Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Swali lako lolote linalomtaja Mungu ni lazima lianze kwa kuthibitisha Mungu yupo.

Ili tujue swali si la hadithi za kufikirika tu.

Thibitisha Mungu yupo.
Hii sahihi, sababu maswali yangu yanatokana na mtiririko wa kile unachokielezea. Kwahiyo maswali yangu kwa namna yoyote ile hayakwepeki.

Shukrani.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kuumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya ni contradiction.

Unaelewa hilo?
Hakuna Contradiction hapo. Hili nimekuonyesha na sababu nimekupa.

1. Unakubali kama humjui Mola ? Sasa ajabu upatie vipi kumjadili ?

2. Hujaonyesha "contradiction" yoyote kiuhalisia zaidi ya kucheza na maneno yenye kuthibitisha ya kuwa humjui Mola.
 
Hii sahihi, sababu maswali yangu yanatokana na mtiririko wa kile unachokielezea. Kwahiyo maswali yangu kwa namna yoyote ile hayakwepeki.

Shukrani.
Hujathibitisha Mungu yupo.

Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.
 
Hakuna Contradiction hapo. Hili nimekuonyesha na sababu nimekupa.

1. Unakubali kama humjui Mola ? Sasa ajabu upatie vipi kumjadili ?

2. Hujaonyesha "contradiction" yoyote kiuhalisia zaidi ya kucheza na maneno yenye kuthibitisha ya kuwa humjui Mola.
Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?

Epicurean.jpeg
 
Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?

View attachment 2172429

Huu mchoro unaurudia, jambo hili nilishalijadili sana humu.

Maana ya ujuzi wa yote ni kuzuia na kuruhusu, upendo kamili kuadhibu,kusamehe, kuonya na kutoa matarajio mazuri.

Kiongozi huu mjadala unapoteza maana kwa wewe kukimbia maswali yangu.
 
Nikikuuliza rangi ya pembetatu duara ni rangi gani utajibuje?
Endapo ikiwa naiona hiyo pembe tatu nitakujibu rangi yake kwa kile ninacho kiona, nikiwa siioni nitakembia sijui.

Kiomgozi wangu kama umenisoma nimekuwa "fair" sana, sijawa kama nilivyo kawaida yangu, nakuonyesha kwamba wewe ni mtupu sana hata kama nikibadilisha mbinu na kuwa mpole na kuamua kujibu maswali yako. Unatakiwa ujistukie sasa
 
Nakwambia hivi.

Hujaweza kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Hoja zako za kumtaja Mungu zote zinatakiwa kuanza na uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Ili usije kuleta hoja za hadithi tupu za kutungwa na watu.

Sasa, thibitisha Mungu yupo.

Usilete mambo ya imani kukariri sijui Mungu hivi, Mungu vile.

Uthibitisho kuwa Mungu yupo ni kitendo cha wewe kuwepo hapa duniani Leo hii Mungu ndio aliyekuleta

Sasa kama wewe haujaletwa na Mungu hapa duniani basi yupo aliyekuleta tutajie ni nani pia weka ushahi au kama umejileta mwenyewe pia weka ushahidi ili tujuwe kuwa hakuna Mungu
 
Walionileta hapa ni baba na mama yangu.

Sasa baba na mama yangu ni Mungu?

Na hata ukitaka kwenda mbali zaidi, unajuaje suala ni la "nani" na si nini?

Umekuta jani la muembe mlangoni mwako, hujui limefikaje, badala ya kuuliza jani limefikaje hapo, unauliza nani kaweka jani hapo.

Kama limewekwa na upepo huoni swali lako la nani litakuwa la makosa?

Wewe unaelewa kwamba dhana nzima ya "hiki kimeanzishwa na kile" ukiifuqtilia sana kwenye fizikia inavunjika?

Unaelewa kwamba kwenye level ya quantum mechanics, chqnzo kinaweza kutokea baada ya matokeo na matokeo yakatokea kabla ya chanzo katika mduara usiomalizika?

Unaelewa kwamba muda wenyewe, unaotupa dhana nzima ya kipi kinaanza na kipi kinafuatia, ukiufuatilia sana unavunjika?

Unaelewa "logical non sequitur" ni nini?

Wewe kusema kwamba mimi kuwapo kwangu ni uthibitisho kwamba Mungu yupo, hakuthibitishi uwepo wa Mungu.

Umeandika tu hilo, hujathibitisha ni vipi Mungu kasababisha mimi kuwapo.

Umeeleza jambo la imani.

Imani si uthibitisho.

Mimi naweza kukuambia naamini mimi ndiye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Imani hiyo hainifanyi niwe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Thibitisha Mungu yupo, usitoe kauli za imani tu zilizojaa logical non sequitur.
 
kufanya maelezo marefu yawe mafupi naomba unithibitishie Mungu yupo
Shabaha yangu ilikuwa ni kukusaidia kupata majibu ya maswali yako yahusuyo FREE WILL na DIVINE DECREE tu na si vinginevyo, vitabu nilivyogusisha kwenye convo umevisoma au umepata muda wa kuanza kuvisoma? je vimesaidia au havijasaidia? vimekuongezea maarifa au havijakuongezea? maswali yako yamejibika au hayajajibika? hujanipa mrejesho wowote kuhusu hilo, cha kushangaza unaonekana kushughulishwa na nachoandika humu ambacho hakijapitiwa, hakijahakikiwa, wala kuidhinishwa na wanazuoni au wabobezi wa hizi fani, ulikuwa na nia ya dhati ya kutafuta majibu ya maswali yako kweli? kama ni kweli ungetumia muda wako kusoma vile vitabu na si kusoma maelezo yangu kisha kuchagua unieleweje - tofauti na ilivyokusudiwa

Unajaribu kunivuta kwenye mjadala ambao sikuukusudia, kwa nini umefanya hivyo? unatakiwa ufahamu kwamba mambo ya aina hii si masuala ya nani ni winner na nani ni losser, haya ni masuala ya nani yupo right na nani yupo wrong, kama tulichowekana sawa awali kilikuingia akilini ungeweza kukausha tu - hakukuwa na ulazima wa kuninukuu na kujaribu kuonyesha watu kama kuna kitu bado sijathibitisha hivi kwenye maelezo yangu - na hali sicho tulichokuwa tunaeleweshana 'specifically' mimi na wewe, kwa upande mmoja ni hivyo, kwa upande wa pili wa utafutaji maarifa kwa heshima kubwa ahsante sana kwa wito

Imani yangu imenifunza adabu za kufanya mijadala yenye tija, vilevile imenifunza kujiepusha na mijadala isiyo na tija, na sisi tunajitofautisha na wale wahadhiri mashuhuri ambao hutumia maneno ya nyimbo za mipasho kujadiliana masuala ya kiroho, misingi yetu haifanani na yao, au yawezekana inafanana kimaandishi lakini kimatendo wao hawaishadadii ipasavyo, hawachungi adabu za 'jidal' au 'minakasha', hayo unatakiwa uyafahamu, kwa mujibu wa misingi yangu binafsi si kila mtu amefuzu kufanya mijadala: siwezi kujadiliana na mtu ambaye macho yake ameyafumbua na masikio yake ameyafungua lakini moyo wake ameufunga 'mertamophically' - watu wa aina hii hawezi kukubali ukweli au haki, na pili siwezi kujadiliana na mtu ambaye hana maarifa ya kutosha kuhusu mada husika - aina ya watu wenye maneno ya aina hii: mimi sijasoma lakini huniambii kitu, na tatu mara nyingi huwa sijadiliani na mtu ambaye nafahamu fika m(i)simamo ali(y)osimamia ni batili na potofu na ameing'ang'ania kwa meno ya magego - na hana hata chembe ya viashiria kuondokana nao, kwa misingi hiyo ningependa kufahamu baadhi ya 'mambo' kabla sijaamua kuingia rasmi kwenye huu mjadala

1. Unahitaji kujadiliana na mimi kwa lengo gani haswa? je ni kupata uongofu, kupinga - kubisha tu, kuongeza maarifa, kutafuta dosari au nini yaani
 
Mpaka hapa hakuna Mtu aliyetuthibitishia uwepo wa Mungu,muumba na mjuzi wa yote,
Nawasitikia sana ndugu zangu waamini wanajipa shida kumtetea kiumbe aliyepo kwenye fikra zao tu na si halisia!
 
Walionileta hapa ni baba na mama yangu.

Sasa baba na mama yangu ni Mungu?

Na hata ukitaka kwenda mbali zaidi, unajuaje suala ni la "nani" na si nini?

Umekuta jani la muembe mlangoni mwako, hujui limefikaje, badala ya kuuliza jani limefikaje hapo, unauliza nani kaweka jani hapo.

Kama limewekwa na upepo huoni swali lako la nani litakuwa la makosa?

Wewe unaelewa kwamba dhana nzima ya "hiki kimeanzishwa na kile" ukiifuqtilia sana kwenye fizikia inavunjika?

Unaelewa kwamba kwenye level ya quantum mechanics, chqnzo kinaweza kutokea baada ya matokeo na matokeo yakatokea kabla ya chanzo katika mduara usiomalizika?

Unaelewa kwamba muda wenyewe, unaotupa dhana nzima ya kipi kinaanza na kipi kinafuatia, ukiufuatilia sana unavunjika?

Unaelewa "logical non sequitur" ni nini?

Wewe kusema kwamba mimi kuwapo kwangu ni uthibitisho kwamba Mungu yupo, hakuthibitishi uwepo wa Mungu.

Umeandika tu hilo, hujathibitisha ni vipi Mungu kasababisha mimi kuwapo.

Umeeleza jambo la imani.

Imani si uthibitisho.

Mimi naweza kukuambia naamini mimi ndiye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Imani hiyo hainifanyi niwe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Thibitisha Mungu yupo, usitoe kauli za imani tu zilizojaa logical non sequitur.
Quran 35:11.
Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii.

Quran 23:14.
Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.

Utaelewa tu shahawa za baba yako zilizochanganyika na yai la mama yako hadi ukatokea wewe Mungu ndio aliyezitengeneza

Sasa kama baba yako shahawa zake zilizofanya wewe uje duniani alizitengeneza mwenyewe kwa ujuzi wake weka ushahidi

Pia yai la mama yako lililofanya wewe uje duniani alilitengeneza mwenyewe kwa ujuzi wake mwenyewe weka ushahidi
 
Thibitisha Mungu yupo kweli na kwamba habari za kuwapo kwake si hadithi za watu tu.

Hili ndilo swali langu la msingi ambalo mpaka sasa halijathibitishwa.

Tafadhali usilete mambo ya imani na mapokeo fyongo.

Nataka uthibitisho wa kimantiki.
 
Nina wasi wasi na uwelewa wako

Nilikuwambia uthibitisho kuwa Mungu yupo ni kitendo cha wewe kuwepo hapa duniani maana Mungu ndio aliyekuleta

Ukasema wewe hapa duniani umeletwa na baba yako na mama yako

Nikakuambia kama umeletwa na baba yako na mama yako weka ushahidi kuwa

Shahawa za baba yako zilizotumika kukuumba wewe baba yako alizitengeneza mwenyewe kwa ujuzi wake

Pia weka ushahidi kuwa yai la mama yako lililotimika kukuumba wewe alilitengeneza mama yako mwenyewe kwa ujuzi wake

Weka ushahidi ili tuendelee mbele na kama huna huo ushahidi sema maana ukisha jibu hayo yatafuata maswali mengime mengi tu

1) hi duniani unayoishi imetengenezwa na nani?

2) Jua ambalo lina mchango mkubwa katika maisha yako ya hapa duniani limetengenezwa na nani?

3) vyakula unavyokula Samaki, nyama ,nafaka ,matunda na majani vimetengenezwa na nani?

Maana naamini kama unapinga hayo yote hayajatengenezwa na Mungu basi lazima utakuwa unamjua aliyetengeneza
 
Unasema shahawa za baba yangu alizitengeneza Mungu.

Unaweza kuthibitisha hili?

Kuuliza swali "Dunia imetengenezwa na nani" si uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Kwanza kwa nini swali liwe "na nani"?

Unajionesha kwamba huwezi kufikiri kidhahania nje ya ku personalize vitu.

Umekuta jani la muembe mlangoni kwako, unauliza, jani hili limewekwa hapa na nani?

Unajuaje swali sahihi ni "na nani" na si "na nini"?

Kama jani limewekwa hapo na upepo, huoni kwamba swali la "hili jani limewekwa hapa mlangoni na nani" ni swali lisilo sahihi?

The same applies kwa maswali yako namba 2 na 3.

Siyo tu huna majibu sahihi.

Hata maswali sahihi huyajui!
 
Unasema shahawa za baba yangu alizitengeneza Mungu.

Unaweza kuthibitisha hili?

Kuuliza swali "Dunia imetengenezwa na nani" si uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Kwanza kwa nini swali liwe "na nani"?

Unajionesha kwamba huwezi kufikiri kidhahania nje ya ku personalize vitu.

Umekuta jani la muembe mlangoni kwako, unauliza, jani hili limewekwa hapa na nani?

Unajuaje swali sahihi ni "na nani" na si "na nini"?

Kama jani limewekwa hapo na upepo, huoni kwamba swali la "hili jani limewekwa hapa mlangoni na nani" ni swali lisilo sahihi?

The same applies kwa maswali yako namba 2 na 3.

Siyo tu huna majibu sahihi.

Hata maswali sahihi huyajui!
Quran 35:11.
Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii.

Quran 86:5.
Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?

6.
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,

7.
Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.

Hayo maandiko ndio uthibitisho wangu kuwa shahawa za baba yako zilizokufanya wewe uje hapa duniani na kujifanya unajua sana hadi kufikia kukana uwepo na uwezo wa Mungu

Weka na wewe uthibitisho wako kuwa shahawa za baba yako amezitengeneza baba yako mwenyewe au hata kama zimetengenezwa na kibwengo weka ushahidi tumjue

Na pia kama wewe ni mjinga na mbumbu yani haumjui aliyetengeneza shahawa za baba yako zilizokufanya uje hapa duniani pia sema
 
Unasema tu kasema hivi, kasema vile.

Nikikwambia thibitisha yupo, unarudia kasema hivi, kasema vile.

Thibitisha Mungu yupo, usihubiri.

Kuhubiri si uthibitisho.
 
Utajijua tu kuwa we we ni tahira

Nikuthibitishie Mara ngapi wakati nimesha kuthibitishia kuwa Mungu yupo katika post 336

Ngoja nikukumbushe kama umesahau ile post

Nilikuwambia uthibitisho kuwa Mungu yupo ni kitendo cha wewe kuwepo hapa duniani maana Mungu ndio aliyekuleta

Ukasema wewe hapa duniani umeletwa na baba yako na mama yako

Nikakuambia kama umeletwa na baba yako na mama yako weka ushahidi kuwa

Shahawa za baba yako zilizotumika kukuumba wewe baba yako alizitengeneza mwenyewe kwa ujuzi wake

Pia weka ushahidi kuwa yai la mama yako lililotimika kukuumba wewe alilitengeneza mama yako mwenyewe kwa ujuzi wake

Wewe ndio uthibitisho wangu physically kabisa kama Mungu yupo sasa ili hu uthibitisho wangu uwe batili weka na wewe uthibitisho wako kuwa wewe haujaletwa na Mungu hapa duniani na ututajie alikuleta

Hauna jipya
Kwanza mtafute aliyekuleta duniani ukisha mjua ndio urudi hapa tufanye discussion kuwa Mungu yupo au hayupo

Siwezi kudiscus na mtu uwepo wa Mungu wakati yeye mwenyewe hatu hamjui aliyemleta hapa duniani
 
Back
Top Bottom