Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Mungu wako, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ambaye hapo hapo kaumba dunia ambayo inaruhusu maovu yaweze kutokea, hayupo.

Kwa nini hayupo?

Unakumbuka tumetoka kuongelea habari ya contradiction, kwamba pembetatu yenye nyuzi 180 ambayo pia ni duara lenye nyuzi 360 hapo hapo haiwezi kuwepo?

Kwa sababu ya contradiction?

Mungu wako huyo ni dhana ambayo ipo sawasawa na pembetatu hiyo.

Upande mmoja, anasemwa kwamba ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote. Huu upande ni sawa na pembetatu yenye nyuzi 180.

Upande mwingine, ameumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya yaweze kutokea. Huu upande ni sawa na duara lenye nyuzi 360.

Kama vile ambavyo haiwezekani pembetatu yenye nyuzi 180 ikawa duara lenye nyuzi 360 hapopo, ndivyo Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hatakiwi kimantiki kuumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya ni contradiction.Kwa nini aumbe ulimwengu unaoruhusu mabaya wakati yeye ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?

Contradiction hii, inaonesha Mungu huyu hayupo, ni hadithi iliyotungwa na watu tu.

Ingekuwa rahisi sana kukubali uwepo wa Mungu huyu kama ulimwengu ungekuwa hauruhusu mabaya.

Ulimwengu huo ambao hauruhusu mabaya, ungekuwa hauna logical inconsistency na dhana ya kuwepo Mungu, wala usinge contradict uwepo wa Mungu.

Lakini, kwa sababu tunaona ulimwengu ambao unaruhusu mabaya, ulimwengu huu una contradict habari ya kuwepo Mungu na unatuonesha kwamba habari hiyo ni hadithi ya kutungwa na watu tu.

Kama vile contradiction katika habari ya kuwepo kwa pembetatu iliyo duara inavyotuonesha pembetatu duara hiyo haipo, ni tungo ya mtu tu.
Sasa unaharibu utaribu kiongozi wangu. Jibu maswali niliyo kuuliza kisha uendelee na haya maelezo.

Shukrani.
 
Sasa unaharibu utaribu kiongozi wangu. Jibu maswali niliyo kuuliza kisha uendelee na haya maelezo.

Shukrani.
Maswali gani, hebu rudia.

Umekubali dhana ya Mungu wako kuwepo ina contradiction?
 
Maswali gani, hebu rudia.

Umekubali dhana ya Mungu wako kuwepo ina contradiction?
Post namba 291.

Sijakubali kwa sababu zifuatazo :

1. Humjui Mola ni nani na ana sifa gani ?
2. Kingine Mola haelezewi kwa dhana.
3. Umeshindwa kutoa ulinganyo sahihi.

Ukishajibu maswali kwenye post namba 291. Narudi kumalizia hapa nilipo ishia.
 
Thibitisha Mungu yupo, na kwamba hizo habari za kuwepo kwa Mungu si hadithi za kusadikika zilizotungwa na watu tu.

Twende pointi moja bada ya nyingine katika uthibitisho wako.
Mungu yupo ila uchawi ndio haupo
 
Mungu wako, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ambaye hapo hapo kaumba dunia ambayo inaruhusu maovu yaweze kutokea, hayupo.

Kwa nini hayupo?

Unakumbuka tumetoka kuongelea habari ya contradiction, kwamba pembetatu yenye nyuzi 180 ambayo pia ni duara lenye nyuzi 360 hapo hapo haiwezi kuwepo?

Kwa sababu ya contradiction?
Naanzia hapa. Unaelewa nini kuhusu "uwezo wote" ? Maana ya uwezo wote si kuzuia tu bali kuruhusu ni katika uwezo wa Mola. Siyo dunia inaruhusu bali Mola anaruhusu hayo kwa hekima zake.

Naomba nikuulize swali dogo, unakubali kwamba "contradiction" pia huonekana iwa mtu ambaye hana elimu juu ya jambo husika unakubali hilo ? Yaani mfano wewe achilia mbali, hujaonyesha hiyo "contradiction" lakini umeona wewe kama kuna "contradiction" kutokana na uchachefu wako wa maarifa ila hilo unalo dai halina contradiction.

Mungu wako huyo ni dhana ambayo ipo sawasawa na pembetatu hiyo.

Upande mmoja, anasemwa kwamba ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote. Huu upande ni sawa na pembetatu yenye nyuzi 180.
Hii siyo kweli sababu Mola ni muweza na hakuna jambo ambalo linatoka nje ya Milki, yake hakuna linalo tokea bila ya idhini yake, huu ndiyo uwezo wa Mola ulio kamili.

Kwa mtazamo wako au kulazimisha iww hivyo, kungeonyesha udhaifu wa Mola. Naomba nikuulize swali lingine, majanga yanapo kuja huwa yanadumu au baada ya muda yanaondoka ? Jibu huwa yanaondoka, je huwa yanaondoka kwa sababu gani au yanajiondoa yenyewe ?

Upendo wote haumaanishi kuwa umili upande mmoja, ni katika upendo kutoa adhabu kadhalika ni katika upendo kukanya na kutoa nasaha. Hui ndiyo upendo wa kweli.
Upande mwingine, ameumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya yaweze kutokea. Huu upande ni sawa na duara lenye nyuzi 360.

Kama vile ambavyo haiwezekani pembetatu yenye nyuzi 180 ikawa duara lenye nyuzi 360 hapopo, ndivyo Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hatakiwi kimantiki kuumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya.
Unasema vipi haiwezekani wakati Mola ameruhusu yatokee ?
 
Hakuna siku mtafika mwisho wa huu mjadala....

Facts na imani huwa hazikai pamoja hata siku moja...

Ila wazee wa imani huwaona wasio na hio imani ni wakosaji sana... But not vice versa... So mijadala kama hii huwa haifiki mwisho...
Mpaka sasa hakuna mtu aliyepangua contradiction ya problem of evil.

Na hilo linaonesha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
 
Post namba 291.

Sijakubali kwa sababu zifuatazo :

1. Humjui Mola ni nani na ana sifa gani ?
2. Kingine Mola haelezewi kwa dhana.
3. Umeshindwa kutoa ulinganyo sahihi.

Ukishajibu maswali kwenye post namba 291. Narudi kumalizia hapa nilipo ishia.
Unamtaja taja Mola.

Unajuaje huyo Mola yupo kweli na habari za kuwepo kwake si hadithi za watu tu?

Unaweza kuthibitisha Mola yupo kweli?
 
Naanzia hapa. Unaelewa nini kuhusu "uwezo wote" ? Maana ya uwezo wote si kuzuia tu bali kuruhusu ni katika uwezo wa Mola. Siyo dunia inaruhusu bali Mola anaruhusu hayo kwa hekima zake.

Naomba nikuulize swali dogo, unakubali kwamba "contradiction" pia huonekana iwa mtu ambaye hana elimu juu ya jambo husika unakubali hilo ? Yaani mfano wewe achilia mbali, hujaonyesha hiyo "contradiction" lakini umeona wewe kama kuna "contradiction" kutokana na uchachefu wako wa maarifa ila hilo unalo dai halina contradiction.

Hii siyo kweli sababu Mola ni muweza na hakuna jambo ambalo linatoka nje ya Milki, yake hakuna linalo tokea bila ya idhini yake, huu ndiyo uwezo wa Mola ulio kamili.

Kwa mtazamo wako au kulazimisha iww hivyo, kungeonyesha udhaifu wa Mola. Naomba nikuulize swali lingine, majanga yanapo kuja huwa yanadumu au baada ya muda yanaondoka ? Jibu huwa yanaondoka, je huwa yanaondoka kwa sababu gani au yanajiondoa yenyewe ?

Upendo wote haumaanishi kuwa umili upande mmoja, ni katika upendo kutoa adhabu kadhalika ni katika upendo kukanya na kutoa nasaha. Hui ndiyo upendo wa kweli.

Unasema vipi haiwezekani wakati Mola ameruhusu yatokee ?
Unamtajataja Mola.

Thibitisha Mola yupo na kwamba habari za kuwepo kwake si hadithi tupu za watu tu.
 
Unamtaja taja Mola.

Unajuaje huyo Mola yupo kweli na habari za kuwepo kwake si hadithi za watu tu?

Unaweza kuthibitisha Mola yupo kweli?
Hili mimi naweza, ila utaratibu lazima ufatwe. Lazima ujibu maswali ninayo kuuliza.
 
Hili mimi naweza, ila utaratibu lazima ufatwe. Lazima ujibu maswali ninayo kuuliza.
Hujathibitisha Mola yupo.

Unasema tu Mola hivi, Mola vile.

Thibitisha Mola yupo kwanza.
 
Hili kwangu rahisi sana. Shida yako hujibi maswali yangu, sasa maana ya mjadala inakuwa haipo tena.
Maswali yako yanajikita kwenye Mola hivi, Mola vile.

Wakati hujathibitisha Mola yupo.

Thibitisha kwanza Mola yupo kabla ya kumtaja kwenye swali lolote.

Vinginevyo tutajuaje swali lako ni/ si batili kama hatuwezi hata kuthibitisha Mola yupo?
 
Hujathibitisha Mola yupo.

Unasema tu Mola hivi, Mola vile.

Thibitisha Mola yupo kwanza.
Hili litafata, usiwe na hofu nalo kabisa, sababu wewe umeshindwa kuthibitisha kutokuwepo kwa Mola, mimi naweza kuthibitisha kuwepo kwake.

Tumalize hili.
 
Maswali yako yanajikita kwenye Mola hivi, Mola vile.
Sasa si ndiyo uonyeshe kutokuwepo kwake kwa kujibu maswali hayo, au kukosoa, au unamuongelea usiye mjua ?

Maswali yangu mepesi sana, na ni kwenye post namba 290 na siyo 291.
Screenshot_20220401_203237_com.android.chrome.jpg

Ni hayo tu tumalize hili.
Wakati hujathibitisha Mola yupo.

Thibitisha kwanza Mola yupo kabla ya kumtaja kwenye swali lolote.

Vinginevyo tutajuaje swali lako ni/ si batili kama hatuwezi hata kuthibitisha Mola yupo?
Ila wewe bado hujathbitisha sasa ingekuwaje kama ningekuwa sijibu maswali yako ? Mjadala usinge leta maana.

Unakubali kama hujathibitisha kutokuwepo kwa Mola ?

Sasa si unaonyesha tu ubatili wa swali langu kama ambavyo mimi huwa nakosa kwanza unachokiamini na kukuonyesha.

Uwepo wa Mola unathibitishwa kwa njia zifuatazo (nakupa dondoo kwanza, maelezo yatafata ukishajibu maswali yangu).

1. Akili
2. Maumbile (mazingira)
3. Ufunuo.
 
Weka ushahidi mwana sayansi gani duniani aliyewwza kutengeneza mbegu za kiume na mayai ya mwanamke ili apatikane binaadam

Mpaka sasa hakuna mwanasayansi yoyoye anayeweza

1)kutengeneza shahawa na mayai ya mwanamke ili azaliwe binaadam

2) Kumfanya binaadam asizeeke na aishi milele

3) kumfufua mtu aliyekufa

Niliweka hizo hoja kwa sababu hizo hoja 3 hapo zinabeba uwezo wa Mungu

Kwa bahati mbaya hujajibu hata moja nilijua utaweka link za makala mbalimbali kuthibitisha hao banadamu wenzako wenye uwezo wa kuumba binadamu wengine kama wewe

Katika Qurani Mungu ametumbia hakuna yoyote anaeweza kuumba hata Inzi zaidi yake yeye Mwenyezi Mungu

Unaongea vitu kana kwamba tunaishi dunia totauti wakati wote tunaishi dunia moja na dunia ni kama Kijiji

Hao wanasansi wako ambao ndio unataka wakutanyie prove kuwa hakuna Mungu sio tu kuumba binaadam hata uwezo wa kuumba organs za binaadam hawana

Hawezi kuumba FIGO
Hawawezi kuumba Moyo
Hawawezi kuumba Ini

Juzi kati kuna mtu walimuwekea organ ya Nguruwe kama sio ini basi ni moyo au figo na wamefeli jamaa ameshindwa kuishi amefariki

Mtabaki tu kudanganyana na kujazana ujinga

Nahata kama ungekuwepo huyo mwanasansi anayetengeneza viumbe hai
Watu kama sisi tungemuliza hayo material aliyoyatumia amepata wapi maana inabidi atoke nje ya universe akatafute hayo material kwa sababu material yaliopo hapa duniani yote ni Mungu hivyo angekuwa hajafanya kitu
"... kwa sababu material yaliyopo hapa duniani ni mungu...." hii ndio level ya ufahamu wako. Naona tuko limwengu mbili tofauti sana za mitazamo. Ni kama tungekutana uwanja wa medani tungeuana maana mawazo yako mbali mno kati yetu. Conclusion ya mungu umeiweka mbele, yaani hivyo ni tofauti kabisa na mtazamo wangu. Hitimisho halifikiwi kirahisi hivyo.

Tukubali tu kutokukubaliana?
 
Yote uliyoongea hayana mashiko.Eti uchawi haupo,mimi nilishawahi kumuona mchawi akiwa katika kazi zake.

Bado utarudi pale pale tu nikikuuliza hiyo big bang theory ilisababishwa na nini na hizo atoms zilitokeaje?
Nimecheka sana. Kwahiyo ukimuona mchawi ina maana uchawi upo? Labda hujanielewa nimemaanisha kwa kauli "uchawi haupo", ni hivi... hakuna namna yoyote ya mazingaombo na porojo za hao wanaojiita wachawi kuwa na athari zozote za moja kwa moja. Na hapa niongeze mitume, manabii, waganga, wachungaji, watabiri, mungu na vyote vya misingi ya imani si lolote si chochote. Kwenda kwa mganga, au nyumba za ibada ni kupoteza muda. Hutopata unachokihitaji huko. Fanya mambo ya msingi na sio hayo ya imani zote ambazo ni potofu kwa ufupi.

Kama ulishawahi kushuhudia uchawi naomba uweke link hapa tukaone exhibition hiyo ya uchawi. Najua hakuna makala. Wachawi sio wasomi au hawaandiki mambo yao. Watakosa soko. Unajua sayansi ya roketi inafanya kazi kwa kuona, sio uchawi ambao matukio yake yote ni hadithi na hisia za watu. Ubaya wa uchawi na ubaya wa kudondosha mabomu utaogopa upi? Ukisema uchawi utakuwa umedhihirisha ulivyopotoka. Sayansi ya tiba inafanya kazi wote tunajua hili, sio maombi ambayo hayana kipimo chochote. Yameenda hujui, utajipa moyo tu. Yanajibiwa vipi au lini, unajipa moyo tu. Ndio maana kuna video na ukitaka za mubashara utaona pia roketi zikiruka au kutua lakini hutoona kamwe video au picha ya mtu anapaa au mtu aliyechanwa na kuhakikiwa amekufa akafufuka (tungependa kuona video mbili mtu kafa kafanyiwa autopsy, ya pili akifufuka)... hao manabii na waganga wakipata tb au infection wataenda hospitali kunywa dawa.

Ni biashara tu. Ndio maana kuna viingilio huko kwenye mambo yenu ya imani. Ukienda kwenye mhadhara wa taaluma kwa mfano Nkurumah hall utaondoka na pesa zako na pengine utakuwa na deppsit ya mawazo mapya lakin nenda kwenye mhadhara wa nabii au mponyaji fulani ukaone ujinga unaoendelea hapo. Waganga, manabii, nyumba za ibada pamoja na kukujaza ujinga wa vitu vya uongo na hela watakuchota ukiwa na akili ya kutekwa na hoja nyepesi nyepesi. Lakini shule ni bure. Vitabu na video zinazotibu ujinga na kukuonyesha uhalisia wa mambo zipo. Utajua mambo mengi kutoka madogo kama kwann anga tunaona ya blue au makubwa binadamu tumetoka wapi na tunaenda wapi.... Ni wewe tu uchague. Weka bando uangalie, kusikiliza na kusoma vitu vya maana au uende kwenye mkesha wa ibada, sadaka yako na mavitabu yaliyojaa hadithi za uongo.

Uamuzi ni wako. Toa ujinga au endelea kujidanganya.
 
Hata mimi nishawaona sana tu, na nishapiga sana mateke nazi zao njiapanda. Uchawi ni matokeo ya uwezo katika kuchanganua changamoto tunazokutana nazo na kutoka na jibu sahihi. Kama uchawi ungekuwa unafanya kazi dunia isingekuwa sehemu salama ya kuishi, kwasab ukinizingua kidogo tu nishakuroga unakua chizi au kukuua kabisa
Uchawi na hizi imani za miungu zingekuwepo hakuna ambaye angefeli, hakuna gari la mizigo au abiria lingeua au kupoteza mali... kusingekuwa na masikini... mambo ni mengi. Kila upande ukiamgalia utaona contradiction ya uhalisia na imani. Waafrika na maji yetu ya kichawi kule kusini wajerumani wasingetuweza na virisasi vya. Huko Marekani walionunua watumwa mashamba yao yamgelaaniwa na kukosa utajiri... mambo ni mengi. Ubishi tu wakuvua imani tulizolishwa toka utotoni.
 
Sasa si ndiyo uonyeshe kutokuwepo kwake kwa kujibu maswali hayo, au kukosoa, au unamuongelea usiye mjua ?

Maswali yangu mepesi sana, na ni kwenye post namba 290 na siyo 291.
View attachment 2172245
Ni hayo tu tumalize hili.

Ila wewe bado hujathbitisha sasa ingekuwaje kama ningekuwa sijibu maswali yako ? Mjadala usinge leta maana.

Unakubali kama hujathibitisha kutokuwepo kwa Mola ?

Sasa si unaonyesha tu ubatili wa swali langu kama ambavyo mimi huwa nakosa kwanza unachokiamini na kukuonyesha.

Uwepo wa Mola unathibitishwa kwa njia zifuatazo (nakupa dondoo kwanza, maelezo yatafata ukishajibu maswali yangu).

1. Akili
2. Maumbile (mazingira)
3. Ufunuo.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kuumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya ni contradiction.

Unaelewa hilo?
 
Hili mimi naweza, ila utaratibu lazima ufatwe. Lazima ujibu maswali ninayo kuuliza.
Swali lako lolote linalomtaja Mungu ni lazima lianze kwa kuthibitisha Mungu yupo.

Ili tujue swali si la hadithi za kufikirika tu.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Back
Top Bottom