Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Huelewi hata falsafa za uthibitisho.

Asiyepo, hathibitishiki kwamba hayupo.
Falsafa ni mawazo ya watu yaliyo mili katika ujinga. Hilo kwanza weka akilini. Nimesoma sana Falsafa, nikaachana nayo.

Swali la msingi, umejuaje ya kuwa hayupo ? Hili ndiyo swali la msingi, yaani kwa ufupi halikwepeki swali hili.
Kwa sababu hayupo na uthibitisho unakwenda sana kuonesha vilivyopo.
Hata hakuna kwa sababu hayupo. Ukiulizwa fulani hayupo ? Ukajibu hayupo, ukiulizwa umejuaje kama hayupo, utajibu tena "Kwasababu hayupo ?". Utakuwa na matatizo ya akili, majibu huwa aidha utoe sababu au useme "Sijui kwanini hayupo".

Falsafa ni kama fani ni elimu ya wasio fikiri kwa usahihi.
Ila, naweza kukuthibitishia Allah hayupo kwa "proof by contradiction".
Proof by Contradiction haiwezi kuthibitisha hilo kwa sababu zifuatazo.

1. Suala la uwepo wa Allah ni hakika.
2. Maarifa yenu ni machache juu ya elimu kuhusu Allah.
3. Proof by Contradiction inakosa sharti kuu la sababu.
Kama vile ninavyoweza kukuthibitishia kwamba hakuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika Euclidean geometry.
Jifunze kutoa mifano na kuiweka mahala pake. Kwanini umeweza kufanya hivyo, kwa sababu unaijua Pembe tatu ni ipi na duara ni nini ? Huu mfano hauwezi kuakisi uhalisia wa uwepo wa Allah, sababu humjui Allah ni nani.
Mungu wako, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anakuwa contradicted na dunia tu
Dunia kwa dhati yake hairuhusu mabaya bali Allah anaruhusu mabaya yatokee kwa hekima zake, na hapo katikati kuna mengi ambayo nyinyi hamtaki kuyajua. Kwa kutokujua kwenu hili ni muhali kwenu.
Mungu huyo angekuwepo, logically kusingewezekana kuwepo na
Hi ni dhana ambayo haina uhakika sababu, tutarudi katika swali la msingi umejuaje hilo ?

Kingine msingi wa Logic ni nini ? Jibu ni akili. Akili ina ukomo au haina ukomo ? Jibu ina ukomo ? Vipi akili iwe marejeo yako pekee ya kufikia hitimisho juu ya jambo ambalo wa akili pekee haiwezi kufanya hivyo ?

Swali langu, ni kuwa unaweza kutithibitishia hiki unachokisema ? Jibu huwezi.
Hilo linathibitisha Mungu wako hayupo.
Hujathibitisha bado hapa kama unarap tu, yaani akili yako imeishia hapo, swali la msingi umejuaje hayupo ?
Ni hadithi za watu tu.
Thibitisha ya kuwa ni hadithi za watu. Sababu hadithi tunazijua sisi.
Kukubali uwepo wa Mungu huyu, ni sawa na kukubali kwamba kuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika planes za Euclidean geometry
Si sawa kama nilivyo kuonyesha hapo juu.
 
Falsafa ni mawazo ya watu yaliyo mili katika ujinga. Hilo kwanza weka akilini. Nimesoma sana Falsafa, nikaachana nayo.

Swali la msingi, umejuaje ya kuwa hayupo ? Hili ndiyo swali la msingi, yaani kwa ufupi halikwepeki swali hili.

Hata hakuna kwa sababu hayupo. Ukiulizwa fulani hayupo ? Ukajibu hayupo, ukiulizwa umejuaje kama hayupo, utajibu tena "Kwasababu hayupo ?". Utakuwa na matatizo ya akili, majibu huwa aidha utoe sababu au useme "Sijui kwanini hayupo".

Falsafa ni kama fani ni elimu ya wasio fikiri kwa usahihi.

Proof by Contradiction haiwezi kuthibitisha hilo kwa sababu zifuatazo.

1. Suala la uwepo wa Allah ni hakika.
2. Maarifa yenu ni machache juu ya elimu kuhusu Allah.
3. Proof by Contradiction inakosa sharti kuu la sababu.

Jifunze kutoa mifano na kuiweka mahala pake. Kwanini umeweza kufanya hivyo, kwa sababu unaijua Pembe tatu ni ipi na duara ni nini ? Huu mfano hauwezi kuakisi uhalisia wa uwepo wa Allah, sababu humjui Allah ni nani.

Dunia kwa dhati yake hairuhusu mabaya bali Allah anaruhusu mabaya yatokee kwa hekima zake, na hapo katikati kuna mengi ambayo nyinyi hamtaki kuyajua. Kwa kutokujua kwenu hili ni muhali kwenu.

Hi ni dhana ambayo haina uhakika sababu, tutarudi katika swali la msingi umejuaje hilo ?

Kingine msingi wa Logic ni nini ? Jibu ni akili. Akili ina ukomo au haina ukomo ? Jibu ina ukomo ? Vipi akili iwe marejeo yako pekee ya kufikia hitimisho juu ya jambo ambalo wa akili pekee haiwezi kufanya hivyo ?

Swali langu, ni kuwa unaweza kutithibitishia hiki unachokisema ? Jibu huwezi.

Hujathibitisha bado hapa kama unarap tu, yaani akili yako imeishia hapo, swali la msingi umejuaje hayupo ?

Thibitisha ya kuwa ni hadithi za watu. Sababu hadithi tunazijua sisi.

Si sawa kama nilivyo kuonyesha hapo juu.
Nikikwambia kuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika Euclidean geometry planes, utakubali?
 
Hili nimelielezea, ukiwa hujalewa jambo bora uulize kulingana na munasaba.

Kingine uhusiano wa Pembe tatu na duara kwenye uwepo wa Mola uko wapi ?

Jibu hakuna Pembetatu ambayo hapo hapo ni duara, na hii inaingia katika sifa anuai za kitu kwazo zinatofautisha kitu kimoja na kingine.

Naam, hoja yako iko wapi hapo ?
 
Nikikuuliza kwa nini hakuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara? Ipo tu, ila wewe akili yako ndogo huijui.

Utasemaje?
 
Nitakuambia haipo kwa sababu pembe tatu ina sifa anuai ambazo zinaitofautisha na Duara. Pembe tatu ina pande tatu zilizo katika mlalo fulani (angle) na duara ni mzunguko sawia wenye kulingana kutokea katikakati yake.

Nitakuomba unionyeshe hilo, ili nipate kujua.
 
Nikuoneshe kivipi? Pembetatu hiyo iliyo duara haionekani, kama Mungu wako.

Ukikataa uwepo wa pembetatu hiyo iliyo duara, kitu gani kinakufanya ukatae uwepo wake?
 
Nitarudi hapo hapo, kwamba kwanini ulisema hilo wakati huna ushahidi au huwezi kuonyesha ?

Mopa wetu haonekani kwa macho hapa duniani, ila siku ya malipo ataonekana. Kadhalika ameweka ishara za kuonyesha uwepo wake. Hapa nitakuuliza, nionyeshe ishara inayo onyesha kuwa kuna duara katika hiyo pembe tatu japo kuwa sisi hatuioni.
Ukikataa uwepo wa pembetatu hiyo iliyo duara, kitu

Ukikataa uwepo wa pembetatu hiyo iliyo duara, kitu gani kinakufanya ukatae uwepo wake?
Sijaona ishara inayo onyesha hilo. Kwahiyo kama wewe umeiona hiyo ishara tuonyeshe hapa.
 
Weka ushahidi mwana sayansi gani duniani aliyewwza kutengeneza mbegu za kiume na mayai ya mwanamke ili apatikane binaadam

Mpaka sasa hakuna mwanasayansi yoyoye anayeweza

1)kutengeneza shahawa na mayai ya mwanamke ili azaliwe binaadam

2) Kumfanya binaadam asizeeke na aishi milele

3) kumfufua mtu aliyekufa

Niliweka hizo hoja kwa sababu hizo hoja 3 hapo zinabeba uwezo wa Mungu

Kwa bahati mbaya hujajibu hata moja nilijua utaweka link za makala mbalimbali kuthibitisha hao banadamu wenzako wenye uwezo wa kuumba binadamu wengine kama wewe

Katika Qurani Mungu ametumbia hakuna yoyote anaeweza kuumba hata Inzi zaidi yake yeye Mwenyezi Mungu

Unaongea vitu kana kwamba tunaishi dunia totauti wakati wote tunaishi dunia moja na dunia ni kama Kijiji

Hao wanasansi wako ambao ndio unataka wakutanyie prove kuwa hakuna Mungu sio tu kuumba binaadam hata uwezo wa kuumba organs za binaadam hawana

Hawezi kuumba FIGO
Hawawezi kuumba Moyo
Hawawezi kuumba Ini

Juzi kati kuna mtu walimuwekea organ ya Nguruwe kama sio ini basi ni moyo au figo na wamefeli jamaa ameshindwa kuishi amefariki

Mtabaki tu kudanganyana na kujazana ujinga

Nahata kama ungekuwepo huyo mwanasansi anayetengeneza viumbe hai
Watu kama sisi tungemuliza hayo material aliyoyatumia amepata wapi maana inabidi atoke nje ya universe akatafute hayo material kwa sababu material yaliopo hapa duniani yote ni Mungu hivyo angekuwa hajafanya kitu
Unapata shida bure kuwaelimisha vichaa

Mungu anasema katika Quran binaadam Mwenye akili timamu akiangalia tu jua linapochomoza na baadae linazama yani mchana unatoweka na kuingia usiku anajua kuwa Mungu yupo

Kwa hiyo ukimuona mtu tokea amezaliwa kila siku anaona mabadiriko ya usiku na mchana pia na yeye mwenyewe yupo hapa duniani wala hakuwahi kuandika barua ya maombi kuja duniani alafu anasema hakuna Mungu basi jua huyo binaadam kuna kitu hakipo sawa katika ubongo wake
 
Nitarudi hapo hapo, kwamba kwanini ulisema hilo wakati huna ushahidi au huwezi kuonyesha ?

Mopa wetu haonekani kwa macho hapa duniani, ila siku ya malipo ataonekana. Kadhalika ameweka ishara za kuonyesha uwepo wake. Hapa nitakuuliza, nionyeshe ishara inayo onyesha kuwa kuna duara katika hiyo pembe tatu japo kuwa sisi hatuioni.

Sijaona ishara inayo onyesha hilo. Kwahiyo kama wewe umeiona hiyo ishara tuonyeshe hapa.
Unaelewa kwamba "pembetatu iliyo duara = Mungu "?

Na kwamba, ukipinga uwepo wa pembetatu iliyo duara, kama unataka kuwa logically consistent, ni lazima upinge uwepo wa Mungu?

Vyote, pembetatu iliyo duara na Mungu vina logical inconsistent, hutakiwi kukubali kimoja na kukataa kingine, ukikataa, kataa vyote, ukikubali, kubali vyote.

Mimi nakataa vyote, wewe uko logically inconsistent, unakataa kimoja na kukubali kimoja.
 
Unaelewa kwamba "pembetatu iliyo duara = Mungu "?
Onyesha hilo ? Unazijua sifa za Duara na sifa za Mola ?
Na kwamba, ukipinga uwepo wa pembetatu iliyo duara, kama unataka kuwa logically consistent, ni lazima upinge uwepo wa Mungu?
Hapa hakuna uhusiano. Sababu duara na pembe tatu ni zao la akili uliyo pewa na Mola. Unakubali hilo ?

Siyo lazima upinge sababu kila kimoja kinasimama kwa sifa zake. Unakubali hilo ?
 
Onyesha hilo ? Unazijua sifa za Duara na sifa za Mola ?

Hapa hakuna uhusiano. Sababu duara na pembe tatu ni zao la akili uliyo pewa na Mola. Unakubali hilo ?

Siyo lazima upinge sababu kila kimoja kinasimama kwa sifa zake. Unakubali hilo ?
Unaweza kuthibitisha Mola yupo kweli na habari zake si hadithi tu?

Kusema tu "Mola yupo" hakumfanyi awepo, kama mimi kusema "pembetatu iliyo duara ipo" hakufanyi iwepo.

Unaweza kuthibitisha Mola yupo?
 
Unaweza kuthibitisha Mola yupo kweli na habari zake si hadithi tu?

Kusema tu "Mola yupo" hakumfanyi awepo, kama mimi kusema "pembetatu iliyo duara" hakufanyi iwepo.

Unaweza kuthibitisha Mola yupo?
Tumeanza vizuri sana aisee,naona unaharibu utaratibu, nimejitahidi sana kujibu maswali yako, ila naona wewe unakimbia maswali yangu.

Kwa heshima na taadhima, naomba ujibu maswali yangu kisha tuendelee.
 
Maswali gani? Mbona na mimi nakuuliza uthibitishe Mola yupo hutaki kunipa uthibitisho?

Mtu akikwambia habari za kuwepo Mola ni hadithi tu kama "pembetatu iliyo duara", utamthibitishiaje Mola yupo kweli na si hadithi tu?
 
Post namba 291.

Umeona tulipo anzia lakini ? Ulijaribu kuonyesha kutokuwepo kwa Mola kwa niia uliyo itaja ambayo ni dhaifu sana kuzidi nyumba ya bui bui. Kisha tukafikia hapa tulipo.

Suala la kuwepo kwa Allah, nimelithibitisha zaidi ya mara tano na hili naliweza muda wowote. Ila itifaki lazima zizingatiwe

Hili naomba nikujibu baada ya wewe kujibu maswali yangu kwenye post namba 291.

Shukrani.
 
Kwanza kabisa, katika kujenga msingi wa kukujibu swali na kukuonesha unapotaka kuoneshwa, unafahamu "logical inconsistency" ni nini?

Unafahamu "contradiction" ni nini?
 
Sifahamu nieleweshe kisha urudi katika hoja ya msingi.

Shukrani.
 
Sifahamu nieleweshe kisha urudi katika hoja ya msingi.

Shukrani.
Sawa.

Logical inconsistency ni mkanganyiko wa kimantiki, mambo hayako sawa. Mushkeli katika mambo kimantiki.

Contradiction ni mambo kujipinga.

Contradiction ina tabia ya kuonesha uongo wa jambo.

Kwa mfano, mtu akisema kwamba, kuna pembetatu ambayo ni duara, wakati tunajua kwamba pembetatu ina nyuzi 180 na duara lina nyuzi 360, hapo tutajua hizi habari ni za uongo. Haiwezekani pembetatu ikawa duara hapo hapo.

Kwa sababu hiyo ni contradiction. Contradiction hiyo inatuonesha hii habari si kweli, hakuna pembetatu ambayo ni duara hapo hapo.

Mpaka hapo tumeelewana na kukubaliana kwamba contradiction imetuonesha pembetatu iliyo duara hapo hapo haiwezekani kuwepo katika Euclidean plane geometry?

Najenga msingi wa kuelewana vizuri upate kunifahamu mantiki yangu.
 
Nimekuelewa, naam tuendelee. Turudi kwenye maswali niliyo kuuliza.
 
Mungu wako, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ambaye hapo hapo kaumba dunia ambayo inaruhusu maovu yaweze kutokea, hayupo.

Kwa nini hayupo?

Unakumbuka tumetoka kuongelea habari ya contradiction, kwamba pembetatu yenye nyuzi 180 ambayo pia ni duara lenye nyuzi 360 hapo hapo haiwezi kuwepo?

Kwa sababu ya contradiction?

Mungu wako huyo ni dhana ambayo ipo sawasawa na pembetatu hiyo.

Upande mmoja, anasemwa kwamba ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote. Huu upande ni sawa na pembetatu yenye nyuzi 180.

Upande mwingine, ameumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya yaweze kutokea. Huu upande ni sawa na duara lenye nyuzi 360.

Kama vile ambavyo haiwezekani pembetatu yenye nyuzi 180 ikawa duara lenye nyuzi 360 hapopo, ndivyo Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hatakiwi kimantiki kuumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya ni contradiction.Kwa nini aumbe ulimwengu unaoruhusu mabaya wakati yeye ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?

Contradiction hii, inaonesha Mungu huyu hayupo, ni hadithi iliyotungwa na watu tu.

Ingekuwa rahisi sana kukubali uwepo wa Mungu huyu kama ulimwengu ungekuwa hauruhusu mabaya.

Ulimwengu huo ambao hauruhusu mabaya, ungekuwa hauna logical inconsistency na dhana ya kuwepo Mungu, wala usinge contradict uwepo wa Mungu.

Lakini, kwa sababu tunaona ulimwengu ambao unaruhusu mabaya, ulimwengu huu una contradict habari ya kuwepo Mungu na unatuonesha kwamba habari hiyo ni hadithi ya kutungwa na watu tu.

Kama vile contradiction katika habari ya kuwepo kwa pembetatu iliyo duara inavyotuonesha pembetatu duara hiyo haipo, ni tungo ya mtu tu.
 
Hakuna siku mtafika mwisho wa huu mjadala....

Facts na imani huwa hazikai pamoja hata siku moja...

Ila wazee wa imani huwaona wasio na hio imani ni wakosaji sana... But not vice versa... So mijadala kama hii huwa haifiki mwisho...
 
Back
Top Bottom