Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Consider hivi

  1. Mungu ni mwenye uwezo wote
  2. Kama Mungu muweza wa yote yupo, basi hakuwezi kuwa na mabaya
  3. Mungu ni mwenye upendo wote na mwema muda wote
  4. Kama Mungu huyo mwenye upendo wote yupo na mwema muda wote, basi hakuwezi kuwa na mabaya
  5. Mabaya yapo
  6. Kama mabaya yapo, hakuwezi kuwa na Mungu
Kwa hiyo mantiki itayofuata hapo itakuwa hivi
  1. Mungu hayupo
  2. Yupo ila sio muweza wa yote (lacking in some power)
  3. Mungu sio mjuzi wa yote
  4. Mungu hana upendo wote na muasisi wa maba
Hapa hakuna ulichofanya zaidi ya kujenga yako katika dhana. Hakuna mambo ya ku "consider" nenda kwenye uhalisia. Yaani mantiki kwa vyovyote haina uwezo wa kukupa ukweli.
Wewe umesema Mungu karuhusu mabaya kuwepo kwa point hiyo unakuwa umechagua option namba 4 inayoonesha Mungu hana upendo wote, kwa hiyo Mungu wako unayemuelezea wewe anayeruhusu mabaya definitely hawezi kuwa mwenye upendo wote na mwema muda wote kwa viumbe wake
Upendo wote ukoje ? Upendo wote maana yake hakuna kuadhibu au kukosoa ? Hii maana ya upendo wote mmeipata wapi ?

Upendo kamili wa Mola ni ule ambao hata wewe unae mkana anakupa pumzi na anakupa rizki. Maana ya upendo ni kutokumea maovu ? Vipi mzazi wako anapo kukanya baada ya kufanya makosa ? Humaanisha hakupendi ?

Upendo wote ni upi huo ? Msaada tafadhali.
Lakini ulipokuja kumuelezea kuwa Mungu katoa freewill ya kumfanya mtu aweze kuchagua apendacho unakuwa umegusa hoja namba 3 kuwa sio mjuzi wa yote

Kwanini nasema Mungu sio mjuzi wa yote

Kwasababu kabla hajampa uhuru huo wa kuchagua, huyu Mungu kupitia sifa yake ya ujuzi wote alipaswa awe mbele ya muda kwa kujua nini kitatokea mbeleni kwa hii freewill nayofikiria kumpa huyu mtu
Allah anajua yaliyopo na yatakayo tokea na ambayo hayajatokea anajua yakitokea yatakuwaje. Kalamu ishaandika miaka elfu 50 kabla ya mwanadamu kuumba.

Maana yake ni kuwa bado unaonyesha wazi ya kuwa unapinga juu ya jambo ambalo huna elimu nalo, yaani huja unachojua kumuhusu Mola muumba.
Kwamba katika muda huo huyu Mungu aliweza kujua kuwa ni kiasi gani freewill hiyo isingefanya kazi kwa ufanisi uliokamilika kwa namna atakavyo, na kwasababu ya error hiyo huyu Mungu angeweza ku fix hapo kupitia uwezo wote alionao na kutafuta suluhu ambayo ingempendeza
Huu utoto mwingine, nimeshakujibu hapo juu.
Lakini tunaona freewill bado inachagua mabaya, kwanini freewill isijihusishe kwa mema pekee?
Ikijihusisha na mema tu, inakuwa siyo freewill tena, freewill ili iwepo lazima kuwe na pande mbili, mazuri na mabaya. Hapi ndiyo kuna maana ya freewill. Kijana una uwezo mdogo sana wa kufikiri. Hata hili dogo limekushinda kung'amua.

Ndiyo maana leo kuna waja wana fanya mema na wapo wanao fanya mabaya, hii ndiyo maana ya freewill.
  1. Kwamba Mungu alishindwa?
  2. Hapana aliweza..
  3. Ila nini sasa mpaka freewill ihusishe chaguzi zisizo mema?
Nani amekwambia freewill inajihusisha na maovu tu ? Unapoamua kumfanya mtu wema ni kwa hiari yako au kwa kulazimishwa ? Jibu ni kwa hiari yako maana yake umechagua mwenyewe yaani kupitia uhuru wa matakwa yako (freewill). Kijana huelewi unachokiandika.
  1. Ni kwasababu Mungu alipenda? Ndio alipenda kwasababu asingependa asingeumba mabaya
  2. Kama alipenda basi mtu kuchagua mabaya kupitia freewill aliyopewa hakuwezi kuwa ni dhambi
Ni dhambi sababu alikuwa au anauwezo wa kutofanya mabaya akiamua. Lakini endapio akafanya mabaya kwa makusudi au bahati mbaya au kwa kutokujua, Allah ameweka wazi mlango wa toba na ukimtaka msamaha ana kusamehe, kwani yeye ni mwingi wa msamaha.

Ili uone akili yako ni finyi sana, yaani unajitungia mambo ambayo Allah hako nayo unayajengea kwa uongo.
  1. Lakini kuna moto wa jehanamu
  2. Moto kwa ajili ya nini?
  3. Kuchoma wale waliochagua kufanya mabaya
Kuwachoma wale waovu walio chagua mabaya kwa hiari yao. Wewe leo hii unapo enda kuiba, hujalazimishwa na mtu, bali ni kwa hiari yako, lakini hapo hapo ungetaka usingeenda kuiba, hii ndiyo maana ya freewill. Vipi unapo amua kufanya ovu na usifanye, hapo unajiweka katika hali gani ? Ni freewill ya maovu tu au pande zote ?

Yaani, kuna maneno niliyasoma juzi ya mwanachuoni mmoja aitwae Ibnul Qayyim al Jawziyah, mazuri sana, juu ya wale ambao wanapinga ufunuo toka Allah, basi Allah atawapa mtihani wa kuwaondoshea akili na itafikia muda ataongea jambo fulani mbele ya mtu mwenye akili, na ataonekana kituko mno. Hilo naliona kwako, yaani unapinga jambo kichwa mchunga jambo ambalo laiti kama ungejitathmini wewe mwenyewe hakika ungejiona mjinga wa kutupwa.
Mpaka hapa we have come to the conclusion this God is sadistic
Angalia magap uliyo yaacha katika hiki ulichokiandika, kwanza hakuna hata swali moja katika maswali zaidi ya matano niliyo yauliza ambalo umejibu.

Pili, umethibitisha ya kuwa humjui Mola, umeandika mambo ambayo Allah katika uumbaji ameyaelezea kwa miaka elfu 50 kabla, sasa inakuwaje mna mkana na huku hamumjui ? Huu ujasiri wanao wajinga kama nyinyi.

Tatu, umemzulia Mola uongo, sasa vipi ufikie hitimisho kwa mambo ya uongo ?

Nne, kwa haya uliyo yaandika majibu unayapata katika wewe mwenyewe ukijiangalia katika matendo yako, je ni kweli "freewill" ipo kwenye mabaya tu ? Jiangalie wewe.

Tano,wito wangu naomba muwe mnajibu maswali ninayo wauliza.

Baada ya hapa sitajibu swali lako lolote mpaka ujibu au mjibu maswali niliyo wauliza

Shukrani.
 
Soma nimeshajibu hili swali zaidi ya mara mbili humu ndani.
Wapi umemjibu hili.?

Wewe unatoa maelezo kwa fikra zako na unahisi ushajibu mtu_ yani kwa ufupi unahubiri badala ya kujibu unachoulizwa

Usiwe msumbufu kama Allah wako asiyekuwepo
 
Uthibitisho kuwa Mungu yupo ni wewe kuletwa hapa duniani

Mungu ndio aliyechanganya majimaji ya yaliyotoka kwa baba yako na kwa mama yako ndio ukapatikana wewe

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Hayo ni maneno bila uthibitisho kamanda thibitisha kama Mimi niliumbwa na Mungu,
Lete fact na scientific method alizotumia kuniumba Ili kuprove uumbaji wake!
 
Hapa hakuna ulichofanya zaidi ya kujenga yako katika dhana. Hakuna mambo ya ku "consider" nenda kwenye uhalisia. Yaani mantiki kwa vyovyote haina uwezo wa kukupa ukweli.

Upendo wote ukoje ? Upendo wote maana yake hakuna kuadhibu au kukosoa ? Hii maana ya upendo wote mmeipata wapi ?

Upendo kamili wa Mola ni ule ambao hata wewe unae mkana anakupa pumzi na anakupa rizki. Maana ya upendo ni kutokumea maovu ? Vipi mzazi wako anapo kukanya baada ya kufanya makosa ? Humaanisha hakupendi ?

Upendo wote ni upi huo ? Msaada tafadhali.

Allah anajua yaliyopo na yatakayo tokea na ambayo hayajatokea anajua yakitokea yatakuwaje. Kalamu ishaandika miaka elfu 50 kabla ya mwanadamu kuumba.

Maana yake ni kuwa bado unaonyesha wazi ya kuwa unapinga juu ya jambo ambalo huna elimu nalo, yaani huja unachojua kumuhusu Mola muumba.

Huu utoto mwingine, nimeshakujibu hapo juu.

Ikijihusisha na mema tu, inakuwa siyo freewill tena, freewill ili iwepo lazima kuwe na pande mbili, mazuri na mabaya. Hapi ndiyo kuna maana ya freewill. Kijana una uwezo mdogo sana wa kufikiri. Hata hili dogo limekushinda kung'amua.

Ndiyo maana leo kuna waja wana fanya mema na wapo wanao fanya mabaya, hii ndiyo maana ya freewill.

Nani amekwambia freewill inajihusisha na maovu tu ? Unapoamua kumfanya mtu wema ni kwa hiari yako au kwa kulazimishwa ? Jibu ni kwa hiari yako maana yake umechagua mwenyewe yaani kupitia uhuru wa matakwa yako (freewill). Kijana huelewi unachokiandika.

Ni dhambi sababu alikuwa au anauwezo wa kutofanya mabaya akiamua. Lakini endapio akafanya mabaya kwa makusudi au bahati mbaya au kwa kutokujua, Allah ameweka wazi mlango wa toba na ukimtaka msamaha ana kusamehe, kwani yeye ni mwingi wa msamaha.

Ili uone akili yako ni finyi sana, yaani unajitungia mambo ambayo Allah hako nayo unayajengea kwa uongo.

Kuwachoma wale waovu walio chagua mabaya kwa hiari yao. Wewe leo hii unapo enda kuiba, hujalazimishwa na mtu, bali ni kwa hiari yako, lakini hapo hapo ungetaka usingeenda kuiba, hii ndiyo maana ya freewill. Vipi unapo amua kufanya ovu na usifanye, hapo unajiweka katika hali gani ? Ni freewill ya maovu tu au pande zote ?

Yaani, kuna maneno niliyasoma juzi ya mwanachuoni mmoja aitwae Ibnul Qayyim al Jawziyah, mazuri sana, juu ya wale ambao wanapinga ufunuo toka Allah, basi Allah atawapa mtihani wa kuwaondoshea akili na itafikia muda ataongea jambo fulani mbele ya mtu mwenye akili, na ataonekana kituko mno. Hilo naliona kwako, yaani unapinga jambo kichwa mchunga jambo ambalo laiti kama ungejitathmini wewe mwenyewe hakika ungejiona mjinga wa kutupwa.

Angalia magap uliyo yaacha katika hiki ulichokiandika, kwanza hakuna hata swali moja katika maswali zaidi ya matano niliyo yauliza ambalo umejibu.

Pili, umethibitisha ya kuwa humjui Mola, umeandika mambo ambayo Allah katika uumbaji ameyaelezea kwa miaka elfu 50 kabla, sasa inakuwaje mna mkana na huku hamumjui ? Huu ujasiri wanao wajinga kama nyinyi.

Tatu, umemzulia Mola uongo, sasa vipi ufikie hitimisho kwa mambo ya uongo ?

Nne, kwa haya uliyo yaandika majibu unayapata katika wewe mwenyewe ukijiangalia katika matendo yako, je ni kweli "freewill" ipo kwenye mabaya tu ? Jiangalie wewe.

Tano,wito wangu naomba muwe mnajibu maswali ninayo wauliza.

Baada ya hapa sitajibu swali lako lolote mpaka ujibu au mjibu maswali niliyo wauliza

Shukrani.
Mungu mjuzi wa yote ambaye anaweza kujua yaliyo mbele ya wakati kabla hayajatokea hana sababu ya kutoa adhabu

Mungu kaona mtu huyu ataenda kuua mtoto asiyekuwa na hatia

Na wakati huo ana uwezo wa kudhibiti tukio hilo lisifanyike

Na anasababu ya yeye kudhibiti kwasababu kwanza hilo tukio halimpendezi lakini ni mwenye upendo wote

Ukisema kwamba Mungu kamuacha mtu huyo aue mtoto asiye na hatia ili kuonesha amempa mtu freewill ya kufanya atakalo.

Kutakuwa kuna mambo mawili
  1. Mtoto aliyeuliwa ametumia vipi freewill ya kuamua kuuliwa au kuto kuuliwa?
  2. Upendo wote wa Mungu uko wapi kama hadi mtoto mdogo asiye na hatia yanamfika mabaya na yeye anaacha yafanyike bila kuzuia?
Honestly kwa jinsi ulivyomtetea Mungu umemfanya muuaji wa mtoto asiwe na hatia na mwenye hatia awe ni Mungu

************
Mfano wako wa mzazi kum-refer na Mungu ni irrelevant

Kwasababu mzazi hana uwezo wote wa kumfanya mtoto aishi katika njia ya kumpendeza yeye.

Na ndio maana anakuwa mkali pale anapoona mtoto hafanyi kila anachokitaka yeye, huyu mzazi hana namna nyingine ya kumfanya mtoto aishi katika misingi ambayo anaitaka yeye bila mafunzo ambayo nayo sio effeciency na ndio maana hufikia hatua ya kumuadhibu kwasababu hana mbadala

***********
Umesema Mungu alishajua yote kabla hayajatokea lakini anaendelea kuwa onya msifanye vitu fulani, anatuma mitume ili msifanye vitu fulani shortly he still expecting something new to his creatures

Yani anaelewa utaua mtoto asiye na hatia, na kuelewa kwake lazima kutimie kwa asilimia zote

Lakini bado anakuonya kuwa usiue

Je mtu huyo anauchaguzi wa kusikia onyo hilo na kuamua kutoua?

Hiyo ndio Logical fallacy ambayo lazima utaiangukia kipindi unamtetea Mungu kwa kujaribu kui solve problem of evil

*****************
Umesema freewill lazima ihusishe mabaya bila mabaya hakuna freewill

Kwamba una maanisha Mungu hausiki na mabaya bali mabaya yanatokana na uchaguzi wa watu kupitia freewill waliyopewa?

Kama watu hufanya kile ambacho Mungu kawaumba waweze kufanya kwanini waadhibiwe kwa hicho ambacho Mungu kawaumba waweze kufanya?

Kama Mungu aliweza kujua kuwa hiki kijusi kitazaliwa nakuwa mtoto, kitakuwa, na kuwa muuaji mkubwa na Mungu akaendelea kukiruhusu kiendelee kuishi tumboni na kuki support hadi katika hatua za kuazaliwa mpaka kikue kufikia utu uzima, kisha mtu huyo aanze utekelezaji wa hayo mauaji.

Sasa kwanini tena mtu huyo aadhibiwe kwa kile aambacho Mungu alimuumba aje akifanye?

Kama huo ulikuwa ni uchaguzi wa mtu kuua je hiyo haikuwa uchaguzi wa Mungu kuumba kiumbe chenye kuchagua uovu?

Ngoja nikupe mfano

Mimi ni mfanya biashara ninaye endesha maduka mawili katika eneo moja hapa mjini. Duka langu moja linajihusisha na uuzaji wa silaha na lingine linajihusisha na maswala ya kimichezo

Kwa bahati nikatembelewa na mtu wangu naye mjua anaitwa Calvin, Calvin akataka kununua silaha nzito ila akanieleza kuwa anachukizwa na hao mabinti waliopo kwenye duka langu la michezo na kwa hivyo basi anaenda kuwafundish adabu

Calvin akaniomba nimuuzie package ya risasi kwa ajili ya silaha, nikamuuzia

Calvin akasema anaenda kuua watu wote waliopo katika eneo hilo, nikamuambia usifanye hivyo. Nikamuambia ni jambo baya sana hutakiwi kufanya

Calvin akaniambia nimfundishe namna ya ku shoot silaha, nikamfundisha

Nikamuonya tena kuwa hupaswi kwenda kutumia hii silaha ku shoot watu

Calvin akatoka na slaha na kwenda kuua kila mtu aliyekuwepo kwenye lile duka linalo jihusisha na michezo

Polisi walivyokuwa wakinihoji nikawasimulia stori nzima ilivyokuwa na nikiwaambia kuwa sio kosa langu ila ni Calvin alikuwa na freewill na nilimuonya asifanye hivyo.

Watu wengi wangeniwajibisha kwa ku-base tu kwenye yale yaliyokuwa sawa kufikiri kwamba Calvin angefanya kutokana na yale ambayo Calvin aliyosema kabla ya kuondoka kwenye duka langu.

Kama nawajibika kwenye sehemu ya mauaji, vipi kuhusiana na Mungu ambaye alimpa Calvin maisha akijua kwa hakika nini Calvin ataenda kufanya kwenye hayo maisha?

Mimi nilijua kidogo tu nini Calvin angeenda kufanya kupitia silaha niliyomuuzia

Mungu alijua kwa hakika na anaweza kuzuia chochote. Au vinginevyo Mungu hakujua, au Mungu hana uwezo wote
 
Hayo ni maneno bila uthibitisho kamanda thibitisha kama Mimi niliumbwa na Mungu,
Lete fact na scientific method alizotumia kuniumba Ili kuprove uumbaji wake!
Kwa hiyo ni nani aliyechanganya maji maji ya mama yako na baba ukapatikana wewe
Tutajie tumjue

Kama baba yako anaitwa John basi wewe mbele ya Mungu sio chochote isipokuwa ni shahawa za John

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo ni nani aliyechanganya maji maji ya mama yako na baba ukapatikana wewe
Tutajie tumjue

Kama baba yako anaitwa John basi wewe mbele ya Mungu sio chochote isipokuwa ni shahawa za John

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Lete Ushahidi wa Mungu kuniumba ACHA janja janja kamanda,
Prove Kwa fact na scientific method juu ya uhusika wa Mungu katika uumbaji wangu,
Nje ya Hapo sitaweza kukubaliana na hearsay aisee!
 
Wapi umemjibu hili.?

Wewe unatoa maelezo kwa fikra zako na unahisi ushajibu mtu_ yani kwa ufupi unahubiri badala ya kujibu unachoulizwa

Usiwe msumbufu kama Allah wako asiyekuwepo
Poa.
 
Mungu mjuzi wa yote ambaye anaweza kujua yaliyo mbele ya wakati kabla hayajatokea hana sababu ya kutoa adhabu

Mungu kaona mtu huyu ataenda kuua mtoto asiyekuwa na hatia

Na wakati huo ana uwezo wa kudhibiti tukio hilo lisifanyike

Na anasababu ya yeye kudhibiti kwasababu kwanza hilo tukio halimpendezi lakini ni mwenye upendo wote
Napowaambia muwe mnajibu maswali yangu, nina maana kubwa sana,haya unayo andika yasingetokea. Ona unavyozidi kudhihirisha ujinga wako.

Anatoa adhabu sababu amekupa uhuru wa kuchagua, na akakwambia ukifanya ovu utalipwa kadha na ukifanya jema utalipwa kadha.

Unapo enda kuua unafanya kwa hiari yako au unalazimishwa sasa kwanini wewe mwenyewe usifanye ?
Ukisema kwamba Mungu kamuacha mtu huyo aue mtoto asiye na hatia ili kuonesha amempa mtu freewill ya kufanya atakalo.

Kutakuwa kuna mambo mawili
  1. Mtoto aliyeuliwa ametumia vipi freewill ya kuamua kuuliwa au kuto kuuliwa?
  2. Upendo wote wa Mungu uko wapi kama hadi mtoto mdogo asiye na hatia yanamfika mabaya na yeye anaacha yafanyike bila kuzuia?
Honestly kwa jinsi ulivyomtetea Mungu umemfanya muuaji wa mtoto asiwe na hatia na mwenye hatia awe ni Mungu
Wewe uliamua uzaliwe au uwe hai ? Jibu hapana, hapa namaanisha mtu hawezi kuamua kuuliwa bali ana uwezo wa kujitetea

Kwahiyo aliyeua ana pata madhambi na ataadhibiwa sababu alikuwa na uwezo wa kujizuia.

Upendo wa Allah uko pale ambapo atakuja kuwalipa hao stahiki zao, muuaji na aliyeuliwa, na mpaka mtoto anakufa ujue ni muda wake wa kifo umefika ndiyo maana kafa, ila kuuliwa ni sababu.
Mfano wako wa mzazi kum-refer na Mungu ni irrelevant

Kwasababu mzazi hana uwezo wote wa kumfanya mtoto aishi katika njia ya kumpendeza yeye
Mfano wangu upo sahihi kwa kukusudia maana. Mola ana huruma na ana mapenzi na mwanadamu ana huruma na mapenzi, tofauti viwili hivyo kwa Allah ni kamili. Naongelea mzazi kumkanya mtoto na kumkosoa. Ukisema hivyo maana yake wewe hukosoi au hukanyi ?
Na ndio maana anakuwa mkali pale anapoona mtoto hafanyi kila anachokitaka yeye, huyu mzazi hana namna nyingine ya kumfanya mtoto aishi katika misingi ambayo anaitaka yeye bila mafunzo ambayo nayo sio effeciency na ndio maana hufikia hatua ya kumuadhibu kwasababu hana mbadala
Na Allah huwa mkali na kuchukizwa pindi mja wake anapomuasi.

Kwahiyo mfano wangu ni mahsusi kabisa.
Umesema Mungu alishajua yote kabla hayajatokea lakini anaendelea kuwa onya msifanye vitu fulani, anatuma mitume ili msifanye vitu fulani shortly he still expecting something new to his creatures

Yani anaelewa utaua mtoto asiye na hatia, na kuelewa kwake lazima kutimie kwa asilimia zote

Lakini bado anakuonya kuwa usiue

Je mtu huyo anauchaguzi wa kusikia onyo hilo na kuamua kutoua?

Hiyo ndio Logical fallacy ambayo lazima utaiangukia kipindi unamtetea Mungu kwa kujaribu kui solve problem of evil
Wapi Allah amesema anatarajia mapya au kwa akili gani ione hilo kwa Allah, hapa unasema wewe.

Mimi na wewe hatujui ila yeye anajua, na kujua kwake hakukuzuii wewe usifanye unachotaka.

Shida yako hujibu madwali yangu, ona sasa umeuliza swali mfano lile nililo kuuliza huko juu. Muuaji angetaka asiue asinge ua, alifanya hivyo kwa hiari yake, huenda kuna hali ilikuwa ina mwambie usifanye hivyo lakini akapingana nayo.

Nakuja kuendelea hapa nilipo ishia...
 
Thibitisha Mungu yupo, na kwamba hizo habari za kuwepo kwa Mungu si hadithi za kusadikika zilizotungwa na watu tu.

Twende pointi moja bada ya nyingine katika uthibitisho wako.
Mwingine huyu hapa!! miaka nenda rudi ni hivihivi tuu!!! ...waache wamuabudu kwani inakupunguzia nini??mpaka udhibitishiwe???Kumbuka imeandikwa ''Imani si Mali ya kila mtu!!...na wala si kila aniitaye Bwana Bwana ataingia ktk ufalme wa mbinguni!!

Duniani wapo wanadamu wa aina mbili tu! Ulijue hilo na uliweke moyoni nao ni.....

1'Wale waliotokana na Mungu mwenyewe mfano mzuri na rahisi ni ABEL! alikufa!
na
2; wale wa kizazi cha nyoka waliotokana na Nyoka yaani shetani!! mfano Cain-aliishi! na Mungu kamuwekea alama! na katika familia nyingi mambo yako ivoivo!! mfano kuna mitoto mingine ni lugumya sana, halishikiki...shule halitaki ni mikorofi balaa japo Baba yao! ana hela, Mali na mauwezo karibu yote! hasa wa kwanza wa kiume! chunguza uone!

na hii ni kutokana na ukweli kwamba Mwanamke Ni Mama wa viumbe vyote!.... Jua kuwa hii ilitamkwa kwa kinywa cha Mungu tu....na so kuna wa kizazi cha nyoka na kizazi cha Mungu!

Kizazi cha nyoka bana yaani mpaka leo kina dhidhirika wazi hawa hawaelewagi neno la uzima tangu zama mpaka leo hii napoongea hapa! hata kwa nyundo!! na hii ilijidhhirisha tangu kwa Esau hadi kwa mwanae Mfalme Daudi.... mwanae Abosalomu alitaka kumuua Baba yake!

na UKIja maisha ya kileo mara nyingi uzao wa kwanza watoto wa kiume ktk familia nyingi ni uzao wa nyoka hawa wanatabia za ki wenge san!! a hawa jamaa hawafanikiwagi kimaisha... ila wapili wa kiume ni kama Malaika na wanakuwaga na akili sana!mafanikio sana na wananyanyua familia zao! Mfano ni Nyerere!! kaka yao mkubwa dorororr!!

Kwa hiyo kizazi cha nyoka kupitia Cain kipo humu Duniani mpaka kesho!! hawa hata uwapigie ngoma gani hawatajuwa uwepo wa Mungu wa kweli! na hawa wakichagua uchawi /Ulozi wana fanikiwaga sana! wana kipaji maeneo haya sana! sana!

lkn wapo wanaishi na sisi!! .......kuna kizazi cha Sethi humu Duniani hawa bana wanaongea na Mungu kma kugusa tu hivi mpaka leo.....na ndo ma-Pastor wa ukweli hao! hawa paradiso inawasubiri kwa hamu!

wakimaliza kazi walizo tumwa na Mungu!!... Mungu ana watwaa kiulainiii mpaka sasa! anafanya ivo! hili nalo huoni kweli? hao wamo humu Duniani ila kwa kuwa weye u kizazi tofauti na wao!! hao hutawajua kamwe! wala kusikia japo una macho!!

Kwa hiyo Mungu wa ukweli hadhi bitishwi na Mwanadamu! mwenye damu na nyama!!! tangia leo elewa hilo!!......atajidhihirisha mwenyewe kwa wkt wake na Majira yake ktk maisha yako km akipenda! ndo tabia yakeee sasa je!

ajabu sasa wala hujawahi jua kwamba yule mwamba hapangiwi na mwanadamu! usitake weye kama weye kudhihirishiwa uwepo wa Mungu na Mwanadamu wa kawaida utasubiri sana Bro! ...ila vuta subira kijana haraka ya nini?????

kwa kuwa imeandikwa kuwa na nukuu ''Kila ulimi utakili ya kwamba yeye ndo...Bwana'' sasa hapo imeandikwa na zaidi ni kuwa tumewaimbia weee!! miaka nenda rudi bado huelewi tu?? ndugu?? haaata!!! una taatizo la msingi!! yaani weye ni mulemule hasa!

kwa kushawishi udhirishiwe na mwanadamu ivo Utafika mahali utaona miungu fake imejaa humu tele!! utapotea mazimaa Mungu mwenyewe anajua na kawataja kabisaaa kuwa kuna miungu tena mingi tu!! kama ile ya wafilist!! Farao wa Misri!!

na hata leo kuna miungu mingi tu tena live!! kwa mfano kuna mungu wa jiwe Rais wenu mfu yule! ..... mungu wa vatican yeye huyu ni mzungu! na mwanae ni Mzungu Blondy mweupeee!! jua kuwa km humjui Mungu wa Ibrahim, Isack na Jacob baaaasi

hapo weyey utakuwa kizazi cha upande wa pili!.......kwa nukuu za Biblia zinasema kondoo walio wake wanamjua mchungaji wao!! hapa wakilinganishwa na wanyama kondoo kuwa hao wanyama wanamjua mchunga wao na ukiangalia hii hekima ni kweli!

kuna miungu Kadhaa inaishi mpakaleo inayo jifanya kam yeye na ina uwezo kwa wanao iamini, Mfano ni mungu Baal!.. Isis....sasa ukilazimisha uthibitisho wa kumuona Mungu wa kweli ni wazi utawaona kina mungu Baal!.......

sasa nikuulize hivi km Mungu hayupo km unavo dhania ? Negativisms dhidi ya Mungu wa kweli zipo tele tena mitaani humo! za nini? au nazo je huzijui kweli? kijana acha utani bana? mfano

wachawi nao si wamejaa mitaani! huwajui kweli??......Majini je?? huyaoni kwani.....wenye husuda wivu, chuki, wezi vibaka waganga huwajui..... km haya yoote huyajui na yalikuwepo na yapo eti hujawahi kuyaona basi jua kabisa una tatizo la Msingi!

hasa upo kwenye kundi hilo la kizazi cha pili hapo juu! Ukiona nguvu hasi jua kuna nguvu chanya pia... na hizi zipo live ktk maisha ya kila siku ya mwandamu naya sema kukufungua akili kijana!

Sikulaumu kuwa hujui uwepo wa Mungu wa kweli ila jua kabisa kuna unae mtumikia na kumuamini bila kujijua siku inakuja atajidhirisha kwako dakika sifuri tu! lkn pia una mahali pako/penu pameandaliwa ajili yenu!!

wala usiwe na wasiwasi!!! usihangaike kuthibitishiwa na Mwanadamu uwepo wa Mungu wa kweli!

Hapo utasubiri sana!...na hutapata Majibu sahihi!! amini nakwambia na haijawahi kutokea Mwanadamu akadhihiri shia walio kizazi cha nyoka uwepo wake hayo ni mawazo yako butu tu!! ni bora uka fanya kazi nyingine!!!

hili jambo lilikuwepo tangu zama na zama! tena hililako wewe cha mtoto tu!! lkn wenzako ilikuwa hivi hivi japo kuwa Mungu alijitokeza wazi ktk maisha yao wao!! lkn walihoji uhalali wa hilo!!

Mfano mzuri ni kulee Kanesh Bernea!!! Kora na wenzake walikuwa na michezo michezo kama yako hii !!Lool!! wali ipata fresh! sasa ndo km weye! unavo fanya mizaha ya kutaka kudhihirishiwa na watu! Nimesema usikie km una masikio!! usifanye moyo wako mgumu!
 
Kwani wapi nimekataza mtu kuabudu?
 
Mungu yupo kwa sababu;
1.Katika maisha yangu nimeshaona wachawi .Wachawi wanafanya uovu hivyo lazima wamtumikie anayewatuma(shetani) hence logically wapo watenda mema wanaomtumikia Mungu.
2.Hakuna asiyeamini Mungu.Wale believers wa big bang theory Mungu wao ni hydrogen atoms zilizofanya collision 💥 na kuunda galaxy.Katika dini Mungu anaweza kuongea n.k.Hivyo chagua Mungu wako ni yupi either hydrogen atoms zilizokuwepo as supernatural or Mungu wa kwenye dini.

NB to atheists:mnasema hakuna Mungu,basi elezea chanzo cha dunia.Kama ni big bang theory,nani aliumba hydrogen atoms.Kama hydrogen atoms hazikuumbwa hence zilikuwepo supernaturally basi hydrogen atoms ndiyo Mungu wenu.
All scientific pioneers who tried to find origin of universe never disbelieved in God.
#Albert Einstein
#Edwin Hubble
#Stephen Hawking n.k
 
Napowaambia muwe mnajibu maswali yangu, nina maana kubwa sana,haya unayo andika yasingetokea. Ona unavyozidi kudhihirisha ujinga wako.

Anatoa adhabu sababu amekupa uhuru wa kuchagua, na akakwambia ukifanya ovu utalipwa kadha na ukifanya jema utalipwa kadha.

Unapo enda kuua unafanya kwa hiari yako au unalazimishwa sasa kwanini wewe mwenyewe usifanye ?

Wewe uliamua uzaliwe au uwe hai ? Jibu hapana, hapa namaanisha mtu hawezi kuamua kuuliwa bali ana uwezo wa kujitetea

Kwahiyo aliyeua ana pata madhambi na ataadhibiwa sababu alikuwa na uwezo wa kujizuia.

Upendo wa Allah uko pale ambapo atakuja kuwalipa hao stahiki zao, muuaji na aliyeuliwa, na mpaka mtoto anakufa ujue ni muda wake wa kifo umefika ndiyo maana kafa, ila kuuliwa ni sababu.

Mfano wangu upo sahihi kwa kukusudia maana. Mola ana huruma na ana mapenzi na mwanadamu ana huruma na mapenzi, tofauti viwili hivyo kwa Allah ni kamili. Naongelea mzazi kumkanya mtoto na kumkosoa. Ukisema hivyo maana yake wewe hukosoi au hukanyi ?

Na Allah huwa mkali na kuchukizwa pindi mja wake anapomuasi.

Kwahiyo mfano wangu ni mahsusi kabisa.

Wapi Allah amesema anatarajia mapya au kwa akili gani ione hilo kwa Allah, hapa unasema wewe.

Mimi na wewe hatujui ila yeye anajua, na kujua kwake hakukuzuii wewe usifanye unachotaka.

Shida yako hujibu madwali yangu, ona sasa umeuliza swali mfano lile nililo kuuliza huko juu. Muuaji angetaka asiue asinge ua, alifanya hivyo kwa hiari yake, huenda kuna hali ilikuwa ina mwambie usifanye hivyo lakini akapingana nayo.

Nakuja kuendelea hapa nilipo ishia...
Unasema anatoa adhabu kwasababu amekupa uhuru wa kuchagua na akakwambia ukifanya ovu utalipwa kadha na ukifanya jema utalipwa kadha.

Hoja yangu ni kwamba katika jambo ambalo huyu Mungu aliliona kabla halijatokea kuwa kiumbe huyu ataenda kulifanya, jambo hilo ambalo halimpendezi yeye. Hicho kiumbe kinaweza kufanya namna yeyote na kwenda tofauti na maono ya Mungu kwa kutotenda hayo mabaya?

Mungu anamuadhibu huyo mtu kwa vigezo gani? kwamba huyo mtu alikuwa mkaidi na kiburi kwa kushindwa kupita njia sahihi?

Kwamba Mungu aliamini huyo mtu alikuwa ana nafasi ya kubadilika na kwenda kinyume

Adhabu ya Mungu kwa mtu huyo inaonesha dosari katika dhana ya freewill, freewill ni kufanya maamuzi bila kuingiliwa au kuwekewa vikwazo. Adhabu inaonesha kuwa mtu huyo hayuko huru na ndio maana asipofanya yale ambayo amelazimishwa kufanya atapewa adhabu

Ebu fikiria. Kama Mungu kamuumba binadamu afanye maovu akijua kabisa kuwa watu hao wataenda kuchagua kufanya maovu, huoni nafasi ya Mungu kuwajibika kwenye uovu huo?

Fikiria kuwa Mungu ni mjuzi wa yote, anayajua yote ya mbele kabla hayajatokea. Mungu katuambia mimi na mke wangu kuwa tutaenda kupitia mlango namba 6 tutazaa mtoto ambaye atakuja kuua watu milion 1

Mimi na wife tumesikia Mungu alichotuambia huku tukijua kuwa Mungu anajua ya mbele kabla hayajatokea, kisha tukapita kutumia mlango namba 6 na tuapata mtoto ambaye alivyokuwa akaja kuua watu milion 1

Je mimi na mke wangu tutawajibika kwa vifo vya hao watu kwa namna yeyote?

Tuliweza kupita mlango namba 1 au mlango namba 2 au namba 7 lakini tukachagua mlango namba 6 baada ya kujua nini kitatokea kama tukipita mlango namba 6

Kama kwa namna yeyote tutakuwa responsible kwa vifo hivyo, je vipi kwa Mungu ambaye anajua zaidi halafu akachagua kuruhusu mimba ya huyo mtoto ikue katika hali ya kiusalama mpaka atakapozaliwa huyo mtoto na kuja kuwa muuaji wa watu milion 1?
 
Wewe uliamua uzaliwe au uwe hai ? Jibu hapana, hapa namaanisha mtu hawezi kuamua kuuliwa bali ana uwezo wa kujitetea

Kwahiyo aliyeua ana pata madhambi na ataadhibiwa sababu alikuwa na uwezo wa kujizuia.
Sikuweza kuamua kuzaliwa au lah kwasababu hakuna freewill

Kutokuamua kwa watu kufanya yale wayatakayo ni ushahidi tosha kuwa watu hawako huru

Mtoto wa miezi mitatu tumboni kwa mama yake anauwezo wa kujitetea kutokufa pindi mama yake akitaka kumuua kwa kuitoa mimba?
 
Upendo wa Allah uko pale ambapo atakuja kuwalipa hao stahiki zao, muuaji na aliyeuliwa, na mpaka mtoto anakufa ujue ni muda wake wa kifo umefika ndiyo maana kafa, ila kuuliwa ni sababu.
Hapa ndio unaniacha highway

Sasa kama mtoto kuuliwa na muuaji maana yake siku zake zilikuwa zimefika, huoni kwamba hiyo ni hatma ambayo Mungu ndio alimuandikia?

Huoni kwamba muuaji ni kama mtekelezaji aliyetumika na Mungu kukamilisha mpango huo?

Sasa kivipi tenamtu huyo kwa kutekeleza mpango wa Mungu ahukumiwe?

Kwa mantiki hiyo huoni kwamba huyu mtekelezaji wa hayo mauaji kupitia mpango wa Mungu katika kufikia hatma ya huyo mtoto, ilipaswa apewe pongezi kwa kukamilisha kazi hiyo?
 
Mfano wangu upo sahihi kwa kukusudia maana. Mola ana huruma na ana mapenzi na mwanadamu ana huruma na mapenzi, tofauti viwili hivyo kwa Allah ni kamili. Naongelea mzazi kumkanya mtoto na kumkosoa. Ukisema hivyo maana yake wewe hukosoi au hukanyi ?
Sio kweli kuwa mzazi anaupendo wote na bado sio sawa kutumia mfano wa mzazi kumlinganisha na Mungu ambaye ana sifa nyingi ambazo ni kuu

Mungu ana huruma, lakini karuhusu mabaya.... hiyo ni contradiction

Mzazi kumkosoa mtoto ni moja ya kuonesha mapungufu ya mzazi, mzazi ana wish jambo fulani ambalo anaona ni bora lifanyike ili kumfanya mwanae aishi katika mstari ambao utamfurahisha mzazi lakini kwa bahati mbaya uwezo huo hana

Na hapo ndipo anajikuta anakuwa mkali na kumuadhibu mtoto vibaya ambapo kuna muda hadi anajutia kufanya maamuzi hayo kwa mtoto lakini he ran out of option

Je naye Mungu ana wish binadamu wafanye mazuri ya kumpendeza ili asiwachome moto lakini hana option ya kuwafanya wawe hivyo anavyotaka?
 
Na Allah huwa mkali na kuchukizwa pindi mja wake anapomuasi.

Kwahiyo mfano wangu ni mahsusi kabisa.
Mungu anakuwaje mkali kwenye tukio ambalo aliliona miaka 30 iliyopita huku akijua huyo mtu huyo hawezi kuepuka bila yeye kufanya juhudi za kumuepusha?
 
Umesema freewill lazima ihusishe mabaya bila mabaya hakuna freewill

Kwamba una maanisha Mungu hausiki na mabaya bali mabaya yanatokana na uchaguzi wa watu kupitia freewill waliyopewa?

Kama watu hufanya kile ambacho Mungu kawaumba waweze kufanya kwanini waadhibiwe kwa hicho ambacho Mungu kawaumba waweze kufanya?
Uhuru wa kufanya matendo unajumuisha yote mazuri na mabaya.

Mola ameumba mabaya ila ametukataza tusifanye na akatupa uwezo wa kuyaepuka mabaya hayo.

Wana adhibiwa sababu wamepewa uhuru na wakaambiwa usifanye mabaya na ufanye mazuri na tukaambwa ubaya wa kufanya maovu na kuambiwa uzuri wa kufanya mema. Swali, sasa kwanini ufanye mabaya ?
Kama Mungu aliweza kujua kuwa hiki kijusi kitazaliwa nakuwa mtoto, kitakuwa, na kuwa muuaji mkubwa na Mungu akaendelea kukiruhusu kiendelee kuishi tumboni na kuki support hadi katika hatua za kuazaliwa mpaka kikue kufikia utu uzima, kisha mtu huyo aanze utekelezaji wa hayo mauaji.

Sasa kwanini tena mtu huyo aadhibiwe kwa kile aambacho Mungu alimuumba aje akifanye?
Uwe unajibu maswali, huyo mtu anapo fanya hilo jambo anakuwa amekusudia au kwa hiari yake ? Yaani kujua kwake Allah hakufungamani na wewe kutenda.
Kama huo ulikuwa ni uchaguzi wa mtu kuua je hiyo haikuwa uchaguzi wa Mungu kuumba kiumbe chenye kuchagua uovu?
Na akaumba kiumbe ambacho kinaweza kuacha kufanya mabaya, yaani yote ameumbwa nayo.
 
Mungu anakuwaje mkali kwenye tukio ambalo aliliona miaka 30 iliyopita huku akijua huyo mtu huyo hawezi kuepuka bila yeye kufanya juhudi za kumuepusha?
Amekupa uwezo wa kuepuka.
 
Back
Top Bottom