Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Mungu yupo kwa sababu;
1.Katika maisha yangu nimeshaona wachawi .Wachawi wanafanya uovu hivyo lazima wamtumikie anayewatuma(shetani) hence logically wapo watenda mema wanaomtumikia Mungu.
2.Hakuna asiyeamini Mungu.Wale believers wa big bang theory Mungu wao ni hydrogen atoms zilizofanya collision na kuunda galaxy.Katika dini Mungu anaweza kuongea n.k.Hivyo chagua Mungu wako ni yupi either hydrogen atoms zilizokuwepo as supernatural or Mungu wa kwenye dini.

NB to atheists:mnasema hakuna Mungu,basi elezea chanzo cha dunia.Kama ni big bang theory,nani aliumba hydrogen atoms.Kama hydrogen atoms hazikuumbwa hence zilikuwepo supernaturally basi hydrogen atoms ndiyo Mungu wenu.
All scientific pioneers who tried to find origin of universe never disbelieved in God.
#Albert Einstein
#Edwin Hubble
#Stephen Hawking n.k
Mtiririko wako una hitilafu kubwa sana. Hitilafu ya lazima chanzo cha kwanza cha ulimwengu kiwe mungu. Kwanini ulazimishe umungu kwenye kila hali? Hakuna hali ya kwamba mungu akakosekana? Anayesema hydrogen atoms mungu wake hizo atoms. Atakayekuja kusema strings utasema mungu wake ni strings? Au weak force? Quantum dynamics? Undefined probabilities?

1. Uchawi ni nn? Uchawi unafanyikaje? Unaathiri vipi vitu na watu? Kiimani na kisaikolojia au ina athari za kihalisia? Wewe ndio wale wanaodhani ukiomba kabla ya kuanza safari au mtihani utafika salama au kufaulu? Unadhani mtu akikuendea kwa mganga ufilisike utafilisika kweli bila wewe kusababisha au sababu ingne isiyohusiana na uganga uliofanywa? Nawe ni mmoja wao? Kama ni hivyo pole sana mkuu.

Lakini tuendelee. Ukielewa na kufata taratibu za kitafiti na uchunguzi utagundua hakuna uchawi, wala bahati, wala mkosi, wala miujiza wala viumbe visivyofata sheria asilia. Hakuna anayepaa tu hivihivi. Hakuna anayepona ghafla bila uhalisia wa kibaiolojia. Hakuna anayekufa pasipo sababu za msingi. Hakuna anayedhuriwa kichawi au kwa nguvu zisizopimika. Kila kitu duniani lazima kifate sheria asilia. Hakuna njia ya mkato. Uchawi haupo. Upo kichwani mwako tu. Hakuna haja ya kuongelea sana hili liko wazi sana kwa wenye kufatilia kiundani mambo ya kwenye jamii zetu.

2. Mungu ni nini au nani? Kwa maana za kibinadamu za kawaida hakuna ushahidi wa uwepo wake. Mungu ana ufahamu? Kama ndio basi atoms haziwezi kuwa miungu. Hazina ufahamu wowote. Kama mungu hana ufahamu basi pengine atoms kweli(unajua kuna vipengele ndani vinavyoathiri na vidogo zaidi ya atoms?) ndio miungu yetu. Miungu hii haihitaji imani za kuombwaombwa au kujengewa mahekalu, kutengewa muda na siku fulani na taratibu fulani ili ziridhike kututimizia mambo yetu hapa duniani. Sadaka zetu zitasaidia nn atoms? Ibada zinakuwa hazina maana. Dini zitatakiwa kutoweka kwenyw jamii watakaoelewa miungu hii. Hoja yako ya atoms ni miungu inafaa kupuuzwa mara moja.

Kuna wanasanyansi wana hoja zao kwamba kama uwepo wa kitu mungu unawezekana basi sio mungu aliyehai na kuwepo kila saa na sehemu. Kuna jina wanapenda kulitumia kuongelea hili kundi la imani; Deism. Yaan madai ya hii ni yawezekana alitenga mafiga matatu akainjika chungu akasepa. Kwahiyo mkono wa mungu kwenye dunia hii wala ulimwengu kiujumla. Hayupo tena alishaondoka akatusahau yapata bilioni kadhaa ya miaka. Hapa hakuna mambo ya miujiza, maono, uchawi sijui mapepo, mikosi, bahati, nyota yako sijui na takataka zingine.

Mimi binafsi, kama walivyo wanasayansi na wasio wengi, nasema ulimwengu ulianza bila ya uwepo wa mungu. Kuweka hoja kwamba alianzisha au yupo siyo suluhisho. Bali ni kuongeza tatizo jipya kwenye mtiririko wa suala hili la chanzo cha ulimwengu. Sana sana unaongeza maswali zaidi. Alitoka wap? Ametengenezwaje(hakuna kisichokuwa na mwanzo wa hivihivi tu. Kama ulimwengu lazima uliumbwa basi hata huyo muumbaji wake aliumbwa. Tusizushe umaalumu kama kinga ya hoja)‽ Kwann aanzishe?(Jibu liwe la maana sio ili "aabudiwe" utaanzisha kingine kwann aabudiwe? Bila kuabudiwa hajatimia?) Kwann alilipua muda husika? Alilipuaje? Alikuwa na lengo la kufikia hapa tulipo sasa?

Ukikaa peke yako na imani zako jitathmini sana na mwisho ujikubali kwamba unaamini lakini hujui unachokiamini hata ukisoma likitabu gani la imani haisaidii!
 
Kuna namna ya kutazama dunia ambayo imani zote zinapukutika.

Everything you physically encounter that may seem to be improbable is actually possible as proven before your senses. It is not magical. Consequently, accept unverified and fabricated truths from other observers at your own peril.

Wataalam wa lugha wanisaidie kuandika kwa kiswahili hapa. Misamiati sina.
 
Uhuru wa kufanya matendo unajumuisha yote mazuri na mabaya.

Mola ameumba mabaya ila ametukataza tusifanye na akatupa uwezo wa kuyaepuka mabaya hayo.
Umesema ametupa uhuru wa kufanya matendo mazuri au mbaya..

Lakini umekatazwa tena usichague aina fulani ya vitu, huo bado utakuwa uhuru?
 
Lete Ushahidi wa Mungu kuniumba ACHA janja janja kamanda,
Prove Kwa fact na scientific method juu ya uhusika wa Mungu katika uumbaji wangu,
Nje ya Hapo sitaweza kukubaliana na hearsay aisee!
Hakuna mwingine Mwenye uwezo zaidi ya Mungu wa kuchanganya shahawa za baba yako na yai la mama yako ukapatikana wewe

Ila kama wewe unamjua aliyoifanya hiyo kazi hadi wewe Leo upo hapa duniani nitajia ni nani na kama humjui pia sema kuwa hamjui aliyefanya hadi Leo hii wewe upo hapa duniani

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Wana adhibiwa sababu wamepewa uhuru na wakaambiwa usifanye mabaya na ufanye mazuri na tukaambwa ubaya wa kufanya maovu na kuambiwa uzuri wa kufanya mema. Swali, sasa kwanini ufanye mabaya ?
Na wakati huo kabla Mungu hajawapatia huo uwezo wa kuamua kuchagua alikwisha jua kuwa hata akiwapatia hawawezi kuchagua kutofanya mabaya?

Kwasababu fate ilishatengenezwa kabla yao, hawa watu wakija kufanya mema itakuwa wanam prove wrong Mungu kuwa hajui yote

Adhabu kwa watu hawa ambao wameumbwa waje kufanya kile walichoumbiwa itakuwa ni uonezi na unafki wa Mungu
 
Uwe unajibu maswali, huyo mtu anapo fanya hilo jambo anakuwa amekusudia au kwa hiari yake ? Yaani kujua kwake Allah hakufungamani na wewe kutenda.
Anakuwa anatimiza hatma aliyoumbiwa na ndio maana hana option ya kubadili fate

Yani every step has been calculated
 
Na akaumba kiumbe ambacho kinaweza kuacha kufanya mabaya, yaani yote ameumbwa nayo.
Kwa hiyo Mungu lazima naye awe responsible kwa maovu ya mtu aliyochagua kwasababu kashiriki katika kuhakikisha mtu huyo anatekeleza hayo mabaya?
 
Hakuna mwingine Mwenye uwezo zaidi ya Mungu wa kuchanganya shahawa za baba yako na yai la mama yako ukapatikana wewe

Ila kama wewe unamjua aliyoifanya hiyo kazi hadi wewe Leo upo hapa duniani nitajia ni nani na kama humjui pia sema kuwa hamjui aliyefanya hadi Leo hii wewe upo hapa duniani

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Uwezekano wa kuchukuwa yai na virutubisho. Kutumia maabara kuvichanganya upo. Nje ya mfuko wa uzazi wa binadamu. Sio jambo la kimungu bali hata binadamu anaweza. Fatilia utaambiwa. Kuna kliniki zinapandikiza mimba baada ya kupata mchanganyiko mzuri. Kuna benki za shahawa na mayai. Kuna wanaoshindwa kuzaa kwa njia ya kuparamiana kawaida au kutaka mtoto bila ya kuwa na mahusiano na mtu mwingne, hizi njia zinawasaidia. Sayansi tiba imewasaidia wengi sana sehemu aliyoshindwa huyo " mungu" na mambo yake.
 
Kuna bank ya kuhifadhi shahawa na mayai nilidhanii utasema kuna mtambo unao tengeneza shahawa na mayai ya binaadam

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Naielewa sana Biblia..ila kuna sehemu naona hapapo sawa kbsa..yaani naona tumepigwa, inakuwaje duniani watu tunaishi kwa kuteseka na magonjwa,vita,kifo eti sababu ni tunda..!
 
Lete Ushahidi wa Mungu kuniumba ACHA janja janja kamanda,
Prove Kwa fact na scientific method juu ya uhusika wa Mungu katika uumbaji wangu,
Nje ya Hapo sitaweza kukubaliana na hearsay aisee!
Quran 35:11
Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii.

Quran 23:14.
Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.

Umeumbwa kupitia hizo process na hizo process naamini unazikubali ila maandiko yanazema Mungu ndio aliyefanya hayo

Najua kuwa wewe hauamini Quran nataka unitajie kwa upande wako ni nani alifanya hizo process hadi Leo hii wewe upo hapa duniani

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Umesema ametupa uhuru wa kufanya matendo mazuri au mbaya..

Lakini umekatazwa tena usichague aina fulani ya vitu, huo bado utakuwa uhuru?
Huo bado ni uhuru sababu ya lile lengo la wewe kuumbwa.
 
Kwa hiyo Mungu lazima naye awe responsible kwa maovu ya mtu aliyochagua kwasababu kashiriki katika kuhakikisha mtu huyo anatekeleza hayo mabaya?
Ameshiriki kivipi ? Nilikuuliza ukifanya mabaya huwa unaamua kwa hiari yako au unafanye ? Haya maswali ungekuwa unajibu yangekuepusha na makosa.
 
Na wakati huo kabla Mungu hajawapatia huo uwezo wa kuamua kuchagua alikwisha jua kuwa hata akiwapatia hawawezi kuchagua kutofanya mabaya?

Kwasababu fate ilishatengenezwa kabla yao, hawa watu wakija kufanya mema itakuwa wanam prove wrong Mungu kuwa hajui yote

Adhabu kwa watu hawa ambao wameumbwa waje kufanya kile walichoumbiwa itakuwa ni uonezi na unafki wa Mungu
Nakuuliza swali, unajua mwisho wako utakueaje ?
 
Muuaji wa watu 50 angeweza kuepuka kuua wakati Mungu alikwishajua kabla hata hajazaliwa kua atakuja kuua watu 50?
Kujua kwake hakukuzuii wewe kufanya unachotaka. Unarudia swali ambalo nimeshakujibu.

Unajua kwanini mwanadamu ameumbwa na matashi, akili na mfano wake ?
 
Sikuweza kuamua kuzaliwa au lah kwasababu hakuna freewill

Kutokuamua kwa watu kufanya yale wayatakayo ni ushahidi tosha kuwa watu hawako huru

Mtoto wa miezi mitatu tumboni kwa mama yake anauwezo wa kujitetea kutokufa pindi mama yake akitaka kumuua kwa kuitoa mimba?
Ndiyo maana kuna mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu, si kwa mtoto mchnga tu bali kwa mtu yoyote.
 
Back
Top Bottom