Mungu mjuzi wa yote ambaye anaweza kujua yaliyo mbele ya wakati kabla hayajatokea hana sababu ya kutoa adhabu
Mungu kaona mtu huyu ataenda kuua mtoto asiyekuwa na hatia
Na wakati huo ana uwezo wa kudhibiti tukio hilo lisifanyike
Na anasababu ya yeye kudhibiti kwasababu kwanza hilo tukio halimpendezi lakini ni mwenye upendo wote
Ukisema kwamba Mungu kamuacha mtu huyo aue mtoto asiye na hatia ili kuonesha amempa mtu freewill ya kufanya atakalo.
Kutakuwa kuna mambo mawili
- Mtoto aliyeuliwa ametumia vipi freewill ya kuamua kuuliwa au kuto kuuliwa?
- Upendo wote wa Mungu uko wapi kama hadi mtoto mdogo asiye na hatia yanamfika mabaya na yeye anaacha yafanyike bila kuzuia?
Honestly kwa jinsi ulivyomtetea Mungu umemfanya muuaji wa mtoto asiwe na hatia na mwenye hatia awe ni Mungu
************
Mfano wako wa mzazi kum-refer na Mungu ni irrelevant
Kwasababu mzazi hana uwezo wote wa kumfanya mtoto aishi katika njia ya kumpendeza yeye.
Na ndio maana anakuwa mkali pale anapoona mtoto hafanyi kila anachokitaka yeye, huyu mzazi hana namna nyingine ya kumfanya mtoto aishi katika misingi ambayo anaitaka yeye bila mafunzo ambayo nayo sio effeciency na ndio maana hufikia hatua ya kumuadhibu kwasababu hana mbadala
***********
Umesema Mungu alishajua yote kabla hayajatokea lakini anaendelea kuwa onya msifanye vitu fulani, anatuma mitume ili msifanye vitu fulani shortly he still expecting something new to his creatures
Yani anaelewa utaua mtoto asiye na hatia, na kuelewa kwake lazima kutimie kwa asilimia zote
Lakini bado anakuonya kuwa usiue
Je mtu huyo anauchaguzi wa kusikia onyo hilo na kuamua kutoua?
Hiyo ndio Logical fallacy ambayo lazima utaiangukia kipindi unamtetea Mungu kwa kujaribu kui solve problem of evil
*****************
Umesema freewill lazima ihusishe mabaya bila mabaya hakuna freewill
Kwamba una maanisha Mungu hausiki na mabaya bali mabaya yanatokana na uchaguzi wa watu kupitia freewill waliyopewa?
Kama watu hufanya kile ambacho Mungu kawaumba waweze kufanya kwanini waadhibiwe kwa hicho ambacho Mungu kawaumba waweze kufanya?
Kama Mungu aliweza kujua kuwa hiki kijusi kitazaliwa nakuwa mtoto, kitakuwa, na kuwa muuaji mkubwa na Mungu akaendelea kukiruhusu kiendelee kuishi tumboni na kuki support hadi katika hatua za kuazaliwa mpaka kikue kufikia utu uzima, kisha mtu huyo aanze utekelezaji wa hayo mauaji.
Sasa kwanini tena mtu huyo aadhibiwe kwa kile aambacho Mungu alimuumba aje akifanye?
Kama huo ulikuwa ni uchaguzi wa mtu kuua je hiyo haikuwa uchaguzi wa Mungu kuumba kiumbe chenye kuchagua uovu?
Ngoja nikupe mfano
Mimi ni mfanya biashara ninaye endesha maduka mawili katika eneo moja hapa mjini. Duka langu moja linajihusisha na uuzaji wa silaha na lingine linajihusisha na maswala ya kimichezo
Kwa bahati nikatembelewa na mtu wangu naye mjua anaitwa Calvin, Calvin akataka kununua silaha nzito ila akanieleza kuwa anachukizwa na hao mabinti waliopo kwenye duka langu la michezo na kwa hivyo basi anaenda kuwafundish adabu
Calvin akaniomba nimuuzie package ya risasi kwa ajili ya silaha, nikamuuzia
Calvin akasema anaenda kuua watu wote waliopo katika eneo hilo, nikamuambia usifanye hivyo. Nikamuambia ni jambo baya sana hutakiwi kufanya
Calvin akaniambia nimfundishe namna ya ku shoot silaha, nikamfundisha
Nikamuonya tena kuwa hupaswi kwenda kutumia hii silaha ku shoot watu
Calvin akatoka na slaha na kwenda kuua kila mtu aliyekuwepo kwenye lile duka linalo jihusisha na michezo
Polisi walivyokuwa wakinihoji nikawasimulia stori nzima ilivyokuwa na nikiwaambia kuwa sio kosa langu ila ni Calvin alikuwa na freewill na nilimuonya asifanye hivyo.
Watu wengi wangeniwajibisha kwa ku-base tu kwenye yale yaliyokuwa sawa kufikiri kwamba Calvin angefanya kutokana na yale ambayo Calvin aliyosema kabla ya kuondoka kwenye duka langu.
Kama nawajibika kwenye sehemu ya mauaji, vipi kuhusiana na Mungu ambaye alimpa Calvin maisha akijua kwa hakika nini Calvin ataenda kufanya kwenye hayo maisha?
Mimi nilijua kidogo tu nini Calvin angeenda kufanya kupitia silaha niliyomuuzia
Mungu alijua kwa hakika na anaweza kuzuia chochote. Au vinginevyo Mungu hakujua, au Mungu hana uwezo wote