kikue kufikia utu uzima, kisha mtu huyo aanze utekelezaji wa hayo mauaji.

Sasa kwanini tena mtu huyo aadhibiwe kwa kile aambacho Mungu alimuumba aje akifanye?

Kama huo ulikuwa ni uchaguzi wa mtu kuua je hiyo haikuwa uchaguzi wa Mungu kuumba kiumbe chenye kuchagua uovu?

Ngoja nikupe mfano

Mimi ni mfanya biashara ninaye endesha maduka mawili katika eneo moja hapa mjini. Duka langu moja linajihusisha na uuzaji wa silaha na lingine linajihusisha na maswala ya kimichezo

Kwa bahati nikatembelewa na mtu wangu naye mjua anaitwa Calvin, Calvin akataka kununua silaha nzito ila akanieleza kuwa anachukizwa na hao mabinti waliopo kwenye duka langu la michezo na kwa hivyo basi anaenda kuwafundish adabu

Calvin akaniomba nimuuzie package ya risasi kwa ajili ya silaha, nikamuuzia

Calvin akasema anaenda kuua watu wote waliopo katika eneo hilo, nikamuambia usifanye hivyo. Nikamuambia ni jambo baya sana hutakiwi kufanya

Calvin akaniambia nimfundishe namna ya ku shoot silaha, nikamfundisha

Nikamuonya tena kuwa hupaswi kwenda kutumia hii silaha ku shoot watu

Calvin akatoka na slaha na kwenda kuua kila mtu aliyekuwepo kwenye lile duka linalo jihusisha na michezo

Polisi walivyokuwa wakinihoji nikawasimulia stori nzima ilivyokuwa na nikiwaambia kuwa sio kosa langu ila ni Calvin alikuwa na freewill na nilimuonya asifanye hivyo.

Watu wengi wangeniwajibisha kwa ku-base tu kwenye yale yaliyokuwa sawa kufikiri kwamba Calvin angefanya kutokana na yale ambayo Calvin aliyosema kabla ya kuondoka kwenye duka langu.

Kama nawajibika kwenye sehemu ya mauaji, vipi kuhusiana na Mungu ambaye alimpa Calvin maisha akijua kwa hakika nini Calvin ataenda kufanya kwenye hayo maisha?

Mimi nilijua kidogo tu nini Calvin angeenda kufanya kupitia silaha niliyomuuzia

Mungu alijua kwa hakika na anaweza kuzuia chochote. Au vinginevyo Mungu hakujua, au Mungu hana uwezo wote
Umecopy wapi hii?? make hata hujui kutetea hoja zako mwenyeweeee!! ndo tatizo hili linawasumbua wengi humu
 
Yote uliyoongea hayana mashiko.Eti uchawi haupo,mimi nilishawahi kumuona mchawi akiwa katika kazi zake.

Bado utarudi pale pale tu nikikuuliza hiyo big bang theory ilisababishwa na nini na hizo atoms zilitokeaje?
Hata mimi nishawaona sana tu, na nishapiga sana mateke nazi zao njiapanda. Uchawi ni matokeo ya uwezo katika kuchanganua changamoto tunazokutana nazo na kutoka na jibu sahihi. Kama uchawi ungekuwa unafanya kazi dunia isingekuwa sehemu salama ya kuishi, kwasab ukinizingua kidogo tu nishakuroga unakua chizi au kukuua kabisa
 
Hata mimi nishawaona sana tu, na nishapiga sana mateke nazi zao njiapanda. Uchawi ni matokeo ya uwezo katika kuchanganua changamoto tunazokutana nazo na kutoka na jibu sahihi. Kama uchawi ungekuwa unafanya kazi dunia isingekuwa sehemu salama ya kuishi, kwasab ukinizingua kidogo tu nishakuroga unakua chizi au kukuua kabisa
Jua tu kuwa wewe hurogeki ni sawa wala hakuna shida.........kwa kuwa Shetani hakutaki Na kwa Mungu pua haupo!!...mara nyingi nyie hamna roho!! Hata Yesu akija hawatambui!! ...saaana mtakimbilia kwa shetani lkn hata wapa vyeo!!

Nyie mtakuwa askari wake wa kawaida tu! yaani makuruta wa kuzimu! hata ukifia kazini huzikwi kwa heshima....Lengo letu sisi wachawi ni wateule wa team Shetani V/V Mungu team!! Baaasi!.......jua kuwa Mungu aliumba viumbe vyote! ikiwa ni pamoja na hao Neutral!

Yaani weye hata ukimuona mchawi mpige tu hakufanyii kitu! hakurogi wala kuku kemea!! ni sawa na mtoto wa jirani yako maskini akifanya jambo Baya wala humkemei!! hata kwanza utajifanya humjui...lkn jirani yako akiwa tajiri utakemea kwa saaana!
 
Back
Top Bottom